Bwana Yesu asifiwe! Ninakusalimu katika Jina lipitalo majina yote, hili ndio Jina lipaswalo kuabudiwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Ninatumaini unaendelea vyema na utumishi wako uliotukuka, leo ni siku njema aliyoifanya Bwana, nitaifurahia na kuishangilia
Kumekuwa na kipindi cha takribani mwezi sasa ambapo tulikuwa hatupati mfululizo wa masomo katika mtandao huu, mtumishi alikwenda shule kusoma na Mungu amemuwezesha kumaliza salama na kwa kishindo kikuu, hivyo tunaendelea na mafunzo yetu kama kawaida na kwa spidi ya ajabu
Tulipoishia..
Fanya utumishi wako kwa Mungu kuwa wa kila iwapo leo na siyo wa msimu hapa ndipo tunapomuona Mungu akijidhihirisha kwetu kwa viwango vingine na vya ajabu kabisa, ndipo mafanikio yetu kiroho na kimwili yanakuwa siyo ajali bali yaliyotoka kwa Mungu peke yake na yaliyobarikiwa yale yanayokwenda mpaka kizazi cha nne kwa ajili ya utukufu wake
Kama hukujifunza nasi somo lililopita lenye kichwa cha habari Mungu ni wa leo ⇒⇒⇒Bofya hapa kujifunza nasi!
Tunaendelea..
Leo tunaanza somo jipya lenye kichwa cha habari mtumwa ni nani? Ni mara nyingi sana umekutana na neno mtumwa kwenye Biblia haswa katika nyaraka za Mtume Paulo, wakati ninafikiri juu ya somo hili nilipata mkanganyiko kwa sababu mtumwa ni mtu asiye na uhuru, ni mtu asiye na haki ni mtu asiyeelewa bwana wake anafanya nini
Nchi za Afrika kipindi cha nyuma zilitawaliwa na mataifa ya ulaya na wazawa wa Afrika walifanywa watumwa ndio maana katika historia tunajifunza juu ya biashara ya utumwa, namna ambavyo mababu zetu walitumikishwa katika mashamba na kufanyishwa kazi ngumu
Hivyo kuona neno Mtumwa linatumika katika Biblia ilinipa ukakasi sana, hivyo imebidi nitafute Biblia ya KJV ambayo ni tafsiri ya kwanza kutokea kwenye Kiebrania na nimegundua kwamba neno lililotumika ni servants (mtumishi) siyo slaves (mtumwa)
Hivyo katika tafsiri ya Kiswahili kulikuwa na tatizo walipaswa kutumia neno mtumishi ambalo ndio kiswahili sanifu cha servants na siyo mtumwa kama ilivyotumika na ninaandika hivi nikiwa na maana na sababu za msingi unapotumia neno ambalo siyo sahihi unapoteza ujumbe uliokusudiwa
Nikushauri na wewe msomaji wakati mwingine unaposoma neno kwenye Biblia na likakutatiza tauta Biblia zingine haswa ya King Jemes Version tizama kule inasemaje na zingine usiridhike kusoma Biblia moja katika kutafsiri kuna maneno ambayo hayakutafsiriwa sawa hivyo ujumbe husika unapotea
Wokovu ni uamuzi siyo lazma ni sawa na kufanikiwa hii ndiyo sababu hujawahi kushikiwa bunduki ukaambiwa haya mkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako! Kitu chochote cha uamuzi binafsi siyo utumwa ni maamuzi ambayo mtu anafanya baada ya kuhubiriwa Injili na kuamua kukata shauri ndiyo maana ukitumia neno mtumishi ni sahihi
Mtumwa ni mtu ambaye anafanya kama anavyoambiwa tena kwa amri wakati mwingi siyo kwa matakwa yake, kile anachoambiwa fanya ni lazma afanye awe anapenda au hapendi, amechoka au hajachoka ni lazima na hakuna muda wa kujadiliana na bosi wako, lakini mtumishi ni tofauti anao muda wa kujadiliana na mwajiri wake, wakashauriana na kufikia maamuzi ambayo hayamuumizi yeyote kati yao
Maana nyingine pana zaidi ni kwamba mtumishi ana haki zake stahiki ambazo mwajiri wake anapaswa kumpatia sawa kabisa na watu waliookoka nao wameajiriwa na Mungu wana haki zao kwa Mungu ndio maana Mungu amejitambulisha kama Mungu wa haki na anamlipa kila mtu sawa na anachostahili Zaburi 31:1 "Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye
Hii ni tofauti na mtumwa kwa sababu hana haki, muda wowote aweza kuuwawa, kuteswa, kufungwa au kuumizwa ndio maana watu wanaomtumikia Shetani hawana haki wakati wowote akijisikia anawateketeza na hawa ndio watumwa wa dhambi, ni chakula cha Shetani na hawawezi kujadiliana naye kumbuka kazi ya Shetani ni hii Yohana 10:10 "Mwizi huja tu kuiba, kuua na kuharibu;
Watumwa wa Shetani huviziwa watende dhambi ili wauwawe, ndio maana ukienda kwa mganga na ukapewa masharti ukakosea hakuna msamaha lazma uwajibishwe na Shetani anafurahia watu wakikosea ili awaangamize, kuwe na sababu ya kufa kwao lakini Mungu ni tofauti kabisa anasamehe na anatoa nafasi ya kuanza upya na hili ndilo linatufanya tumuogope Mungu Zaburi 130:4 "Lakini kwako kuna msamaha, ili wewe uogopwe.
Haijalishi unamtumikia Shetani katika kiwango gani jambo la kukuhakikishia ni kwamba ni lazima ataiba uzima wako, ataiba afya yako ataharibu ndoa au biashara yako na mwishowe atakuuwa kwa sababu ndiyo kazi yake, Shetani hana urafiki wa kudumu wala wa kusaidia mtu akikupatia kitu amelenga katika kukumaliza
Yesu Kristo anataka tuishi maisha ya milele tena yenye utele na furaha Yoh 10:10 "Mimi nalikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele, Yesu Kristo hakutaka tuishie kuwa watumishi wake bali alitupeleka katika hatua nyingine ambayo alituita rafiki zake Yoh 15:15 "Siwaiti tena watumwa (watumishi KJV) kwa maana watumwa hawajui atendalo bwana wake, lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewataarifu
Tutaendelea tena kesho.......!
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
THANK YOU FOR YOUR TEACHING
ReplyDeleteNimebarikiwa na SoMo lako Dada
ReplyDelete