Ninakusalimu katika Jina lipitalo majina yote, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, nina imani kubwa kwamba wewe ni mzima wa afya na unaendelea na kazi zako vyema, huu ni wakati mwingine ambao Roho Mtakatifu anataka kutufundisha neno la Mungu kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe
Ninakukaribisha ujumuike nami katika kujifunza neno hili la uzima, mwalimu au mhubiri anapofundisha neno naye hujifunza kwa wakati huo, Mungu akubariki unapoenda kujifunza neno lake siku hii ya leo katika Jina la Yesu Kristo ukutane na neno lako, Amen
Tulipoishia....
Hivyo ili uweze kupona katika sehemu hizi ambazo malango yake siyo ya haki ni lazima uhakikishe kwamba unamuomba Yesu Kristo akufungulie Zab 118:17 "Nifungulieni malango ya haki, nitaingia na kumshukuru BWANA, hapo ndipo utakapoweza kuzishinda nguvu za malango yasiyo ya haki
Leo tunaendelea na somo hili la malango ya kiroho sehemu ya saba na leo tutajifunza juu ya malango ya ukoo au familia, kumbuka katika siku ya jana tuitizama malango ya mji na namna ambavyo Shetani anatumia malango hayo kuharibu hatma za watoto wa Mungu. Kama hukusoma somo la jana kipekee unaweza ⇒⇒KUBOFYA HAPA KULISOMA
Endelea.....
Familia zetu zimetokana na koo tofauti, ninamaanisha mwanamme anapoowa au mwanamke anapoolewa anakwenda kwenye familia nyingine na kufanyika mwili mmoja na mme/ mke wake lakini wote wawili kila mmoja ametoka katika ukoo wake ambapo kila ukoo una mila, tamaduni na utaratibu wake
Katika koo tunazotokea huwa kuna malango ambayo hutengenezwa na waliotutangulia, yaani mababu na mabibi zetu hawa kama wakienenda katika njia ya haki hata kizazi kinachofuata baada ya wao kuondoka kitakuwa katika haki kwa sababu hakuna lango la kumruhusu Shetani kutoa mashitaka juu yetu
Ukweli ni huu kwamba wokovu wetu haujakamilika kama bado kuna hati za mashitaka juu yetu, kama umeokoka na kumkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako haupaswi kusumbuliwa na kifungo cha aina yoyote, iwe ni fedha, magonjwa, kukosa uzao, kutokuolewa, hasira n.k
Ufunuo 12:10 "Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele ya Mungu wetu, mchana na usiku
Mshitaki anayeongelewa hapa ni Shetani na tunajua ya kwamba hawezi kutushitaki kama hana haki za kisheria zinazomruhusu kutushitaki, tukumbuke ya kwamba Mungu wetu ni mwaminifu na wa haki na humlipa kila mtu sawa na matendo yake Warumi 2:6
Kinachompatia Shetani haki ya kutushitaki ni malango ambayo tumeyafungua kwa ajili yake kupitia dhambi, laana pamoja na uovu anatumia vitu hivi kuwashitaki mbele za Mungu na ndio maana watu wengi wapo kwenye vifungo ambavyo wanatamani kutoka lakini wanashindwa, lakini kwa uvuvio wa neno unalosoma hapa Yesu Kristo anakwenda kukutoa katika kifungo hicho
Baada ya mfululizo wa somo hili kwa msaada wa Roho Mtakatifu nitaandika sala maalumu kwa ajili ya kuweza kukuchomoa katika kifungo chochote kile kwenye malango ya sehemu unapotokea au ulipokwenda hivyo endelea kujifunza na tengeneza hasira ya kiungu ya imani
Hivyo Shetani anaweza kuingia katika malango yako kama kuna moja kati ya mambo haya;
Jambo la kwanza ni Uovu, uovu ni dhambi ambayo imekomaa hata ikapita kutoka kizazi kimoja hata kingine dhambi hii hufungua milango ya magonjwa na mahangaiko kwa mfano babu zako na bibi wanaweza kuwa sababu ya magonjwa ulionayo, dhambi iliyofanywa na mababu au mabibi inayohusisha ushirikina, uchawi, umwagaji damu, ibada za kafara na haikutubiwa ni moja ya njia ya malango ya Shetani
Maombolezo 5:7 "Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao, hivyo haijalishi ulikuwepo au haukuwepo lakini kama upo katika ukoo husika uovu huo utakuhusu ni mpaka utakapoamua kushughulikia suala hili, mstari wa pili unasema "Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni; na nyumba zetu kuwa mali ya mataifa
Uovu unaweza kusafiri kupitia cheneli zifuatazo inawezekana kwenye dhambi inayojulikana au isiyojulikana, nadhiri, viapo vinavyohusisha damu, nchi kwa watu wake kwa mfano Jer 3:6-10, kuasi, kurithi kwa wazazi mwanz 16:1 pia inawezekana kupitia majina 1Nyak 4:9-10 "Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nilimzaa kwa huzuni
Jambo la pili ni laana, laana ni tamko hasi ambalo husemwa kwenye maisha ya mtu, familia, kundi la watu au nchi ukisoma Biblia kuna mtu alikuwa anaitwa Baalamu huyu alikuwa kazi yake ni kutamka laana na baraka kwa mataifa na watu Hesabu 22:6 "Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi
Jambo la tatu ni dhambi, hii ni kwenda kinyume na neno la Mungu siri ni hii laana na uovu unaendelea kuwepo kwenye maisha ya mtu au familia fulani alimradi tuu wanafanya dhambi hivyo njia ya kiuhakika ni kufunga malango haya ambayo yanatumiwa na Shetani
Tufanyeje sasa ?
Tunapaswa kuidai kufungua malango kwa nguvu suala la kudai haki na stahiki zako siyo lelemama ni mapambano ndio maana Mathayo11:12 inasema "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
Haukai kuongea maneno na kutangaza kwamba naumwa naumwa, kwetu hatuolewi, kwetu hatufanikiwi, kwetu hatupendani bali unazivaa silaha unaingia kwenye ulimwengu wa Roho unapigana kuidai stahiki zako kiungu, ukiwa na ufahamu pamoja na maarifa sahihi
1Kor 4:20 "Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu, hizi nguvu siyo za mwili ni za Kiroho hivyo ni lazima kujijenga katika eneo la Kiroho matokeo yataonekana nje tuu, watu watamjuaje Yesu tunayemtumikia kama hatendi matendo makuu katika maisha yetu?
Tutaendelea...... Kusoma makala nyingine inayofanana na hii unaweza⇉⇉ KUBOFYA HAPA KUSOMA YOTE
Kumbuka hakuna kitakachofanya kazi kama usipomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi ya maisha yako leo, anayeleta mabadiliko halisi na ya kweli ni Yesu peke yake ndiyo maana leo anakuambia Hebr 3:15 "Leo kama mtaisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama wakati wa kuasi,
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana