MALANGO YA KIROHO- SEHEMU YA NNE - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Thursday, August 9, 2018

MALANGO YA KIROHO- SEHEMU YA NNE

CO-Founder at MT Pendo Wisso

Bwana Yesu asifiwe! Namshukuru Mungu aliyetuwezesha kuiona tena siku hii njema ya leo ni kwa uweza wake pekee na siyo uwezo wetu, huu ni upendeleo wa ajabu ninalisifu na kuliinua Jina la Yesu Kristo ambaye ni Bwana na mwokozi wa maisha yetu


Tumekuwa na siku tatu nzuri za neno la Mungu lenye kichwa cha habari cha malango ya kiroho, ninamshukuru Mungu ambaye kupitia Roho Mtakatifu ananifunulia neno la kuandika kila siku ambalo ni jipya na linaloleta migeuko katika maisha ya watu wake, ninashukuru pia kwa kila ambaye anatuma ujumbe kushukuru na kusema namna Mungu alivyombariki katika neno


Leo pia tutaendelea na neno lile lile la Malango ya Kiroho sehemu ya nne, ninaomba Mungu akakutane na hitaji lako unavyokwenda kusoma neno lake katika Jina la Yesu Kristo aliye hai, Amen


Tulipoishia jana....


Hii ni siri ambayo unapaswa kuifahamu mtu ambaye anafahamu kusudi lake na akawa analifanyia kazi anaweza kukaa bila fedha  maadamu moyo wake unakuwa umetulia na unaangalia sehemu moja ole inakuwa kwa yule ambaye hajui cha kufanya na hela hana ndio wizi huanzia hapa, kukata tama, hofu ambayo huletwa na Shetani na kuonesha kwamba hakuna ambacho kashafanikisha n.k


Kama hukusoma neno la Mungu la jana la malango ya kiroho sehemu ya tatu ⇒⇒⇒BOFYA HAPA KUISOMA YOTE


Endelea hapa leo....


Hivyo tunakuwa kwenye mlango mwembamba pale tunapokuwa tunatembea kwenye kusudi la kuumbwa kwetu, kadiri tunavyokuwa waaminifu Mungu anatufanyia kitu kingine Mungu anasema katika Luka 16:10 "Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia, ili tuweze kupokea mambo makubwa lazima tuoneshe uaminifu katika yale madogo tunayopewa
ndipo Mungu hutufungulia mlango mkubwa 1Kor 16:9 “ Kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, hivyo Mungu huupanua zaidi mlango wako kadiri unavyokuwa mwaminifu katika kusudi alilokupatia


Siyo biashara kumi zinafungua mlango wa biashara kumi bali ni biashara moja ulioianzisha ndio itazaa biashara kumi maadamu tuu utakuwa mwaminifu, kwa kushirikiana na Mungu katika biashara yako na kuifanya kwa nguvu na maarifa yako yote


UFUNGUO WA MLANGO UKO WAPI?


Neno la Mungu linasema kwamba lolote ambalo tutalifunga hapa duniani na mbinguni litakuwa limefungwa, na tutakalofungua hapa dunianiani na mbinguni litafunguliwa Math 18:18 kama kuna kufunga na kufungua basi kuna mlango na kuna ufunguo


Yupo mtu ambaye alishajitoa kwa ajili yetu ili kuuchukua ufunguo, hivyo muda huu Yeye ndiye mwenye funguo na anazo funguo zote naam ana master key ambayo ni ya uzima na mauti ni uamuzi wako kuamua unataka kuutumia ufunguo upi, umeshamfahamu ni nani? Si mwingine ni Simba wa kabila la Yuda naam Yesu Kristo mwenyewe ndiyo mwenye funguo za milango yote


Funguo hizi ameshatupatia na tunakaa nazo nyumbani mwetu, wengine huzitumia jumapili kwa jumapili, wengine hawazifahamu kabisa na wengine wanaotambua siri yake wanaziangalia kila siku na funguo hizi siyo kitu kingine bali ni neno la Mungu


Kila aina ya kifungo kinachomsumbua mtu iwe ni cha kurithi, cha kuzimu, majini, mapepo huwa kinafunguliwa na neno la Mungu ndiyo maana kati ya kitu cha kwanza Mkristo anachopaswa kupingana nacho ni ujinga wa kiroho, ni lazima usome neno na kulielewa kiundani na kuweza kulitumia 


Isaya 22:22 “Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka nitauweka begani mwake , yeye atafungua wala hakuna ambaye atakayefunga, naye atafunga wala hapana atakayefungua, hivyo kama Simba wa kabila la Yuda ana funguo hatuna budi kumuomba atupatie funguo ili tuweze kuzitumia kutatua changamoto zetu


Ni vema mpaka hatua hii uwe umeshakuwa na uelewa mkubwa wa neno kwamba Mungu hubariki na Mungu hulaani na hata kuuwa pia pale ambapo watu wanapomuasi na kwenda kinyume na neno lake, aliangamiza kwa moto na kwa maji dunia ya kwanza na ya pili, hii inaelezea vizuri kwa nini katika kila kusanyiko la Mungu wapo wanaobarikiwa na wanaolaaniwa


Ukienda Kanisani ukaiba unategemea nini kama siyo kulaaniwa, kitu kikubwa kuliko vyote tunapaswa kumuomba  Yesu Kristo mwenyewe atufungulie mlango wa imani katika maisha yetu, mambo mengi yanayotutesa katika maisha ni kwa sababu tuu imani yetu ni dhaifu


Tambua ya kwamba kila mlango ambao unamuomba atakufungulia, lakini unapaswa kuwa na msingi wa neno la Mungu wa kusimamia ili Mungu apate kulitimiza neno lake, sisi ni watu wa mataifa kumbuka Mungu ndiye aliyesema ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona, bisheni nanyi mtafunguliwa Mdo 14:27“……..amewafungulia mataifa mlango wa Imani” imani yetu inapoongezeka mambo mengi ambayo yanatusumbua huwa yanayeyuka yenyewe kumbuka ya kwamba nuru haichangamani na giza


Hivyo njia za kuweza kumuomba Mungu kufungua mlango ambao unatusumbua ni kuhakikisha ya kwamba tunakuwa na moyo wa Ibada, huu ndio unamfanya Yesu Kristo kutupatia ufunguo ambao unafungua kila jambo la maisha yetu, kumbuka Mungu huangalia tena mlango ambao umejifunga maishani mwetu na kuufungua tena hapo ndipo tunapoaanza kupokea baraka kutoka kwake


TUNAJUAJE KWAMBA MLANGO NI SAHIHI AU LAA?


Ni kupitia Roho Mtakatifu aliye ndani yetu, Yeye hutushuhudia na hutusemesha mara nyingi juu ya mambo mengi tatizo ni kwamba wengi huwa hawataki kumsikiliza, Paulo alikumbana na changamoto nyingi sana kwenye kuiendeza injili kwa mataifa kwa sababu wakati mwingine alikuwa anashindwa kumsikiliza Roho Mtakatifu, hata kufungwa kwake ni kutokana na kutomtii Roho Mtakatifu pale alipomuambia asiende....


Inaendelea......

Kumbuka hakuna kitakachofanya kazi kama usipomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi ya maisha yako leo, anayeleta mabadiliko halisi na ya kweli ni Yesu peke yake ndiyo maana leo anakuambia Hebr 3:15 "Leo kama mtaisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama wakati wa kuasi,

Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote


Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;


SALA YA TOBA


Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa


Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani


Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.


Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu 

Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana



Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa
whatsup nambari 0715113636

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana