Bwana Yesu asifiwe! Ninatumaini unaendelea vizuri katika siku hii njema ambayo Bwana ameifanya kwa utukufu wake, Mimi pia ni mzima wa afya na nimejawa na furaha na amani tele, Roho Mtakatifu aliye mwalimu mwema katika siku hii ya leo akakufundishe na kukuonesha kile alichoandaa kwa ajili yako
Tumekuwa na siku tatu tukifundishana juu ya somo la chunga ulimi wako kama nilivyosema sikuwa nimepanga somo hili lakini ninashangaa ninaendelea nalo na leo pia tutaendelea nalo sehemu ya nne, kuna kitu maalumu sana kwa ajili yako siku ya leo na Mungu akubariki sana
Kama hukusoma sehemu ya tatu ya somo hili la Chunga sana ulimi wako unaweza ⇒⇒⇒Kubofya hapa kulisoma
Tulipoishia.....
Huenda hauamini kwa sababu unafikiri ni mpaka uombewe na mtumishi fulani ndiyo utapokea, lakini leo acha nikuambie ukweli huu mtu anayeweza kujiombea mwenyewe na akapona pasipo msaada wa mwingine ndiye Imani yake inakua
Tunaendelea.....
Ninaposema chunga sana ulimi wako ninamaanisha usizungumze mambo ambayo hupaswi kuzungumza au ambayo hayana maana, tunamtumikia Mungu ambaye anataka tuwe na maneno mawili tuu lakini wengi wana maneno matatu na hii ndiyo inayosababisha matatizo kwa watu wengi
Ninaposema Mungu anataka tuwe na maneno mawili ninamaanisha ndiyo au hapana, kama unataka kitu maneno yako yaoneshe unakitaka kama hautaki kitu maneno yako yaoneshe kukikataa hii ndiyo maana halisi ya ndiyo au hapana, ubaya wa watu wana maneno mengi yasiyo na maana sehemu ya kusema ndiyo au hapana wanazunguka kujitetea
Bora ukawa wazi kwenye maamuzi yako kwa sababu wengi wanateseka kwa sababu wanataka kukaa katikati, hawasemi maamuzi yao juu ya mambo fulani, mtu muwazi ndiye anayeishi maisha anayoyataka ndiye mtu pekee anayeweza kusema ndiyo au hapana, ukijidai unafichaficha mambo yako unakuwa mtu wa katikati
Mathayo 5:37 "Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo;Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu
Kama ninataka kuwa mimi ninapaswa kuwa huru, siyo mimi wazazi wangu wanaotaka niwe, siyo mimi rafiki zangu wanaotaka niwe, siyo mimi ndugu zangu wanaotaka niwe bali mimi ninaetaka kuwa mimi, wengi wanateseka na kusema maneno ya kuzunguka zunguka kwa sababu hawajaamua kuwa wao, mimi nilishafanya uamuzi wa kuwa mimi, hakuna anayeweza kunibadilisha
Ninatambua ya kwamba nipo hapa kwa muda mchache lazima nifanye kile ambacho moyo wangu na roho yangu unapenda, siyo kile ninachoamuliwa na watu kufanya, upo kwenye utumwa kwa sababu huwezi kufanya maamuzi yako mwenyewe na siku ukitoka huko maneno yako yatakuwa machache utakuwa mtu wa ndiyo au hapana
Muda wa kuishi maisha ya wengine umeisha, anza kuishi maisha yako kwa kusema na kufanya kile unachokitaka siyo unachoamuliwa ni mfungwa tuu anayefanyiwa maamuzi kama umeokoka umekuwa huru tena kweli kweli, sababu kubwa ya kuwa makini na maneno tunayoyaongea ni kwa sababu siku ya hukumu kila mtu atahukumiwa sawa sawa na maneno yake
Mathayo 12:37 "Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa, tambua hilo leo hukumu siyo matendo tuu hata maneno pia ndiyo maana inakubidi uache kuongea hovyo hovyo vitu visivyo na msingi na umbea uache, mambo yasiyokuhusu achana nayo kitu cha kushangaza ni kwamba umbea huwa haumhusu mtu anayeutamka ni wakati wa kuzungumza mambo yako sasa umeongea ya wengine vya kutosha na hayajakusaidia
Watu wengi ni wadaku wanachunguza maisha ya wengine kuliko wanavyojichunguza binafsi katika kufanya hivi wanatenda dhambi ya kuhukumu, kama jambo halikuhusu achana nalo utajiepushia mengi, utaokoa muda na dhambi zitakukimbia pia Mithali 11:13 "Mwenye udaku hupitapita akifunua siri; bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo
Kipimo cha utu uzima siyo umri au ndevu ni uwezo wa kusikia mambo na kuyapuuzia au kuyafanyia utatuzi kama yanakuhusu au umehusishwa na siyo kutangatanga ukisambaza habari za watu ambazo hazikuhusu na ambazo hazibariki wengine
Halafu watu wengi hawafahamu maana halisi ya kuokoka na kuwa na dini, maana yake ni kubadilika mwenendo wako na kuuchunga ulimi wako, mtu yeyote aliyeokoka halafu ana maneno mengi huo wokovu wake una shida, ni lazima ujue wakati wa kufungua kinywa na wakati wa kufunga kwa ajili ya utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo
Maana ya kuokoka ni kufanana na Yesu kama unasema umeokoka halafu kutwa kucha unaongea kama radio ya mbao ndugu yangu unamwaibisha Yesu, kwanza hayupo hivyo haongee hovyo mbona kuna mambo mengi sana ya kufanya kuliko kuongea hovyo? Yakobo 1:26 "Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hazuii ulimi wake kwa hatamu, ili hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai
Ulimi unaobariki ndiyo unaolaani ni suala la kujua namna ya kuutumia, lakini pia usipende kuongea mambo yasiyo na maana na watu ambao wameasi kwa nini kujichanganya nao? Ipo sababu maalumu ya kuzungumza nao ambayo ni kuwaonya juu ya uovu wao ni kuitangaza hukumu ya Bwana kwao ni kuwaambia Mungu anawapenda na anataka warudi kwake, habari za kupiga soga zisizo na maana kama umeshampokea Yesu achana nazo
Kuna umuhimu mkubwa wa kuzuia kinywa chako, unajiepusha sana na mambo mengi, ugomvi mwingi na mapigano na mafarakano yanayotokea yanasababishwa na kinywa namna ambavyo mtu anavyoongea aina ya maneno anayotumia, unaweza kuepuka haya kwa kulinda kinywa chako na kuacha kuongea hovyo Mithali 21:22" Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu
Kama umempokea Yesu na unasoma Neno la Mungu unapaswa kuongea maneno ya hekima, kama bado hujafikia hatua hiyo bado una safari ya kusafiri zaidi lakini pia tambua wokovu maana yake ni kuwa na nidhamu kufanya mambo ya msingi tuu unayopaswa kufanya na kuwaacha wapumbavu waendelee na upumbavu wao Mithali 10:31 "Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima; Bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali
Wakati mwingine nina maneno magumu lakini tambua kwamba wokovu haukamiliki kwa siku moja, inawezekana umeokoka lakini bado ni mbea na mnafiki, ukiendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu ataendelea kukubadilisha taratibu mpaka utakapokamilika, tabia mbaya ni kama ngozi ni neema ya Mungu pekee inaweza kuiondoa, Mithali 27:17 "Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake
Kubwa zaidi penda kujifunza, noa akili yako na neno la maarifa na ufahamu kwa watu unaowaamini na unaoona wana kitu, hivi ndivyo tunavyobadilika na kukua kutoka kwenye tabia mbaya na kuingia katika tabia nzuri inayovutia na kupendeza, wokovu ni safari kuwa tayari kuisafiri na furahia kila linalokuja njiani wakati unaelekea kwenye kile Mungu alichokuandalia
Mtume Paulo baada ya kumaliza safari yake alitamka maneno haya 2Tim 4:7 "Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda, hauwezi kufikia hatua hii kwa kuongea hovyo wala kwa kutokuwa na muda wa kutosha kujifunza neno la maarifa Mtume Paulo alikuwa anasoma sana kila aliposafiri alimuambia Timotheo abebe vitabu vyake
Ninatamani kila mtu anapofikia mwisho wa safari yake atamke maneno hayo, hili linawezekana kwa kila anayeamini, Mungu akulinde na kukuongoza kufikia kile ambacho amekusudia maishani mwako, Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo ikae nasi sote. Amen
Itaendelea tena....
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana