Bwana Yesu asifiwe? Namshukuru Mungu kwa ajili ya muda huu ambao amenipatia na ambao amekupatia wewe kuweza kujifunza neno lake, tunaendelea na neno tulilolianza juma hili la malango ya kiroho na leo tunaangalia sehemu ya tatu ya somo hili
Ninaomba Roho Mtakatifu aliye mwalimu mwema akakufundishe muda huu kile ambacho amekusudia kukufundisha, na Mungu akupatie hekima ya kuweza kukifanyia kazi ili uweze kupata matunda yake katika Jina la Yesu Kristo, Amen
Tulipoishia jana...
Siku zote unapaswa kukumbuka kwamba Mungu ana mpango na wewe
Isaya 55:8 “ Mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema
BWANA, hivyo hata kama jaribu liwe gumu kiasi gani kama limetoka kwa Mungu
hakika una heri kwenye maisha yako, tena Mungu anasema kama vile mbingu zilivyo
mbali na nchi ndivyo jinsi njia zake zilivyo tofauti na njia zetu, hivyo
muamini Mungu na amini neno lake pia
Endelea..
Mara zote Mungu anapofungua mlango wa majaribu kwetu huwa ameshajithibitishia kwamba una uwezo wa kuupita, lakini pia huwa ni
kwa nia ya kukuimarisha katika imani mara nyingi imani za watu hujengeka zaidi
wanapopita majaribu, huwa pia ni kwa kusudi la kukuimarisha na kukufanya uzidi
kumtegemea Mungu pekee ndiyo maana akasema...,
1Kor 10:13"Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini changanya na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili
Hivyo Mungu anapofungua mlango wa majaribu au changamoto
kwako huwa ni kwa nia ya kuangalia kama bado utaendelea kumtegemea hata kama
una matatizo, kitu pekee kitakachokusaidia kutokukata tamaa au kumkufuru Mungu ni ule upendo ambao utakuwa umeujenga kwa Mungu na siyo imani kumbuka imani ina kipimo lakini upendo hauna, upendo hufufua imani iliyokufa
Kama hukusoma neno la Mungu la jana la Milango ya kiroho sehemu ya pili⇒⇒⇒ UNAWEZA KUGUSA HAPA KUISOMA
Sisi sote tupo uchi mbele za Mungu na anayajua matendo yetu
yote hivyo anafahamu wapi ambapo tunapoanzia na tutakapoishia ndio maana hata
akiruhusu mlango wa majaribu huwa hayazidi kiwango chetu cha kuyakabili maana
anafahamu kabisa tuna nguvu kidogo sana ndio maana …
Ufunuo 3: 8 “Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango
uliofunguliwa mbele yako, ambao hakuna awezae kuufunga kwa kuwa unazo nguvu
kidogo….” Sisi ni mali ya Mungu anajua ukuu na udhaifu wetu, na Mungu anapoamua
kuufungua mlango kwa ajili yako hakuna mamlaka yoyote ile inayoweza kuufunga
Hakuna mtu yeyote
au mamlaka yoyote ambayo inaweza kumpinga mtumishi ambaye Mungu
amemfungulia mlango, hakuna jini au pepo au shetani wa aina yoyote anayeweza
kumlaani mtu aliyebarikiwa kwa kufunguliwa mlango wa mafanikio kutoka mbinguni,
hata wangekaa wakuu wote wa anga duniani bado hawawezi kumshinda mtu
aliyefunguliwa na Mungu baraka kwenye maisha yake
Ni lazima tuombe kwa bidii ili kufungua milango yetu, kabla
ya kuhubiri huwa tunaomba lengo siyo tuu kumkaribisha Roho Mtakatifu lakini pia
kufungua mlango wa ujumbe wa Mungu ambao utahubiriwa uweze kukubalika na kila
mtu aweze kupata neno moja tuu la kubadili maisha yeke Wakolosai 4:3 Mkituombea
na sisi pia kwamba Mungu atafungulie mlango kwa lile neno lake tuinene siri ya
Kristo ambayo kwa ajili yake nimefungwa”
Hivyo neno la Mungu ni siri, Ufalme wa Mungu umejengwa katika siri za kiungu ni wale ambao wanaweza kuzitambua siri hizo ndiyo wanaofanikisha maisha yao hapa duniani, ndio maana tunapokwenda kwenye mahubiri siyo kila neno ni kwa ajili yetu, tunaomba neno moja tu kwa ajili yetu litakalobadilisha maisha yetu
Neno la Mungu linasema katika kitabu cha Zaburi 107:20 "Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao, ni mpaka Mungu alitume neno lake kupitia mtumishi wake ndipo matendo makuu yanaweza kudhihirika
Biblia inaposema mlango mwembamba ina maana mtu asiyekuwa na
mambo mengi kwenye maisha yake
Math 7:14 “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana,
na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kupitia mlango huo
Binadamu hakuumbwa ili afanye kila kitu, ndio maana Mungu
ana kusudi na kila mtu na moja ya jambo la msingi kuliko yote ambalo ni lazima
uhakikishe unalifahamu ni kujua ni kwa nini Mungu alikuumba, hii inakusaidia
usiende kwenye mlango mpana wa kutaka kufanya kila kitu mlango ambao hupeleka
watu upotevuni
Mungu anatufikiria mambo mema na ndiyo maana alituumba Yeremia 29:11 "Maana nayajua mawazo niyawaziayo ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye
Ni furaha sana mtu mmoja akifahamu kwa nini Mungu alimuumba
njia inakuwa nyembamba kwako tuu pale ambapo unalifahamu kusudi lako na
kulifanyia kazi kwa nguvu na maarifa yako yote, dunia ya sasa tuna wataalamu
wengi wa sifuri kwa sababu tuu hawajataka kutafuta kusudi la kuumbwa kwao na
wengine wanafikiri wameumbwa ili kufanya kila kitu matokeo yake wanaangukia
kwenye mlango mpana
Wengine wana kampuni za makaratasi, wanatembea nazo kwenye bahasha wanasema wanasambaza kila kitu, vifaa vya steshenari, vifaa vya ujenzi n.k huwezi kufanya kila kitu ndiyo maana hakuna mtaalamu wa kila kitu ni lazima uwe na kitu kimoja kinachofahamika unakifanya
Hii ni siri ambayo unapaswa kuifahamu mtu ambaye anafahamu
kusudi lake na akawa analifanyia kazi anaweza kukaa bila fedha maadamu moyo wake unakuwa umetulia na
unaangalia sehemu moja ole inakuwa kwa yule ambaye hajui cha kufanya na hela
hana ndio wizi huanzia hapa, kukata tama, hofu ambayo huletwa na Shetani na
kuonesha kwamba hakuna ambacho kashafanikisha n.k
Kumbuka hakuna kitakachofanya kazi kama usipomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi ya maisha yako leo, anayeleta mabadiliko halisi na ya kweli ni Yesu peke yake ndiyo maana leo anakuambia Hebr 3:15 "Leo kama mtaisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama wakati wa kuasi,
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana