Mungu hajawahi kuwahi wala kuchelea huja kwa wakati sahihi, ukitumia akili yako na kuamini amechelewa jua tatizo ni lako siyo la Mungu, haijalishi itakuchukua muda gani kukamilisha kile ambacho Mungu amekuambia jua wakati utapita na utafika
Unaporukia kufanya kitu ambacho Mungu hajakuita kufanya unakosa amani, Wafilipi 4:7 "Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo. Tunapokuwa ndani ya Kristo tuna uhakika wa kukamilisha kusudi letu
Mungu anatupatia kila ambacho tunakihitaji kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu Wafilipi 4:19, ndiyo maana ni muhimu kahakikisha ya kwamba tupo ndani ya Kristo na Kristo yupo ndani yetu, baada ya kifo cha Yesu Kristo Mungu hatuoni sisi tena bali anamuona Kristo ndipo anapotujibu maombi yetu
Kama hukusoma sehemu ya tatu ya makala ya wakati inayoitwa GUSA HAPA ⇉⇉⇉⇉ JILA JAMBO NA WAKATI WAKE
Yule ambaye amejishika sana na Kristo ndio anauhakika wa kukamilisha mambo yake kwa wakati sahihi, ni muhimu tufahamu kwamba mafanikio yetu ni utukufu kwa Mungu, umasikini na vifungo siyo sifa nzuri kwa Mungu
Ndiyo maana Mungu anakuita kwake kila wakati kupitia Yesu Kristo ili aweze kukutatulia umasikini wako, changamoto zako, afungue vifungo vyako na atengeneze njia ambayo ni njema kwa ajili yako
Kizazi chetu kimebahatika sana tofauti na vizazi vingine kwa sababu hatumtafuti tena Mungu nje bali ndani yetu, wewe ni mkubwa sana kimaandiko kuliko Musa, Elia, Elisha, Yohana Mbatizaji tatizo ni kwamba hujafahamu tuu ukuu wako
Mathayo 11:11 "Lakini nawaambieni Hajatokea mtu katika uzao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkubwa kuliko yeye. Yohana alikuwa mkuu kuliko wote waliomtangulia sababu alikaa na Yesu Kristo isitoshe alimbatiza
Lakini Yesu Kristo hakukaa ndani ya Yohana Mbatizaji ndio maana kwenye ufalme wa mbinguni sisi ni wakubwa na tupo karibu zaidi na Mungu kuliko yeye, tatizo ni moja watu wengi hawajaujua ukuu na nguvu ambayo Mungu amewapatia kwa neema
Mungu ni Roho na tupo naye wakati wote, anasema katika Yohana 4:24 "Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika katika roho na kweli, hatumwabudu Mungu katika mwili kwa sababu miili yetu inapingana na Roho Wagalatia 5:17 "Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho ikishindana na mwili; kwa maana hizi zinapingana, hata hamwezi kufanya mnayoyataka
Kutumainia mwili ni pamoja na kuziamini akili zetu ndiyo maana huwa mara nyingi tunawaambia watu usiwe kama Yesu alisema anarudi mpaka leo hajarudi, kama umewahi kusema hivi Mungu akurehemu, na tambua kwamba wewe ndio umesababisha hajarudi mpaka leo kwa sababu ni mpaka Injili ihubiriwe kote na watu wamfahamu ndiyo atakapokuja sasa swali kwako ni jee hata akija sasa utakwenda mbinguni?
Umemuweka Yesu moyoni na kushika mafundisho yake? Je unazifuata taratibu na kusimamia kile ambacho alifundisha hatuwezi kupata haki zetu kwa Mungu kama sisi hatujajiweka safi mbele ya uso wake
Kunena kwa lugha siyo sababu ya kusamehewa, yule ni Roho anazungumza ndani yako ni karama ambayo Mungu anampatia kila mtu kwa neema ambaye ana kiu na shauku ya kunena na huu ndio ubatizo wa moto lakini ni mpaka utakapotubu dhambi ndipo utakaposamehewa
Hata mfungwa wa gerezani huwa anahitaji chakula tena kwa wakati sahihi na uliokusudiwa, chakula chetu ni neno la Mungu na tambua ni pale mtu anapotubu ndipo anapojiweka safi mbele ya Mungu
Kizuizi cha majibu ya maombi yetu kwa wakati ni dhambi kwa sababu asili ya dhambi ni Shetani, kitu kitakachokuletea ushindi hadi kwenye vizazi vyako hutegemea zaidi namna ulivyosimama na Mungu katika maisha yako ya sasa
Wapo watoto wanaorithi laana badala ya baraka kwa sababu ya maovu yaliyofanywa na babu na bibi zao, hivyo hata wakati wanamuomba Mungu hawajibiwi kwa wakati, Mungu hupatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne
Urithi mwema na wa baraka ni wa kumcha Mungu, hakuna kinachokwenda kwa Mungu kikarudi kwa hasara na huu ndio wakati mzuri wa kumtumikia Mungu tungali vijana,
Nayo dhambi hutakaswa kwa Neno, siyo nao wanitafutao wataniona bali Nao wanitafutao kwa bidii wataniona, ukiacha dhambi hutapungukiwa kitu, na isitoshe ni kwa manufaa yako mwenyewe, Mungu hakuiti ili umsaidie bali akusaidie
Kaa ukijua hakuna ibada ya Mungu ambayo Malaika hukosekana huwepo eneo la tukio wakizunguka hata kabla haijaanza, kabla hujaanza kusoma makala hii ulishaandaliwa kifikra na neno hili ulikusudiwa, malaika wako wakutunze siku hii ya leo katika kila unachofanya
Kumbuka harufu za binadamu hutofautiana kila mtu na harufu yake, ni kama vidole vyetu huu mwili ni kama wa Esau lakini sauti ni kama ya Yakobo.
Kumbuka yote haya hayawezi kufanya kazi kwako kama hujampokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, Mungu anakupenda sana na hata sasa anakuita tena katika utukufu wake, kama Yeye hashindwi huwezi kuwa ndani yake ukashindwa, tafadhali sali sala hii kwa imani kama hujampokea Yesu
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"
TV Online Channel
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Bafikiwa
ReplyDeleteAmeni, umebarikiwa sana na wewe mtumishi wa
Delete