Bwana Yesu asifiwe, Ninatumaini umeamka salama na unaendelea vyema na shughuli zako za kila siku, karibu tena katika mtandao huu kujifunza nasi neno la Mungu, ni ombi langu Roho Mtakatifu akupatie ufunuo wako katika somo hili tunaloendelea kujifunza, Mungu akubariki sana katika Jina la Yesu Kristo, Amen
Tulipoishia...
Yesu Kristo anataka tuishi maisha ya milele tena yenye utele na furaha Yoh 10:10 "Mimi nalikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele, Yesu Kristo hakutaka tuishie kuwa watumishi wake bali alitupeleka katika hatua nyingine ambayo alituita rafiki zake Yoh 15:15 "Siwaiti tena watumwa (watumishi KJV) kwa maana watumwa hawajui atendalo bwana wake, lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewataarifu
Kama hukujifunza nasi somo la jana unaweza ⇒⇒⇒Kubofya hapa kujifunza pamoja nasi
Tunaendelea...
Katika somo la jana tulikuwa tunaweka msingi wa somo hili na tuliweza kuona kwamba neno mtumwa katika Biblia ya kiswahili lilikuwa linanipa ukakasi na nikaamua kusoma Biblia kadhaa ikiwemo KJV ambayo ndiyo tafsiri ya kwanza kutokea kwenye Kiebrania na neno lililotumika ni mtumishi na siyo mtumwa
Leo pia nitaendelea kukazia katika msingi wa mtumwa ni nani ili kukuandaa kwa ajili ya somo hili refu, nisipoweka msingi mwanzoni mwa somo hili huenda mbeleni usielewe kabisa ndio maana jana na leo ninaweka msingi huenda hata kesho nikaendelea pia
Tuliona pia Yesu Kristo alisema sisi siyo watumishi tuu bali alituita rafiki zake, rafiki ni wa karibu kuliko hata ndugu zetu wakati mwingine Mithali 18:24 "Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu" hivyo kimantiki ni kwamba tuna watumishi ambao ni rafiki za Mungu na tuna watumwa ambao wanamtumikia Shetani
Mtumwa kazi yake ni kuadhibiwa na siyo kutunukiwa ndiyo maana neno la Mungu linasema Warumi 6:23 "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" kwa nini kwa sababu mtumwa hastahili mambo mazuri mbele ya bwana wake na hana haki wala urithi na umiliki
Wana wa Hajiri ambaye alikuwa kijakazi (mtumwa wa Sara) hawawezi kurithi pamoja na wana wa Sara kwa kuwa wao ni watumwa Wagalatia 4:25 "Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu kwa sasa; kwa kuwa yuko utumwani pamoja na watoto wake, katika mstari wa 30 inasema vizuri zaidi Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kawa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa muungwana
Sisi siyo watumwa tena kwa sababu hatutumikii dhambi, na pia tunajua ni nini ambacho Bwana wetu anafanya kwa sababu hutufunulia kupitia Roho wake Mtakatifu, kamwe usikubali mtu akuite mtumwa wa Bwana kwa sababu sasa wewe upo huru Wagalatia 5:1" Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa"
Unapompoke Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako haubaki katika ubinadamu wa kawaida bali unahamishwa na unakuwa mtoto wa Mungu kabisa na unapata hati miliki ya Jina la Yesu ndio maana hupaswi kuitwa mtumwa Yoh 1:12 "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake"
Lakini nisisitize kitu kimoja hapa mtoto ambaye hakui anaweza kuwa hana tofauti na mtumwa, ukimpokea Yesu Kristo unakuwa mtoto wa Mungu lakini unapaswa kukua kutoka kwenye utoto na kuwa mwana hili ni jukumu lako, siku hizi tuna watoto wengi kanisani wana miaka 40, 50, 60 ila ni watoto ndio maana wanasumbuliwa na wachawi, magonjwa na laana
ukiwa mwana huwezi kusumbuliwa kamwe
Kumbuka Yesu Kristo hakuwahi kujiita mtoto wa Mungu bali mwana wa Mungu jua kuna tofauti ndio maana Mtume Paulo naye alisema maneno mazito Wagalatia 4:1 "Lakini nasema kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ni bwana wa yote" hivyo hupaswi kuwa mtoto wakati wote la sivyo utakosa urithi wako unapaswa kukua kiroho ili kumiliki milki zako
Ukiwa mtoto unafikiri kama mtoto, unakunywa maziwa na siyo kula chakula na unatumikishwa na kawaida za dunia, mwana anakula chakula kigumu, hatumikishwi na dunia bali dunia inamtii kile anachokisema, ninaposema dunia ninamaanisha anasa, nguvu za giza na mambo yanayofanana na haya Wagalatia 4:3 "Kadhalika na sisi tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia"
Zaidi ya yote tambua kama ungekuwa mtumwa Mungu asingeimimina Roho yake ndani yako, unaanza kukua na kuwa mwana baada ya kubatizwa kwa moto yaani Roho Mtakatifu Wagalatia 4:6-7 "Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa mwanawe mioyoni mwetu, aliye, Aba, yaani, Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu
Tutaendelea tena kesho.......!
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana