Ninakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ni matumaini yangu wewe ni mzima wa afya na unaendelea vyema, kwangu mambo ni mazuri sana nina furaha na amani tele, Mungu anaendelea kuonekana katika kila hatua tunayopiga akijifunua kwa neno la nguvu na kutupatia maarifa mapya kila siku
Tulipoishia......
Itoshe sasa anza kumuita Mungu kwa kinywa chako, muambie unampenda na unalipenda neno lake, mwambie upo tayari kusikia kutoka kwake na utaona mambo yakibadilika kuwa mazuri kwako, Zaburi 66:17 “Nilimwita kwa kinywa changu…..
Kwa kawaida jumamosi huwa hatuna mafunzo ni muda wa kupangilia mambo yangu na kutafakari wema wa Mungu maishani mwangu lakini leo kwa kifupi sana nimeandaa somo hili kuna kitu ambacho utajifunza hapa kama hukusoma chunga sana ulimi wako sehemu ya tano ⇒⇒⇒bofya hapa kulisoma lote
Tunaendelea.....
Ni lazima tuwe sana makini na ndimi zetu kwa sababu ndimi ni kama nyembe, ukali wa maneno yanayotamkwa na ulimi unaweza kuleta madhara kama ya mtu aliekatwa na kiwembe, kila aina ya ugomvi au kutokuelewana sehemu yoyote husababishwa na ulimi, Zaburi 52:2 "Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila
Hii ndiyo maana kama katika maombi yako ulikuwa huna ombi la kumuomba Mungu akuponye ulimi wako na hila inabidi kuanzia sasa uwe na ombi hili, kwa sababu matatizo mengi yanasababishwa na sisi wenyewe wala hata siyo Shetani, ni maneno tunayotamka ndiyo yanatuletea madhara
Kuongea maneno ya uwongo na kuongea maneno yasiyokuhusu ni ugonjwa, mtu anayesema maneno ya hila hana tofauti kabisa na mgonjwa wa kisukari au wa presha, na inambidi amuombe Mungu amponye kama anavyoponya wagonjwa wengine, Zaburi 120:2 "Ee BWANA, uniponye, Na midomo ya uwongo na ulimi wa hila
Nikupashe habari kwamba ulimi unazuiwa, unajichunga na unanuia kabisa sitaongea mambo ambayo hayanihusu siyo suala tuu la kuomba uponywe ni lazima uchukue jitihada za kujizuia kumbuka wokovu ambao haukuwajibishi siyo wokovu ni uvivu huo, ni lazima uwajibike kwa kila neno linalotoka kinywani mwako uwe umelichuja na kulifikiri
Mithali 29:20 "Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki (mwenye uharaka) katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye
Lakini pia ni muhimu kufahamu ya kwamba Mungu hakutupa ulimi wa kujipendekeza kwa watu wala wa kukiri maneno ya udhaifu, tumepewa ulimi wa uhodari na ujasiri haijalishi ni hali gani unapitia kamwe hakuna kutamka wala kukiri udhaifu ni wewe na Mungu wako mpaka kieleweke na siyo namna nyingine
Mithali 26: 28 "Ulimi unenao uwongo huwachukia wale uliowajeruhi; na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu
Tena Mungu anasema ataikata kabisa midomo ya kujipendekeza, na ulimi unenao maneno ya kiburi, hauna haja ya kujipendekeza kwa binadamu mwenzio ya nini kumtumainia mtu ambaye naye hajakamilika? Tunajipendekeza kwa Mungu sababu ni mkamilifu na anawalipa tahawabu wote wamtumainio
Zaburi 12:3 "BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Na ulimi unenao maneno ya kiburi;
Tambua ya kwamba unao ulimi lakini siyo wakwako kila kitu umeazimwa na Mungu ndiyo maana Mungu ni Bwana wako, usifikie hatua ya kuona unaweza kutumia viungo ulivyopewa unavyojisikia, wala kutamka maneno kwa kuzitumainia nguvu zako mwenyewe kumbuka hata unabii unaojifanyia ni kwa kuutafuta kwenye neno la Mungu
Zaburi 12:4 "Waliosema kwa ndimi zetu tutashinda; Na midomo ni yetu wenyewe, ni nani aliye bwana juu yetu?
Nikutakie wik-end njema na yenye kupendeza......
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa

Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636

No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana