WANAWAKE WALIOCHUKUA HATUA ZA HATARI KWENYE BIBLIA- SEHEMU YA NNE - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Tuesday, November 27, 2018

WANAWAKE WALIOCHUKUA HATUA ZA HATARI KWENYE BIBLIA- SEHEMU YA NNE

Ninakusalimu sana katika Jina la Bwana Yesu Kristo, ni asubuhi njema na tulivu sana aliyoifanya Bwana kwa ajili yetu ili tuweze tena kuzitangaza sifa zake na uaminifu wake katika maisha yetu, nina furaha na amani tele ninakukaribisha katika mtandao huu tuendelee kujifunza pamoja Neno la Mungu kwa pamoja, ninamuomba Roho Mtakatifu akupatie roho ya ujasiri kama mwanamke ambaye tutajifunza hivi leo
Tulipoishia
Abigaeli alijiweka katika hatari yeye pamoja na ndoa yake kwa kufanya maamuzi kinyume kabisa na mumewe lakini maamuzi haya yalimfanya mumewe aishi siku kumi zaidi kwa sababu baada ya hapo Bwana alimpiga Nabali naye alikufa, mbeleni kabisa tunaona alikuja kuposwa na Mfalme Daudi naye akawa mke wa Mfalme
Kama hukuweza kuungana nasi katika kipindi kilichopita cha mfululizo wa somo hili la wanawake waliochukua hatua za hatari kwenye Biblia sehemu ya tatu ⇒⇒⇒Unaweza kubofya hapa kujifunza nasi!

Tunaendelea
Wanawake kwenye Biblia tumefanya mambo makubwa na tuliweza kuwauwa mpaka makamanda wa majeshi, waliokuwa na heshima zao na vyeo vyao, kama vile Biblia inavyosema wanawake ni jeshi kubwa kweli sisi ni jeshi kubwa na tumelidhihirisha hilo mara nyingi katika maombi, katika huduma na katika kazi  Zaburi 68:11 "Bwana analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa
Leo tunamwangalia mwanamke mwingine shupavu na hodari aitwaye Yaeli aliyeikana amani kati ya nyumba yake na ya mfalme Yabini kwa kumuuwa kamanda wa jeshi aliyeitwa Sisera, kama unasoma vizuri Neno la Mungu utakuwa unakumbuka utawala wa Waamuzi wa Israel kabla ya utawala wa kifalme kuja, Israel ilikuwa ikitawaliwa na waamuzi (judgers) 

Utawala wa Waamuzi ulikuwa mpango wa Mungu kwa Israeli kwa wakati ule, lakini mataifa ya jirani na Israeli yalikuwa na namna nyingine ya utawala ambayo ilikuwa ni ya ufalme, wakati ulifika Israeli ikataka utawala wa kifalme na ndipo mfalme wa kwanza wa Israeli akawa Sauli
Moja ya mtawala mwamuzi aliyekuwa mwanamke ni Debora, na wakati wa utawala wake taifa la Mungu teule la Israeli lilikuwa chini ya mateso ya mfalme Yabini wa Kaanani, huyu aliwatesa sana wana wa Israeli 

Wana wa Israeli walimlilia Mungu awakomboe na mateso ya Sisera ambaye likuwa na magari ya chuma mia moja ambayo aliyatumia kuwatesa sana Waamuzi 4:3 "Wana wa Israeli wakamlilia BWANA; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia kenda; naye akawaonea wana wa Israeli kwa nguvu muda wa miaka ishirini
Roho wa Bwana akawa juu ya Debora naye akamwambia kamanda wake aitwaye Baraka wakwee na kwenda kupambana na Sisera pamoja na jeshi lake, maana Bwana angemtia Sisera mikononi pake, Baraka akamwambia, Wafalme 4:8 "Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi.

Huyo ni mwanaume anaogopa kwenda peke yake mpaka asindikizwe na mwanamke, ingekuwa ni kipindi kama hiki chenye msemo wa wanaume wa Dar basi huyu wangesema anatokea Dar-es-salaam, ila mwanamke tulionyesha ujasiri akaenda nae
Debora akamwambia ataenda naye lakini Bwana atamtia Sisera mikononi mwa mwanamke na siyo mikononi mwa Baraka, hii ni baada ya kuruhusu woga kumuingia, Mungu ametuasa sana juu ya woga kwa sababu woga unapotezea watu wengi mambo mengi

Ndivyo ilivyotokea Yaeli mke wa Heberi aliweza kumuuwa Sisera baada ya vita kumuelemea na kukimbilia katika hema la Yaeli, Waamuzi 4:21 "Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa.

Kumbuka kilichomfanya Sisera kukimbilia katika hema la Yaeli ni amani ambayo ilikuwapo baina ya nyumba ya mumewe na mfalme hili tunaliona Wafalme 4:17 "Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikilia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni.

Hivyo ni dhahiri kabisa kwamba Yaeli alichukua hatua ya hatari ya kuhatarisha ndoa yake, amani iliyokuwepo baina yao, mahusiano baina ya mfalme wa Hazori na nyumba ya mmewe kwa sababu tuu alimuuwa Sisera, hiyo nayo imetufanya tumuweke Yaeli katika kundi la wanawake waliochukua hatua za hatari katika Biblia

              YESU NI BWANA!
Tutaendelea tena kesho.......!
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;

SALA YA TOBA 

Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa


Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani

Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.

Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu 
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 071511363

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana