CO-Founder at MT Pendo Wisso |
Bwana Yesu asifiwe! Namshukuru sana Mungu aliyekulinda mpaka wakati huu sifa na utukufu ni kwake peke yake, juma lililopita tulikuwa na mfululizo wa makala ya kubali kubadilika na bado siku hii ya leo nazidi kuchochewa rohoni niendelee na neno hili la mabadiliko na leo tukiwa sehemu ya nane
Tunapaswa kutambua kwamba tupo katika majira ya nyakati za mwisho, na wale ambao wanaokubaliana na kipindi hiki cha majira ya uamsho ndio walio katika nafasi ya kufanikiwa na kuendana na maandiko ya neno la Mungu
Kama hukusoma sehemu ya ya saba ya makala hii kubali kubadilika ⇉⇉⇉BOFYA HAPA KUISOMA YOTE
Uasho ni mwamko mkubwa sana wa neno la Mungu kwa viongozi wa dini na waumini kwa ujumla, ni kiu na shauku kubwa ya kutaka kumjua Mungu na kumtumikia, ni kutaka kuishi maisha ya utakatifu na kiu kubwa ya neno la Mungu
Kipindi hiki cha uamsho kimeanzia Afrika, Mungu kwa matendo yake makuu amehamisha utawala na ukuu wa kanisa kutoka bara la Amerika na Ulaya na kuuleta Afrika na huu ni mpango mkuu wa Mungu kwa kanisa lake, sasa katika bara la Afrika ndio kuna makanisa makubwa zaidi duniani kuliko mabara mengine
Mungu analeta mabadiliko haya makusudi kabisa na analithibitisha neno lake la Yoel 2:28 " Hata itakuwa baada ya hayo, ya kwamba nitaimimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu wa kiume na wa kike, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono
Mungu ameshaanza kuthibitisha haya vijana wemeanza kutawala sehemu mbalimbali, hata katika uongozi wa nchi yetu utaona kwamba kuna sura nyingi za vijana tofauti na kipindi cha nyuma ambapo tulizoea ni wazee ndio wanaoongoza kwa sababu ya hekima na maarifa, lakini sasa roho ya maono imemwagwa kwa vijana na ndio wanaoweza kuongelea nyakati zijazo sasa
Tumeona pia vijana wengi wakifanya mambo makubwa na ya ajabu katika kipindi hiki cha uamsho na wengine wakivunja rekodi za kidunia hata kuingia katika orodha za watu matajiri zaidi ulimwenguni mfano Mark Zuckerberg, Elon Musk nk hii yote inathibitisha kipindi cha mabadiliko yaani uamsho katika dunia hii
Katika kipindi hiki ile tabia ya kusema naomba niombee, niombee inaanza kupotea na watu wanataka kupata mabadiliko yanayodumu ndio maana Mungu amemimina kwa nguvu kiu na shauku ya neno lake kwa watu ili waweze kumjua na kujua namna ya kujisimamia wenyewe
Kipindi hiki kipo maalumu kwa ajili ya kuwakumbusha watu ya kwamba katika dunia hii hakuna mtu ambaye anapaswa kuendesha maisha yako, wala kukupangia cha kufanya ila wapo tuu ambao wanaweza kukupatia maarifa ya kuendea kile ambacho unakihitaji kwa njia rahisi na kwa utaratibu maalumu, hii ndiyo sababu kubwa ya Mungu kumimina kiu ya kusoma neno la Mungu
Mungu anataka kila mtu amjue na aanze kutenda na kuishi katika kusudi ambalo amemuandalia, Yoh 7:28-29 " Basi akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenituma ni wa kweli, msiyemjua ninyi, Mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma
Katika majira haya ya uamsho watu ambao wanaosoma sana ndio wanaopata maarifa mapya, wanaofahamu namna mbalimbali za kutatua changamoto na wanaofanya mambo makubwa kutokea , wale ambao wanaobadilika kuendana na majira haya ndio wanaoirithi nchi Isaya 1:19 "Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi
Tumekuwa tunashuhudia katika kipindi hiki makanisa yakijaa kupita kawaida na watu wengi wakitubu na kuokoka kuliko kipindi cha nyuma, watu wameanza kuelewa Mungu wa kweli yupo na anatenda matendo makuu Ufunuo 2:5 "Basi kumbuka ni wapi ulipoanguka; ukatubu ukafanye matendo kwanza, ukafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako mahali pake, usipotubu
Ili kuweza kuendana na kasi ya kipindi hiki cha uamsho ni lazima uwe tayari kubadilika na kukubaliana nacho ndipo Mungu anapoweza kufanya suala lako kuwa jipya, kipindi cha mabadiliko ya hali ya hewa wakati wa baridi ukifika huwa tunavaa nguo za pamba na masweta kamwe hatulaani wala kukitaa kipindi hiki na kipindi cha joto tunaacha kuvaa nguo za pamba, hivyo njia njema ya kuendana na mabadiliko ni kubadilika nayo
Kipindi hiki cha uamsho kinatupeleka katika sehemu mpya kiroho, kiuchumi, kiutawala, kiutamaduni ambayo hatukuwepo awali na hii inadhihirisha nguvu na uweza wa Mungu katika matendo yake, wale wenye neno la Mungu ambalo ndiyo taa ya maisha ndio wanaoweza kudumu katika kipindi hiki cha uamsho
Mungu amenipa ujumbe huu asubuhi ya leo, uwe maalumu kwa ajili yako, Mimi sijui unaona uamsho katika sehemu gani kwenye maisha yako, katika kipindi hiki wale ambao walitambua kusudi la kuja kwa Yesu ndio wanaoweza kuona udhihirisho wa nguvu na utendaji wake
Yesu Kristo hakuja duniani kueneza dini bali kuueneza ufalme wa Mungu, Math 4:17 "Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia, bahati mbaya wengi huchanganya dini na ufalme wa mbinguni, dini ni utaratibu fulani tuu wa kumwabudu Mungu ambao unatumika hapa duniani na ndiyo maana mbinguni hakuna dini kuna ufalme
Roho za udini ndizo zilifanya Yesu kusulubishwa na kuuwawa, ni vyema ukafahamu kwamba dini haitupeleki mbinguni, ila siku ambayo utagundua siri hii kubwa ya Yesu kuja duniani na kuiishi Injili utakuwa na uhakika wa kwenda mbinguni pamoja naye
Kumbuka hakuna kitakachofanya kazi kama usipomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi ya maisha yako leo, anayeleta mabadiliko halisi na ya kweli ni Yesu peke yake ndiyo maana leo anakuambia Hebr 3:15 "Leo kama mtaisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama wakati wa kuasi,
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote":
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana