Ninakusalimu katika Jina la Yesu Kristo, Jina lipitalo majina yote ulimwengu huu hata ule ujao, leo ni siku njema sana inayopendeza na Mungu amifanya kwa utukufu wake ili tumsifu na tumtukuze yeye pekee, ni matumaini yangu kwamba wewe ni mzima wa afya na unaendelea vyema na kazi zako za kila siku
Leo tunaendelea na kichwa cha somo cha Mungu ni wa leo sehemu ya pili, kama hukupata nafasi ya kujifunza nasi sehemu ya kwanza ya somo hili ni vyema ukaanza nayo kisha ukaendelea sehemu ya pili ili kujiwekea msingi mzuri unaweza ⇒⇒⇒Kubofya hapa kujifunza sehemu ya kwanza
Tulipoishia somo lililopita.....
Hivyo njia nzuri ya kuwashinda wanaotaka kuleta majibizano ya ndimi ni kunyamaza, ni mara nyingi watu humsema mtumishi fulani vibaya ili tuu aongee ila unapokuwa kwenye maficho ya Mungu anakuepusha na kujibizana nao unakaa kimya na huduma inasonga mbele zaidi kwa utukufu wa Mungu Baba Mwenyezi
Kama hukupata wasaa wa kujifunza neno hili la "Mungu anayejificha sehemu ya tano" unaweza pia kujifunza kwa ⇛⇛⇛Kubofya hapa kujifunza mwanzo hata mwisho
Tunaendelea....
Mungu hataki kuwa wa kesho sababu anataka tumtumikie kila siku, hatupaswi kutafuta uso wa Mungu tunapokuwa na shida pekee La Hasha! Tunautafuta uso wa Mungu kila iwapo leo sababu pasipo Mungu hatuwezi kufanikisha mambo yetu wenyewe katika maisha
Tukitaka kufika mbali zaidi katika kazi, biashara, mahusiano huna budi kutengeneza muda wa kufanyia kazi kila siku katika kitu unachotaka kifanikiwe, hata kumtumikia Mungu huna budi kufanya kila siku, Mungu anasema katika Isaya 48:17 "BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata
Yule ambaye anatengeneza mahusiano yake na Mungu kila iwapo leo ndiyo anamuona kwa viwango vingine, Mungu hana upendeleo na huangalia moyo kama unampenda anakujua, Mdo 10:34-35 "Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo, bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa naye
Hivyo kwenye maisha yako usikae ujione kwamba huwezi kufika sehemu fulani au mtu fulani ana neema kuliko wewe, wote tuko sawa utofauti ni kwamba yeye anamcha Mungu kuliko wewe ukijitoa kama anavyojitoa unakuwa kama yeye hata na zaidi, ndiyo maana nasema kwamba "I am not local preacher, I am international preacher" Yohana 10:14 "Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; je hautaki kujulikana na Mungu? Unapomtumikia Mungu kwa moyo wako wote unajulikana kwake
Hapa ni pale unapomfanya kuwa maisha yako ndipo Mungu anapofikia hatua ya kusema huyu ni Mtumishi wangu, mtu anapokugusa anakuwa kagusa mboni ya jicho lake, mtu anapokukosea anakuwa kamkosea Mungu mwenyewe Zakaria 1:8 "Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake
Unapomfanya Mungu kuwa wa leo na siyo wa kesho naye anajidhihirisha kwako kila leo, Wakristo wengi wamemfanya Mungu kuwa wa jumapili tu hivyo siku sita anajitumikia yeye na ya saba tu kwa Mungu ndio maana hawaishiwi na matatizo
Kama unataka kuyatengeneza maisha yako zaidi hauna budi kuhakikisha kwamba unamtumikia Mungu katika viwango vingine, hauna budi kuyaangalia mahusiano yako na Mungu, hauna budi kulisoma neno lake na kuomba kila wakati, tunaweza kufikia viwango vya kina Ayubu vya Mungu kujivunia kuhusu sisi pale tunapogeuza utumishi kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku na siyo suala la jumapili tu
Kila kitu chema kina gharama za kulipia utahangaika sana kuzunguka huku na kule kutafuta mafanikio, miujiza na kwingine watakupatia mapepo kabisa siri ni hii tengeneza mahusiano yako na Mungu, nuru haichangamani na giza unapozama ndani kabisa kwenye damu ya Yesu, unapomfanya Yesu kuwa maisha yako hilo pepo au huo ugonjwa ni lazima utayeyuka, huo mpenyo unaoutafuta ni lazima utatokea hata unapotaka kwenda ni lazima utafika
Hakuna siku nzuri ya kumtumikia Mungu kama leo, leo ndio leo ni lazima tumtumikie Mungu kuanzia leo na kuendelea kwa sababu Mungu ni wa leo na siyo kesho, kama umekuwa unatumia nguvu zako kutafuta vitu vyako na bado haujafanikiwa ni kiasi cha kubadilisha gia na kuanza kumtegemea Mungu pekee na kumfanya Yeye kuwa kila kitu kwenye maisha yako
Neno linasema hivi kwenye Mathayo 6:33 "Tafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na haki yake na hayo mengine yote mtazidishiwa, tatizo la watu wengi wamebadili neno la Mungu na wanataka kwenda wanavyofikiri wao, wanataka mengine yote kwanza kisha ndio wautafute ufalme wa Mungu, kama Mungu ndiye aliyeweka utaratibu huu alikuwa na maana yake kinachotokea ni kwamba wengi hawapati wanachotaka na inapelekea watu kichanganyikiwa
Hata wale ambao wamepata kwa neema ya Mungu wanafikiri vile walivyokuwa navyo ni nguvu zao maana hawakuvipata katika utumishi hivyo baada ya muda wanajiinua wao na ghadhabu ya Mungu inawaka juu yao kisha wanarudi walipokuwa kwenye umasikini
Tunamtumikia Mungu kila siku kwa sababu Mungu anataka tumtumikie, ndiye anayetulinda na kutubariki, ndiye anayetupatia nguvu, hekima na maarifa ya kupata utajiri, ndio maana suala la kumtaka Mungu ni la kila siku na kila saa sio kwa msimu fulani
Fanya utumishi wako kwa Mungu kuwa wa kila iwapo leo na siyo wa msimu hapa ndipo tunapomuona Mungu akijidhihirisha kwetu kwa viwango vingine na vya ajabu kabisa, ndipo mafanikio yetu kiroho na kimwili yanakuwa siyo ajali bali yaliyotoka kwa Mungu peke yake na yaliyobarikiwa yale yanayokwenda mpaka kizazi cha nne kwa ajili ya utukufu wake
Tutaendelea tena kesho.......!
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana