Ninakusalimu katika Jina la Bwana Yesu Kristo, ninatumaini unaendelea vizuri kabisa, hii ni siku nyingine njema sana aliyoifanya Mungu kwa ajili ya utukufu wake, kuna baraka mpya kwa waaminio kila siku na ninatamka katika Jina la Yesu Kristo hutopishana na baraka zako siku hii ya leo
Kuingia katika mtandao huu na kujifunza Neno la Mungu ni sababu tosha ya kuwa una kiu ya kujifunza neno la Mungu na kwa sababu hujafuata udaku wala habari zisizo na maana Mungu ninaemtumikia akubariki katika Jina kuu la Yesu Kristo, Amen!
Tulipoishia...
Wokovu ni kuishi maisha ya Kristo hapa duniani kama Kristo Yesu hakuwahi kuumwa na aliamua kuyachukua magonjwa yako basi hupaswi kuumwa kabisa, jitathimini upya na angalia ni wapi una matatizo kisha rekebisha magonjwa siyo fungu la mtu aliyeokoka hata kidogo, Mimi hata uniamshe usiku wa manane ghafla uniambie mimi ni mgonjwa nitakujibu "I will never be sick" yaani "Sintokaa niumwe" na ninamaanisha na hili nimeambukiza hata marafiki zangu nao huwa wanakiri vivyo hivyo
Tambua kwamba masomo haya yako katika mtiririko unaofuatana, uanapokosa kujifunza somo moja huenda usielewe vizuri somo jingine ndiyo maana nakushauri kama hukutengeneza muda wa kujifunza nasi somo la jana la mtumwa ni nani- sehemu ya tano unaweza kuungana nasi kwa kujifunza lote kwa ⇉⇉⇉Kubofya hapa na utajifunza lote
Tunaendelea.....
Jana tuliangalia sifa ya pili ya mtumwa ambayo ilikuwa inasema kama umeokoka na unasumbuliwa na magonjwa wewe ni mtumwa, na tuliweza kuweka msingi na kufahamu maana ya kuokoka ni kufanana na Yesu Kristo kile ambacho alicho nacho ndicho unapaswa kuwa nacho, kama hakuwahi kusumbuliwa na magonjwa nawe pia haupaswi kusumbuliwa
Leo tunaendelea na pointi ya jana ya utumwa katika magonjwa sehemu ya pili ambapo tunaangalia nguvu iliyopo katika meza ya Bwana, kumbuka jana tuliangalia wokovu leo tunaangalia kuhusisha nguvu ya meza ya Bwana katika kupata afya ya kiungu, na msemo wa leo ni kama unakula meza ya Bwana na unasumbuliwa na magonjwa wewe ni mtumwa
Yesu Kristo aliamua kutuosha kwa damu yake ili tupate ondoleo la dhambi na tuweze kuwa wafalme na makuhani mbele za Mungu Uf 3:6, 5:10 "Ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi" hivyo sisi sio binadamu wa kawaida bali ni wana wa ufalme na makuhani ni lazima ujione namna hii kwa sababu ndivyo neno linavyosema juu yako
Yohana 6:48 "Mimi ndimi chakula cha uzima" Yesu ndiye chakula cha uzima maana yake kila ambaye anakula chakula hiki hawezi kufa kamwe bali anakuwa na uzima wa milele, chakula ninachoongelea hapa ni mwili na damu ya Bwana Yesu Kristo, neno uzima ni kuwa na uhai, ni kutokufa ni kutokuwa na shida yeyote ile
Kama unaenda Kanisani au unamfuata Yesu ili akupatie chakula cha kawaida kama wali, au makande na maharagwe umeshapotea na ndiyo maana unasumbuliwa na magonjwa, hatuendi kwa Yesu ili tupate chakula cha kibinadamu bali cha kiungu, ukila chakula cha kiungu una uhakika wa kuwa na afya tele na magonjwa kukukimbia kwa sababu Yesu ni chakula cha uzima
Yohana 5:26-27 "Yesu akajibu, akasema, Amin, amin, Nawaambieni, Ninyi mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba, Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa.." tunapokula mwili na damu ya Yesu Kristo tunamkaribisha kuingia ndani ya miili yetu nasi tunakuwa kitu kimoja naye, tunafanyika kuwa yeye
Ni ajabu sana kama unakula chakula hiki na unasumbuliwa na magonjwa, yawezekanaje ule na unywe uzima alafu uwe na magonjwa? hakika ni jambo la kushangaza sana, huwezi kuwasha taa yenye mwanga mkali kwenye giza na giza lisiondoke, Yohana 1:5 "Nayo nuru yang'aa gizani nalo giza halikuiweza" tambua kuna sehemu hujaweka vyema imani yako ndiyo maana haupokei
Kuweza kuondoka kwenye utumwa wa magonjwa kupitia meza ya Bwana ni lazima ujione mtu wa tofauti kwa sababu Yesu Kristo hayupo nje yako bali ndani yako nawe ndani yake kwa namna nyingine mnabadilishana nafasi, jambo hili unalolifanya hata malaika wa mbinguni hawajawahi kulifanya, hata baba yako Ibrahimu hakuwahi, Musa hakuwahi, Daudi rafiki wa Mungu hakuwahi, sisi ni wa pekee kuliko manabii na watumishi wote wa agano la kale
Kama unataka kuamini wewe ni mtu wa pekee tizama fikiri juu ya hili, malaika walifanya dhambi moja tuu wakaja duniani wakajichukulia wana wa binadamu wakazaa nao na kuwafundisha mambo yasiyowahusu, baada ya uasi wao huu walimuomba Henoko awaombee msamaha kwa Mungu tena kwa maandishi ili Mungu awasamehe dhambi walioifanya lakini kamwe Mungu hakuwasamehe na hukumu inawahusu
Yuda 1:6 "Kwa malaika wasiolinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu" leo hii binadamu ukifanya dhambi hata iwe ya namna gani isipokuwa kumkufuru Roho Mtakatifu unasamehewa sasa hujioni wewe ni wa pekee sana?
Huku kutokujua upekee wetu ndiko kunakofanya Shetani anawatesa watu na magonjwa, vifungo, mateso ndiyo maana muimba Zaburi Asafu akasema Zaburi 82:5 "Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; misingi yote ya nchi imetikisika" Ni lazima uitambue nafasi yako ili kuishi maisha ya kiungu hapa duniani, usipoijua hata kama umeokoka utateseka sana na utakufa kama wanadamu wa kawaida
Baba zetu walifia jangwani kwa sababu hawakula chakula cha uzima Yohana 6:49 "Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa" kwa sababu huwezi kamwe kufananisha chakula cha malaika na chakula cha uzima, mana ni chakula cha malaika Zaburi 78:25 "Mwanadamu akala chakula walacho malaika; Akawapelekea chakula cha kuwashibisha"
Hivyo kuanzia leo tambua kwamba haupaswi kuumwa wala kuteseka kwa namna yoyote kama unashiriki meza ya Bwana kwa imani, jichunguze tena ni wapi unakosea hakikisha unajiandaa kiroho kabla ya kushiriki na utaona mambo yakibadilika na magonjwa yakikukimbia katika Jina la Yesu Kristo aliye hai
Nihitimishe siku hii ya leo kwa kusema kwamba kuna mambo makuu matatu yanayomfanya Yesu Kristo aishi ndani yetu na sisi ndani yake na siku ya jana tuliangalia jambo la kwanza ambalo ni wokovu na leo tumeangalia meza ya Bwana na kesho tutaangalia neno la Mungu, afya ya kiungu ni haki yako kama umeokoka na ninakuona ukiwa na uzima katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Amen!
YESU NI BWANA!
Tutaendelea tena kesho.......!
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana