MALANGO YA KIROHO--SEHEMU YA KWANZA - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Monday, August 6, 2018

MALANGO YA KIROHO--SEHEMU YA KWANZA

CO-Founder at MT Sialove Lukumay

Namshukuru Mungu kwa ajili yako kwa sababu amekuwa mwema kwako hata kwangu pia, tlikuwa na siku kama nane tukijifunza neno la Mungu lenye kichwa cha habari Kubali kubadilika, katika somo la jana tuliangalia juu ya uamsho ambao unatokea sasa katika bara la Afrika na mambo ambayo vijana wanafanya

Nilipaswa kuendeleza somo la Kubali kubadilika siku hii ya leo lakini nimekawia kuliandaa hivyo nimeona ni vema kama tukijifunza somo hili jipya kwa siku ya leo ambalo lilikuwa tayari limeandaliwa kwa ajili yako, hivyo nitakapokuwa na wakati mzuri zaidi tutaendelea na somo la Kubali kubadilika angalau makala mbili za mwisho


Katika maisha tunayoishi hapa duniani binadamu ana uwezo wa kuingia na kutoka, na ili tuweze kuingia au kutoka sehemu yoyote ile kwenye maisha tunahitaji kuutafuta mlango ulipo Yesu alikuwa na maana kubwa sana alipokuwa akisema maneno haya Math 7:7 "ombeni nanyi, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni nanyi mtafunguliwa;


Kubisha kunakozungumziwa hapa siyo kwa mlango wa kawaida kama wengi wanavyofikiri, ni kubisha katika ulimwengu wa kiroho, kukataa na kupingana na kila nguvu ambayo inazuia na inakinzana na kile ambacho Mungu ameandaa kwa ajili yako


Lakini kufahamu mlango ulipo na kukosa ufunguo wa kufungulia mlango ni changamoto, nakumbuka kipindi fulani nilisahau ufunguo kwenye gari la ofisini na kwa bahati mbaya nilishakwenda umbali mrefu, ilinibidi nirudi kazini kuufuata ufunguo


Kama haukusoma neno la Mungu la jana la kubali kubadilika sehemu ya nane⇒⇒⇒ BOFYA HAPA KUISOMA YOTE 


Hivyo kufahamu mlango ulipo na namna ya kuufungua ni mambo mawili tofauti, lakini mtu ambaye angalau anafahamu mlango ulipo hata kama hana ufunguo amemzidi yule ambaye hafahamu na yupo kwenye nafasi nzuri ya kupata ufunguo na kufungua  mlango


Haijalishi una umbo kubwa kiasi gani kama hauna funguo ya kufungua malango ya nyumbani mwako hutoweza kuingia ndani, haijalishi umewahi kuzaliwa au una miaka mingi kiasi gani kama haufahamu mlango na ufunguo sahihi wa kupata unachokitaka maishani mwako jua kabisa hautakaa ukipate kamwe


Kupata kitu chochote katika maisha kunahitaji mpango, naamu maandalizi muhimu na maalumu kwa mfano maandalizi ambayo mzazi anayafanya ya kumpeleka mtoto shule ya serikali na ya binafsi ni tofauti kabisa, maandalizi ya kusafiri ndani ya nchi na ya kwenda nje ya nchi ni tofauti kabisa


Aina ya mlango unaotaka kufungua kwenye maisha yako au kuufunga inategemeana sana na ni mlango wa aina gani na hata mbinu na mikakati itakayotumika ni tofauti kabisa Math 18:18 "Amin, nawaambieni, yoyote mtakayofunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayofungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni


Mwalimu wangu aliwahi kuniambia hakuna neno lolote lile limeandikwa kwenye Biblia kwa bahati mbaya, jua lipo kwa sababu malumu kama hujaelewa muombe Roho Mtakatifu akupatie mafunuo au mfuate mtu unaejua amekuzidi kiwango cha Kiroho aweze kukufafanulia vyema


Sasa nimefikia hatua ya kuelewa alichokuwa ananiambia ninaelewa kwamba nikiambiwa ardhi ina kinywa Mwanzo 4:11 “ Basi, sasa umelaaniwa wewe, katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kutoka kwako, hii inamaanisha ardhi inaweza kumeza na kutapika na kama ni hivyo basi ni lazima yapo malango ya ardhi naam upo mlango wa kuingia katika ardhi


Hivyo sichukulii kirahisi mstari wowote ninaousoma kwenye Biblia kirahisi ninajiuliza mara mbili unamaanisha nini na nikishindwa kuulewa katika hali ya kawaida naomba tena msaada wa Roho Mtakatifu na njia hii imekuwa inanipatia maana ya mistari mingi ninayoisoma



Binadamu naye ana milango ambayo vitu hupita kupitia hiyo, milango mikuu miwili ambayo ni macho na masikio, kitu chochote huingia katika akili kupitia masikio au kuona Biblia inasema kwenye Warumi 10:17 “ Basi imani chanzo chake ni kusikia ; na kusikia huja kwa neno la Kristo, Bartimayo kilichoamsha imani yake ni kusikia ndio maana japokuwa hakuwahi kumuona Yesu kwa macho lakini alisikia kwamba anaponya na aliamini ndio maana alipokea uponyaji wake


Kumbuka hakuna kitakachofanya kazi kama usipomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi ya maisha yako leo, anayeleta mabadiliko halisi na ya kweli ni Yesu peke yake ndiyo maana leo anakuambia Hebr 3:15 "Leo kama mtaisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama wakati wa kuasi,

Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote


Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;



SALA YA TOBA


Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa


Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani


Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.


Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu 


Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana



Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa
whatsup nambari 0715113636



Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote":.

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana