Ninakusalimu katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti nina amini kwamba wewe ni mzima wa afya na unaendelea vyema na kazi uliyopewa na Mungu, ninazidi kumshukuru Mungu kwa ajili yako na kwa kila hatua ambayo unapiga kwenye maisha, kwa sababu hatua zinadhihirisha uwepo wa Mungu katika maisha yetu
Ninakukaribisha tena kipekee katika mtandao huu kujifunza Neno la Mungu pamoja nasi, nikuhakikishie upo sehemu sahihi na haujapotea, na kwa sababu una kiu ya Neno la Mungu basi Yesu Kristo mwenyewe aliye maji ya uzima na akuhudumie katika Jina la Yesu Kristo kupitia Roho wake wa mafunuo
Tulipoishia....
Sasa wewe umeokoka halafu bado unasumbuliwa na mambo ya kichawi?
jua bado hujaamua kusimama kwenye Neno la Mungu, ninamaanisha hili nimeshachoma
moto nyumba ya mchawi ninaposhi na jioni baada ya siku moja akanitumia majeshi
ya paka akidhani ataniweza nikayafurumsha na damu ya Yesu usiku wa manane,
ukweli ukijua nafasi yako hakuna kitu kitakutishia katika hii dunia
kinachohusiana na uchawi, ushirikina, magonjwa, kulogwa n.k omba tuu ufunuo
usiende kichwa kichwa maana utapigwa vizuri tuu na utaomba poo!
Tambua
kwamba masomo haya yako katika mtiririko unaofuatana, uanapokosa kujifunza somo
moja huenda usielewe vizuri somo jingine ndiyo maana nakushauri kama
hukutengeneza muda wa kujifunza nasi somo la jana la Mtumwa ni nani- sehemu ya saba unaweza
kuungana nasi kwa kujifunza kwa ⇒⇒⇒Kubofya hapa kujifunza nasi, tambua ya kuwa linki hii itakuwezesha kusoma mfululizo wote huu wa somo hili kuanzia sehemu ya saba mapaka ya kwanza
Tunaendelea....
Jana
tuikuwa na somo zuri sana la Neno ni nini? na tuliweza kuona katika sehemu ya
kwanza kwamba Neno ni Yesu Kristo mwenyewe, tafadhali hakikisha unabofya linki
hapo juu kama hukujifunza somo la jana kwa sababu ndio lililotengeneza msingi
wa neno la leo
Kumbuka
mada yetu ni mtumwa ni nani, na bado tupo kwenye sifa ya pili ya mtumwa
inayosema "Kama wewe umeokoka na
unasumbuliwa na magonjwa wewe ni mtumwa" tambua ya kwamba
wokovu umekutenga na magonjwa, katika baraka za Mungu kwetu hakuna baraka ya
magonjwa bali ya afya ya kiungu Kutoka 23:25 "Ninyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye
atabarikia chakula chenu, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati
yako"
Wokovu kama unavyoelezewa katika Neno la Mungu "siyo hali ya utoto" ni hali ya "uwana yaani majukumu" ni sawa nikisema wanaoumwa angali wako kwenye wokovu ni watoto, kuna ambacho unapaswa kufanya kwanza kabla ya magonjwa kuondolewa maishani mwako, ukisoma vyema mstari huo haujasema magonjwa hayatokuja ila yataondolewa na Mungu na hii ni baada ya kumtumikia
Maana nyingine ya Neno hilo la uzima ni kwamba kama utaacha kumtumikia Mungu magonjwa hayatoondolewa na pia yataendelea kuja, kuondolewa kwa magonjwa kumefungamanishwa na utumishi ambao utamfanyia Mungu, na fahamu hili mapema Mungu haitaji kitu kingine chochote kutoka kwako zaidi ya utumishi wako kwake
Lakini hatuwezi kamwe kumtumikia Mungu kama hatumpendi, hivyo hatua ya kwanza kabisa ni kuanza kumpenda Mungu na maana rahisi ya kumpenda ni kulishika Neno lake, naam ni kufanya kile ambacho linasema ufanye Yoh 14:23 "Yesu akajibu, Mtu akinipenda, atalishika Neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake
Kinachokufanya usiumwe siyo kwa sababu wewe ni hodari wa maombi au hodari wa kukaa kanisani ila kwa sababu ni hodari wa kushika na kufanya kile ambacho Neno la Mungu linasema, lakini pia hautaumwa kwa sababu Mungu Baba na Mwana wameweka makao ndani yako, Kama Mungu haumwi nawe hauwezi kuumwa na tunajua hakika Mungu kamwe hawezi kuumwa
Swali la kujiuliza ni
kwa nini uumwe wakati unamtumikia Bwana, wokovu ni kukubali kumtumikia Mungu
ndiyo maana nasema kwa msisitizo haupaswi kusumbuliwa na magonjwa kama
umeokoka! tuendelee tena na sehemu ya pili ya neno endelea pale tulipoishia
jana
Neno ni nini?
Sehemu ya pili, Neno ni hukumu ya Mungu, tambua ya kwamba tupo
hapa duniani kwa muda na safari yetu itatia nanga mbinguni siku moja, penda
usipende kuna siku mwili utatengena na roho na baada ya hapo hakuna hadithi ya
ziada kitakachofuata ni hukumu kulingana na matendo uliyotenda ungali hapa duniani,
ubaya na uzuri wa mbinguni hakuna wakili wa kukutetea kwa maana Wagalatia 6:5 inasema "Kila mtu atauchukua mzigo wake
mwenyewe"
Hukumu kwa lugha ya
kiroho ni stahiki ya malipo anayopaswa kulipwa kila mtu kulingana na matendo
aliyoyatenda angali yu hai hapa duniani, swali la kujiuliza ni kwa nini Neno la
Mungu ni hukumu ya Mungu? kwa nini Mungu hakuweka namna nyingine ya kutuhukumu
zaidi ya kutumia neno lake? Yohana
12:48 "Yeye anikataaye mimi, asiyekubali maneno yangu, anaye amhukumuye;
neno hilo nililolinena ndilo litakalomuhukumu siku ya mwisho"
Neno la Mungu ni hukumu ya Mungu kwa sababu zifuatazo;
Moja, Mungu ni Mungu na habadiliki kamwe, kama kungekuwa na
uwezekano wa Mungu kubadilika Neno lake lisingakuwa hukumu yake, angetuonea na
asingekuwa Mungu wa haki hata kwa mmoja wetu Malaki 3:6 "Kwa kuwa mimi, BWANA, sina
kigeugeu.." KJV imeandika hivi "For Iam LORD, I change not" tafsiri tamu ni "Kwa kuwa mimi BWANA, sibadiliki"
Kutokubadilika huku kwa
Mungu katika Neno lake na hukumu zake ndio kunakutufanya tuwe na uhakika wa
kuwa na afya ya kiungu kupitia ahadi alizozisema katika Neno lake, usikubali
kuwa mhanga wa magonjwa wakati umeokoka labda kama hujampokea Yesu, ni kitendo
cha kumuamini Mungu ili alithibitishe neno lake la afya tizama Isaya 44:26 "Nalithibitisha neno la mtumishi
wangu"
Mtumishi anayeongelewa
hapa siyo mchungaji ni mtu yeyote kumbuka mwanzo nilifundisha hapa kwamba
wokovu umetufanya kuwa wana wa ufalme na watumishi kwa Mungu, kila aliyeokoka
ni mfalme na mtumishi wa Mungu Ufunuo 3:6 "Na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa
Mungu, naye ni Baba yake;..."
Mbili, Neno la Mungu ni sheria, hakuna sheria ambayo haijaandikwa ndio
maana hata Neno la Mungu liliandikwa na manabii, mitume na watumishi wake, ili
sheria yeyote ipate kutenda kazi ni lazima kuwe na utaratibu maalumu wa
kuhukumu ambao umeandikwa kwa suala la kiroho ni Neno la Mungu, lakini pia sheria ya Mungu ambalo ndio Neno lake ni kamilifu na haina upendeleo hata kwa mtu mmoja Zaburi
19:7 "Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA
ni amini, Humtia hekima mtu asiye nayo" kumbuka chochote kinachokwenda tofauti na sheria inavyosema
kinapaswa kuhukumiwa, vivyo hivyo magonjwa ni tofauti na neno la Mungu ni
jukumu lako kuyahukumu
Tatu, Neno la Mungu linaishi milele, kama kwa mfano lingekuwa
linapitwa na wakati kama fasheni za nguo na aina za simu lisingelifaa katika
hukumu lakini Neno la Mungu lipo lilivyo milele, 1Pet 1:25 "Bali Neno la Bwana hudumu hata milele. Na
neno hilo ni neno jema lililohubiriwa kwenu" Kila alichokisema Mungu
ndivyo kilivyo na kitakavyoendelea kuwa hata milele na milele tizama kasema
hivi katika Isaya 53:5 "Na
kwa kupigwa kwake sisi tumepona" amini ndivyo ilivyo
umepona kisha laani huo ugonjwa uone kama hautakuacha
Hivyo nikupe habari
njema kwamba hakuna hukumu mpya yeyote ile, yote yameshaandikwa kwa ajili yako,
Mungu ameshakuambia hukumu itakuwaje kabla hata ya hukumu yenyewe ili ile siku
usije kusingizia hukuwa unafahamu, huu ni muda wa kusoma tena na tena kitabu
cha Ufunuo wa Yohana acha kukikimbia hukumu ndiyo itakuwa vile katika ile siku
kuu ya Bwana na inayotisha
Kwa mfano nikiuliza watu
waliotenda dhambi watakwenda wapi kila mmoja ataniambia ni motoni, umejuaje ni
kupitia neno la Mungu ambalo ndio hukumu ya Mungu, hakuna mafunuo mengine ya
hukumu zaidi ya yaliyopo usitegemee kuna mabadiliko yatatokea wa motoni waende
uzimani hata siku moja, umeulea sana huo ugonjwa imetosha sasa uhukumu kupitia
Neno la Mungu na ukuache acha kuwa mtumwa wa magonjwa na umempokea Yesu
Kumbuka ya kwamba hata
hapa duniani tunahukumiwa kwa maneno ya binadamu mahakamani kulingana na sheria
ya mahakama inavyosema, vivyo hivyo hata mbinguni itakavyokuwa katika siku ile
ya hukumu kila mtu atahukumiwa sawa na Neno la Mungu na kama umekuwa unahukumu
wengine hapa duniani kama wadhambi acha kuchuma dhambi zisizokuhusu siyo jukumu
lako
1Kor 4:5 "Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati
wake, hata ajapo Bwana; ambapo atayamulika yaliyositirika katika giza, na
kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atapata sifa yake kwa
Mungu" hili neno ni zito sana natamani kulielezea
lakini nitakuchosha kwa leo itoshe
Nimalizie kwa kusema
kwamba Mungu hakuja kwa ajili ya wakamilifu au watu wasiotenda dhambi, alikuja
kwa hao walevi, wazinzi, wachawi, masikini, wezi, waongo n.k hakuna haja ya
kuhukumu mtu hata sisi tulikuwa huko ni kuomba neema iliyokuokoa iwaokoe na wao
kwa ajili ya utukufu wake Kristo Yesu, hivi ndivyo tunavyojenga mwili wa Kristo
siyo kwa kuwahukumu
Pia tambua ya kwamba ni
heri mlevi anayeonekana kuliko mchawi asiyeonekana kumbuka katika ile siku kila
kitu kitawekwa wazi, wewe unaeloga wenzio usiku na kumhukumu anayelewa mchana
hata wewe pia utahukumiwa, Neema ya Bwana wetu Kristo na usharika wa Roho
Mtakatifu ukae nasi sote sasa hata na milele, Amen!
YESU NI
BWANA!
Tutaendelea tena kesho.......!
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia
njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe
anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati
wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama
unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka
unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana
nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na
kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga
nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja
tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana