MTUMWA NI NANI?- SEHEMU YA TANO - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Monday, November 12, 2018

MTUMWA NI NANI?- SEHEMU YA TANO


Ninakusalimu katika Jina la Bwana Yesu Kristo wa Nazareti ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na shughuli zako na Mungu anaendelea kukuonesha njia sahihi katika kila kitu ambacho unakifanya, siku hii ya leo ninaomba katika Jina la Yesu Kristo ufunuliwe kwa namna yako hiki ambacho tunajifunza kwa pamoja

Tulipoishia....

Katika nchi za Afrika kuna siku za kuadhimisha watu waliokufa hakuna siku za maombi na toba kwa ajili ya nchi, katika hali kama hii ni vigumu sana kuona baraka za Mungu zikitiririka kwa wananchi, pia tambua ya kwamba jukumu la wazazi wako lilikuwa kukuleta duniani na kukulea, shukuru Mungu kama ulienda shule mengine ni jukumu lako, pambana ndio maana ukapewa akili siyo ya kuombaomba bali ni kufikiri kwa kina na kuja na majibu

Kama hukutengeneza muda wa kujifunza pamoja nasi somo la mtumwa ni nani- sehemu ya nne jana unaweza kuungana nasi kwa ⇒⇒⇒Kubofya hapa kujifunza somo lote!

Tunaendelea....

Leo tunaangalia sifa ya pili ya mtumwa, kama umeokoka na unasumbuliwa na magonjwa wewe ni mtumwa, nianze kwa kusema hivi kuna watu waliompokea Yesu Kristo lakini hawajafahamu nguvu walionayo hivyo wamebakia kuwa Wakristo wasio na nguvu na matokeo yake wameishia kusema Yesu Kristo anaweza wakati maisha yao hayathibitishi hilo na pia wanasumbuliwa na magonjwa

Tufikie hatua ya kile tunachokikiri kionekane kwenye maisha yetu, ninamshangaa sana mtu anayeumwa kuliko asiye na fedha kwa sababu kupona ni rahisi na haraka zaidi kuliko kupata fedha, uponyaji ni papo hapo fedha inahitajika muda fulani kuzipata, kwa nini unaumwa wakati umeokoka?

Ninaomba nikukumbushe alichokiandika nabii Isaya hata kabla ya ujio wa Yesu Kristo, Isaya 53:5 "Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu, Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona" kama Yesu Kristo alifanyiwa yote hayo kwa ajili yako na umemkiri kwa nini unaumwa? Nikupashe habari moja kwamba kama unasumbuliwa na magonjwa na umeokoka wewe ni mwizi la sivyo unieleze umeupata wapi huo ugonjwa wakati Yesu Kristo alishauchukua

Tuache kuwa tunaokiri tuu kwa maneno na moyoni hatuamini kwa sababu ukiamini ni lazima vitu vitatokea maishani mwako, siandiki kukudhihaki kama unasumbuliwa na magonjwa, ila nakuambia ukweli wa Neno la Mungu ndivyo mambo yalivyo kama umempokea Yesu Kristo hapaswi kusumbuliwa na ugonjwa wa aina yoyote ile

Tizama tena 1Petr 2:24 "Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa" magonjwa kwa namna nyingine yaliletwa na dhambi na kama Yesu Kristo aliamua kuutoa uhai wake kwa ajili ya dhambi zako ili achukue magonjwa yako, na wewe ukamkiri kama Bwana na mwokozi wa maisha yako kwa nini unakubali kuumwa?

Nikuambie suala hili kwamba kuumwa angali umeokoka ni kutokujua haki zako na mtu asiyefahamu haki zake ni mtumwa, anza kuona ugonjwa kama dhambi na kitu ambacho hupaswi kabisa kusumbuliwa nacho ndipo hutakaa usumbuke na magonjwa tena, anza kuishi maisha halisi ya wokovu ambao Mungu amekukusudia kama mkristo

Ni ujinga unakufanya uumwe, siku ukifunuliwa hutokaa ukubali kuumwa maana ni uamuzi, Mimi ninaeandika nilishafanya uamuzi kwamba magonjwa siyo sehemu yangu na imekuwa hivyo, naandika tena hapa sitokaa niumwe sababu najua kwa nini Yesu Kristo aliamua kuutoa uhai kwa ajili yangu siitaji kuumwa tena

Nikushirikishe ushuhuda huu mwezi uliopita nilipatwa na wakati mgumu sana, kwa sababu sehemu ya magonjwa hainihusu adui alikuja na njia mpya na hii kweli ilinisumbua nikiri hili, nilisumbuliwa na ndoto moja ya uovu mbaya sana na kama siku tano mfululizo nilikuwa naota ndoto hiyo inajirudia ikafika sehemu naogopa hata kulala, nikabadili ratiba nilale mchana hata mchana ikanirudia tena

Ndoto hii ni mbaya na ovu sana kiasi ambacho sijawahi kumshirikisha mtu ilihusu nini huwa nasema ni ndoto ovu sana, kuna kiwango fulani cha imani ukifika ndoto kama hizi unaweza kuziua kwa maombi na zisirudie tena, siyo kwamba sikuwahi kuota ndoto mbaya kabla niliwahi na nilikuwa naziuwa hapo hapo kwa maombi na hazirudi tena

Lakini mambo yalikuwa tofauti sana katika ndoto hii, niliamka usiku wa manane nikaiuwa pasipo mafanikio, kwa sku kadhaa sikujisumbua kufunga maana najua nikitamka kwa sehemu niliyopo ni lazima mambo yatokee ila hakuna mabadiliko niliyoyaona, ikafika sehemu nikahisi imani yangu imepungua lakini nikasema hapana sijaacha kuomba wala kusoma Neno

Kufupisha habari kuna siku nikaomba mchana kisha nikaenda Kanisani na nilimuambia Mungu leo nipe Neno moja tuu naye akanipatia Warumi 8:37 "Lakini katika mambo hayo yote sisi ni zaidi ya washindi, kupitia kwake yeye aliyetupenda" hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kufanikiwa kunyamazisha akili yangu kwa zaidi ya dakika 15 nifundishwe na Roho Mtakatifu maana ya Neno hilo

Baada ya kufundishwa nikuambie kwamba nilikuwa kama mwehu manake sikuomba bali nilitamka na kuanzia wakati ule sikuwahi kamwe kuota tena ndoto ile, huu ni moja ya ufunuo ambao Roho Mtakatifu aliowahi kunifunulia na nikajifunza kwamba ukifunuliwa kitu hata Shetani akisikia unavyoongea anajua na hauna haja ya kuomba unatamka na mambo yanatokea

Hivyo ujinga ndio unakufanya uwe mgonjwa wakati umeokoka omba ufunuo, katika kipindi hiki huna sababu ya kuwekeza kwenye magonjwa bali kwenye miradi mbona kuna biashara nyingi tuu za kuwekeza na faida ikaonekana kuliko kuwekeza kwenye magonjwa?

Inasikitisha sana kukutana na binadamu mwenye fedha halafu anaambiwa usile kitu fulani kisa ugonjwa, yaani fedha umepewa na Mungu, mwili siyo wako ni hekalu la Roho Mtakatifu halafu daktari anakuambia usile chakula fulani mbona mimi naona ni ujinga, hatua ya kwanza ni kukataa unachoambiwa kisha omba Mungu akufunulie siri za afya uone kama utaendelea kupangiwa chakula

Usikubali kabisa kuona wokovu ni suala jepesi hapana ukiokoka uko juu ya kila kitu na hupaswi kusumbuliwa na chochote, wokovu wako wa nini sasa kama unaumwa iko wapi tofauti yako na ambaye hajaokoka? Kama umeokoka na kucha upo hospitali na unakutana huko na ambao hawajaokoka sasa watavutiwaje na wokovu wako?

Wokovu ni kuishi maisha ya Kristo hapa duniani kama Kristo Yesu hakuwahi kuumwa na aliamua kuyachukua magonjwa yako basi hupaswi kuumwa kabisa, jitathimini upya na angalia ni wapi una matatizo kisha rekebisha magonjwa siyo fungu la mtu aliyeokoka hata kidogo, Mimi hata uniamshe usiku wa manane ghafla uniambie mimi ni mgonjwa nitakujibu "I will never be sick" Sintokaa niumwe na ninamaanisha na hili nimeambukiza hata marafiki zangu nao huwa wanakiri vivyo hivyo 

                    YESU NI BWANA!


Tutaendelea tena kesho.......!
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;

SALA YA TOBA

Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa


Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani

Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.


Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu 

Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana

Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa
whatsup nambari 0715113636

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana