CHUNGA SANA ULIMI WAKO- SEHEMU YA TATU - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Tuesday, September 11, 2018

CHUNGA SANA ULIMI WAKO- SEHEMU YA TATU


Ninakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ni matumaini yangu wewe ni mzima wa afya na unaendelea vyema, kwangu mambo ni mazuri sana nina furaha na amani tele, Mungu anaendelea kuonekana katika kila hatua tunayopiga akijifunua kwa neno la nguvu na kutupatia maarifa mapya kila siku 

Tumekuwa tunaendelea na kichwa cha habari cha chunga sana ulimi wako, kama nilivyosema tokea awali sikuwa nina mpango wa kuandaa somo hili lakini ninashangaa siku hadi siku ninaendelea na somo hili, ikiwa namna hii ninaamini kuna watu wanapaswa kupokea hili kwa wakati huu ndio maana ninakuwa mzito kuendelea na kitu kingine kirefu 

Kama hukujifunza nasi neno la jana la chunga sana ulimi wako sehemu ya pili unaweza ⇒⇒⇒Kubofya hapa kulisoma

Tulipoishia.... 

Wokovu ni stahiki zako ni haki zako unazopaswa kuzipata, wengi hufikiri wokovu ni kwa watu wa kiroho pekee hapana wokovu ni kwa kila mtu ni yale mambo ya msingi ambayo unapaswa kuyapata katika maisha yako ambayo ulikuwa umeyaoteza baada ya Adamu wa kwanza kutenda dhambi


Tunaendelea....
Ninamshuku sana Yesu Kristo na ninajidai ndani ya Yesu, moja ya kitu ambacho nina uhakika umeshakifahamu kwa siku hizi mbili ni tofauti kati ya maneno na neno, maneno ni ya binadamu na neno ni la Mungu, mtu hategwi kwenye Neno anategwa kwenye maneno kwa sababu kwenye maneno mengi kuna uovu

Leo kipekee tutaangalia kipengele cha maneno tunayojitamkia kisha yanasababisha magonjwa kati yetu au yakasababisha uhai, na mwishoni tutaona nini kinakuza imani ya mtu katika eneo fulani

Maneno yanazungumzwa na mdomo ndiyo maana mtu anategwa, lakini neno linazungumzwa na moyo, ni kitu ambacho ni dhahiri na halisi hivyo hakiwezi kumtega mtu, sababu kubwa inayomfanya Mungu aweze kuwa Mungu ni kwamba hazungumzi maneno bali anazungumza neno

Mungu akisema kitu amemaanisha, hasemi kwa kufurahisha au kumfedhehesha mtu La hasha anasema kama jinsi kilivyo kwa sababu neno la Mungu ndiyo Mungu mwenyewe ndiyo sheria yenyewe ndilo linalomuwajibisha Mungu, kama Mungu anaajibika kwa neno lake inakuwaje mwanadamu? Zaburi ya 119:105 "Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia zangu

Mara nyingi watu wakiongea vitu hawamaanishi wanaongea kwa sababu wana mdomo, hivyo watatamka vitu visivyo na maana na ambavyo wao wenyewe haviamini, lakini katika ulimwengu wa roho maneno huchukuliwa na kufanyiwa kazi wakati huo huo, ngoja nikuambie Shetani akisikia umetamka neno moja baya ni neema kwake analitumia hio hilo kukushitaki

1Petro 5:8 "Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze, tambua kwamba hawezi kukumeza kama haujampa nafasi kwa maneno yako

Mara nyingi sana watu wanamuomba Mungu kitu lakini baada ya muda wanaanza kutamka maneno ya kujikatisha tamaa huenda Mungu hataki nipate kitu hiki sasa, au Mungu hajanijibu au Mungu ameninyamazia katika suala hili, ngoja nikuambie hakuna sala ya mwenye haki ambayo haijibiwi, haujapokea kwa sababu adui amepata hati za mashitaka juu yako

1Petro 3:12 "Kwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana uko juu ya watenda mabaya;

Leo tuna wagonjwa wengi wa maneno yao wenyewe, kwetu kuna kisukari, kwetu kuna presha, kwetu kuna saratani sasa kama unasema kwenu kuna magonjwa kwani nini na wewe usiumwe? Mimi wataumwa wote magonjwa yote lakini siyo mimi kamwe, siwezi kuokoka halafu niumwe hili ni agano nililoweka na Mungu na ni lazima nitayaishi maneno yangu 

Mithali 16:24 "Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani, hivyo tamka maneno mazuri juu ya afya yako, juu ya familia yako hivi unapotamka mabaya kwani unataka kuona vitu vibaya maishani mwako?

Ngoja nikuambie kitu kama umeokoka ukiumwa na magonjwa kama malaria, kifua au mafua usinywe dawa, omba mpaka upone hii ndio njia ya kuangalia kama neno la Mungu linafanya kazi, niliumwa malaria siku tatu niliapa sitakunywa dawa nikasema kama Mungu hawezi kuniponya ni bora nife nilitaka athibitishe neno lake Kutoka 15:26 ".......Kwa kuwa mimi ndimi BWANA nikuponyaye"

Ukweli ni kwamba maradhi yapo ndiyo maana kuna uponyaji, ni mpaka uwe kama Yesu ndiyo maradhi yakikuona yanaumwa yenyewe, ila kwa sasa Mungu ameahidi ataondoa maradhi kama ukimtumikia na kuzishika amri zake 

Siongei kujisifia ninamaanisha na nilikuwa kwenye mfungo wa siku tatu, niliumwa kiasi ambacho siku niliyomaliza mfungo nikarudi nyumbani usiku saa sita kitanda changu chote kilijaa maji kuashiria kwamba homa ilikuwa inataka kuniua, ninakumbuka ile siku kama jana vile

Niliamka kwa hasira kali sikuenda kumuomba Mungu tena ile hasira ilinifanya nimwite Shetani kwa nguvu nikamwambia Yesu aliteswa na kusulubishwa kwa dhambi zangu, hii malaria ninajua haitoki kwa Mungu ni wewe umeileta, sasa ninatamka kwa mamlaka niliyopewa ya Luka 10:19 ninaulaani ugonjwa huu katika Jina la Yesu

Muda huo huo na sekunde hiyo hiyo nikapona, ndio maana nina imani ya ukichaa siyo mara moja nimegoma kunywa dawa ni mara nyingi, huwezi kusema Mungu ni mponyaji halafu ukiumwa unakimbilia dawa ni Mungu gani huyo Jee unamwamini? Hizi siyo stori ni maisha yangu halisi sinywagi dawa na sina mpango wa kunywa na Shetani na vibaraka wake wanajua

Ukiona kanisani unaambiwa mchungaji wenu anaumwa na amelezwa hospitalini ujue kuna shida kwenye imani yake, mchungaji unakubalije kuumwa kiasi cha kulazwa hospitali, Jee haufanyi kazi ya Mungu? Kondoo wa Mungu nani atawatumikia? Kama mchungaji wenu anaumwa kiasi cha kulazwa basi ninyi washarika mtakuwa mochwari

Ni muda sasa wa kuacha kutamka Mungu anaweza wakati hatuoni akiweza kwenye maisha yetu, ni muda sasa wa kuacha kusema Mungu ni mponyaji wakati tukiumwa tunawaza kufa, kama anaweza hakikisha una vithibitisho, kama ni mponyaji ukiumwa acha kukimbilia hospitali mwambie niponye nikujue kwamba kweli wewe ni Mungu

Tafuta neno la Mungu juu ya uponyaji kisha simamia neno hilo mpaka akuponye hivi ndivyo tunavyomuweka Mungu kwenye majaribu ndivyo tunavyombananisha mpaka atupatie tunachotaka Jer 1:12 "Umeona vyema, kwa maana naliangalia neno langu, ili nilitimize

Kasome tena habari za watumishi wa Mungu kwenye neno la Mungu ni wapi walipokuwa wanaumwa, Mungu anasema ukinitumikia nitaondoa magonjwa kati yenu, inapaswa unapoumwa ndiyo uwe unaumwa ugonjwa wa kukuuwa kama Elisha siyo unaumwa na kulazwa mara unaibuka hii siyo fungu langu kama unamtumikia Mungu wa namna hiyo mimi nimeshatoka huko 2Wafalme 13:14 "Basi Elisha alikuwa ameshikwa ugonjwa wake uliomwua;...

Na magonjwa ni maneno tunayoyatamka wenyewe siyo kitu kingine, na magonjwa tukiyatamkia Neno la Mungu yanayeyuka hapo hapo, unahitaji muujiza kidogo tuu ili kuweza kumuamini Mungu zaidi ninaandika hivi kwa sababu nina vithibitisho huku sio kujidai ni imani niliyonayo ndani ya Yesu wangu, maadamu nipo na Yesu hakuna mchawi wala ugonjwa unaoweza kunizidi nguvu

Huenda hauamini kwa sababu unafikiri ni mpaka uombewe na mtumishi fulani ndiyo utapokea, lakini leo acha nikuambie ukweli huu mtu anayeweza kujiombea mwenyewe na akapona pasipo msaada wa mwingine ndiye Imani yake inakua

Tutaendelea.......


Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote

Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;


SALA YA TOBA

Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa


Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani

Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.


Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu 


Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana


Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa
whatsup nambari 0715113636

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana