Ninakusalimu katika Jina lipitalo majina yote, hili siyo Jina lingine bali Jina la Yesu Kristo, jina lipaswalo kuabudiwa na kusifiwa, lenye nguvu na mamlaka, jina tulilopewa kwa ajili ya kumshinda mwovu na jina lenyo wokovu wetu, ninatumaini wewe ni mzima wa afya na unaendelea vizuri kabisa
Tulipoishia
Jana pia tuliendelea na somo letu la wanawake waliochukua hatua za hatari kwenye Biblia na jana tuliona sehemu ya pili ambapo tulimwangalia mwanamke aliyeitwa kahaba kwenye Biblia yaani RAHABU tuliweza kuona ni namna gani aliweza kuikomboa familia yake kwa kuchukua hatua za hatari za kuwaficha wapelelezi kama hukubahatika kujifunza nasi unaweza ⇒⇒⇒⇒Kubofya hapa tujifunze wote !
Leo kipekee kabisa tunaangalia namna ambavyo mwanamke mwenye Jina sahihi alivyookoa uhai wa mmewe na watumwa wake kwa kuchukua hatua za hatari, jee unamfahamu mwanamke huyo? kama hapana basi endelea kujifunza nasi
Tuendelee
Katika maisha yetu huwa tunachukulia kiholela lakini majina ambayo tunawaita watoto wetu, hubeba hatma zao kwenye ulimwengu wa kiroho, kila mtu aliyekutana na mguso wa Mungu kama Jina lake halikuwa jema alibadilishwa Jina na kupatiwa Jina jipya
Katika Neno la Mungu kuna watu wengi ambao tunaweza kuwatumia kama mfano kudhihirisha hili wa kwanza kabisa ni Baba yetu Abramu alibadilishwa kuwa Abrahamu yaani baba wa mataifa mengi Mwanzo 17:5 "Wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Abrahamu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi" mstari wa 15 "Sirai mkeo hutamwita jina lake Sirai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara (mama wa mataifa mengi)
Petro maana yake ni kigeugeu, mtu asiyeaminika muda wowote anakukana ndiyo maana Yesu akambadili Jina na kumwita Simoni/ Kefa yaani mwamba jina la Petro lilimuandama hata baada ya Yesu kuondoka bado alikuwa anabadilika ndio maana kuna wakati Mtume Paulo alimkemea sana juu ya tabia yake Wagalatia 2:11" Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nilishindana nae uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu"
Kwa nini alishindana nae?
Mstari wa 12 "Kwa maana kabla hawajaja watu kadhaa waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa, lakini hao walipokuja, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa"
Yakobo maana yake ni muibaji wa hatma na baraka za wengine, ndiyo maana alimuibia nduguye Esau japokuwa Mungu alimpenda Yakobo na kumchukia Esau, Makaki 1:3 "Bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani" lakini swali la kujiuliza ni kwa nini Mungu alimbadili jina Yakobo na kumuita Israeli? Ina maana jina lake lilikuwa na tatizo
Sauli maana yake mtesaji, muonevu na asiejali wengine Mtume Paulo alikuwa ndiye anayeongoza kwa kupanga njia za kuwauwa mitume, na hata kifo cha Stefano alikuwepo na alikuwa anashangilia ndiyo maana baada tuu ya kukutana na mguso wa Mungu alibadilishwa jina kutoka Sauli kuwa Paulo, wapo wengi lakini hawa ni baadhi tu kipindi kingine tutawaangalia kwa undani
Ukimuita mtoto wako tabu au shida nakuhaikishia maisha yake yatasawiri jina hilo na hii tunaiona hata katika Biblia, kitabu cha 1Sam 25 1-44 kuna habari ya tajiri mpumbavu aliyesawiri jina lake Nabali, (tafsiri yake tunaipata mstari wa 25 ) "Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma"
Kwa nini majina yetu ni ya muhimu
Majina yetu ni kitambulisho chetu katika ulimwengu wa roho, kila jina lako linapotajwa wewe ndiye unaetambulika na siyo mwingine, ndio maana kitambulisho hiki hata leo ukilitaja jina la Yesu Kristo mapepo yanatoka na kukimbia kwa sababu maana ya Jina Yesu ni mkombozi wa ulimwengu, pepo likisikia lazma likimbie
Pia kumbuka mambo hayaanzi katika ulimwengu wa mwili bali wa roho, ndiyo maana ni lazima kuhakikisha unaweka mambo yote sawa katika ulimwengu wa roho ikiwemo jina lako ili kusiwe na kitu chochote cha kuzuia baraka au neema ambayo Mungu amekuandalia tuendelee na habari ya Nabali
Kwa nini majina yetu ni ya muhimu
Majina yetu ni kitambulisho chetu katika ulimwengu wa roho, kila jina lako linapotajwa wewe ndiye unaetambulika na siyo mwingine, ndio maana kitambulisho hiki hata leo ukilitaja jina la Yesu Kristo mapepo yanatoka na kukimbia kwa sababu maana ya Jina Yesu ni mkombozi wa ulimwengu, pepo likisikia lazma likimbie
Pia kumbuka mambo hayaanzi katika ulimwengu wa mwili bali wa roho, ndiyo maana ni lazima kuhakikisha unaweka mambo yote sawa katika ulimwengu wa roho ikiwemo jina lako ili kusiwe na kitu chochote cha kuzuia baraka au neema ambayo Mungu amekuandalia tuendelee na habari ya Nabali
Sasa usiniulize alifanikiwaje na kuwa tajiri wakati alikuwa ni mpumbavu, kumbuka ndoa ni baraka Nabali alikuwa amemuoa Abigaeli ambaye Biblia imemuelezea kama mwanamke mwenye akili njema na mzuri wa uso, Daudi alituma watu wake kwa Nabali kwa ajili ya kuwapatia chakula baada ya Mfalme kukaa kwa muda pamoja na watu wake na mifugo yake na kumtunzia pasipo hata mmoja kupotea
Matokeo yake Nabali alimdharau mfalme kwa kusema maneno haya kwa Watumishi wa Daudi mstari wa 10 "Naye Nabali akawajibu wale watumishi wa Daudi, akasema, Huyu Daudi ni nani? Na mwana wa Yese ni nani? Siku hizi kuna watumwa wengi wanaomtoroka kila mtu bwana wake!
Majibu haya yalimchukiza sana Mfalme kiasi ambacho aliandaa jeshi lake tayari kwenda kumuuwa Nabali na watumishi wake wote, lakini Abigaeli alijuzwa na mtumishi wake juu ya maneno mabaya aliyotamka mumewe (Nabali) kwa mfalme Daudi
Mstari wa 18 Ndipo Abigaili akafanya haraka, akatwaa mikate mia mbili, na viriba viwili vya divai, na kondoo watano waliofanyizwa tayari, na vipimo vitano vya bisi, na vishada mia vya zabibu, na mikate ya tini mia mbili; akavipakia vitu hivi juu ya punda
Baada ya hapa alimuomba Mfalme msamaha sana naye mfalme aliridhia na kumshukuru kwa kumfanya asimwage damu sababu ndio walikuwa wanakuja kumuangamiza Nabali na watumishi wake
Abigaeli ameingia katika wanawake waliochukua hatua za hatari kwa sababu cha kwanza alifanya hivi kinyume na mume wake, ukumbuke mumewe alishawanyima chakula na akawa anajiandaa kwa karamu nyumbani mwake
Abigaeli alijiweka katika hatari yeye pamoja na ndoa yake kwa kufanya maamuzi kinyume kabisa na mumewe lakini maamuzi haya yalimfanya mumewe aishi siku kumi zaidi kwa sababu baada ya hapo Bwana alimpiga Nabali naye alikufa, mbeleni kabisa tunaona alikuja kuposwa na Mfalme Daudi naye akawa mke wa Mfalme
YESU NI BWANA!
Tutaendelea tena kesho.......!
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana