KUBALI KUBALIKA- SEHEMU YA KUMI - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Tuesday, August 28, 2018

KUBALI KUBALIKA- SEHEMU YA KUMI


Ninatanguliza salamu zangu kwako kwa Jina lipitalo majina yote Jina la Yesu Kristo, ninatumaini unaendelea vyema na ninakulialika tena leo tuweze kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kwa ajili ya utukufu wa Mungu

Nikupongeze unayeendelea na mfungo kama unataka kujumuika nasi ⇒⇒BOFYA HAPA KUPATA MAELEKEZO yote ya mfungo, jana tulikuwa na somo maalumu la maana ya namba saba kiroho na ninaona katika takwimu lilikuwa na wasomaji wengi sana kama hukulisoma⇒⇒ BOFYA HAPA KUSOMA

Tulipoishia......
Biblia imeandikwa ili sisi tuweze kubadilika, ndiyo maana hakuna kitu ambacho hakipo kwenye Biblia, Mungu ameweka kila kitu ili ujifunze na uweze kupata maarifa, kama unataka hekima kuanzia sasa fanya kiapo cha kusoma neno la Mungu kila siku

Kuanzia jana tumeendeleza somo lenye kichwa cha habari kubali kubadilika ambapo tuliendelea sehemu ya tisa kama hukusoma somo la jana ⇒⇒ BOFYA HAPA KUSOMA

Tunaendelea...

Huwezi kuyakimbia mabadiliko kwa sababu Mungu ndiye muasisi wa mabadiliko, tangia awali tumemuona akifanya mabadiliko, tizama uumbaji wa mbingu na nchi yote yale ni mabadiliko Mwanzo 1:1 "Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi

Baada ya anguko la Adamu wa kwanza bado Mungu anakuhitaji ubadilike ili uweze kuwa mwana wake tena, ndiyo maana alimtuma Adamu wa pili kuja kuhubiri Injili akituambia tutubu kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia Mathayo 4:17 "Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia

Hatuwezi kwenda mbinguni kama tusipotubu dhambi na kutubu dhambi ni kukubali kubadilika na kuiendea njia mpya na kuachana na njia ya zamani, tunahitajika kubadilika kwa sababu Shetani alivuruga mpango wa awali wa Mungu kwa wanadamu baada ya kumdanganya Eva akala tunda alilokatazwa na Mungu kula

Kubadilika ni suala la roho, akili na moyo zaidi kuliko mwili, tambua ya kwamba siyo mwili unabadilika bali ni roho, akili na moyo hivi vikishabadilika mwili lazima ukubaliane navyo, kwa sababu ni mtu wa kidunia anayeendeshwa na mwili na mazingira, mtu wa mbinguni anaendeshwa na roho

Siku ambayo utaamka na kufikiri ya kwamba unamfahamu Mungu ndiyo itakuwa mwisho wa kubadilika kwako, watu wote wanaofikiri wanamfahamu Mungu hawafahamu hata nukta yake, Mungu ni wa ajabu sana na hachunguziki ndiyo maana maisha yanakuwa na maana kwa sababu hauwezi kumfahamu Mungu

Tunajifunza kuhusu Mungu na ukuu na uweza wake katika neno lake na mpaka tunakufa bado hatuwezi kummaliza Mtume Paulo alijitahidi sana kumchunguza Mungu lakini alikiri kutokumliza Wafilipi 3:10 "Ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake

Ni watu ambao wana kiu na shauku ya kutaka kumjua Mungu wao kila siku ndio wanaofanya matendo makuu na ya miujiza katika maisha, kama hutaki kujifunza zaidi juu ya Mungu kupitia neno lake utabakia kuwa wa kawaida, siri zake anazifunua kwa wale wenye kiu ya kutaka kumjua 

Kumhofu Mungu ndiyo mwanzo wa kuruhusu matendo makuu kutokea kwenye maisha yako, haiwezekani kabisa kuishi bila kubadilika na hakuna kitu kisichobadilika hata ukila chakula bado kinabadilika ili kiweze kutumika kwenye mwili 

Mungu ameyatengeneza mabadiliko na kufanya muda na vipindi mbalimbali vya maisha kuwa njia ya kuruhusu mabadiliko, Mhubiri 3:1 "Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu

Kinachozuia mabadiliko ni ufahamu, kwa sababu mabadiliko siku zote yatamhitaji mtu kusafiri kiufahamu kutoka sehemu aliyopo na kwenda mbele na kuchukua kilichopo na kukileta katika wakati uliopo na kuanza kukitumia kwa ajili ya manufaa ya kizazi chake

Mtu yeyote yule ambaye amejishibisha na maarifa na ufahamu wa kutosha juu ya badiliko analotaka kuliendea kwenye maisha yake hana shaka na kulifikia, unaogopa kusogea kwa sababu hujajiandaa vya kutosha, jishibishe na ufahamu itakuwa rahisi kubadilika

Mabadiliko siyo kwa ajili ya watoto, mabadiliko ni kwa ajili ya watu wazima wasiokimbia majukumu, wanaotambua mambo hayatokei yanyewe bali husababishwa kutokea, mtoto anakunywa maziwa siyo chakula 1Kor 3:2 "Niliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza

Mabadiliko kwa watoto inamaanisha mwili yaani kurefuka, kunenepa, kupungua na mambo yanayofanana na haya, mbadiliko kwa mtu mzima ni kuukubali ukweli na kuvaa majukumu ili kuweza kuwa huru Yohana 8:32 "Tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru, kweli ndiyo inaleta mabadiliko

Mabadiliko ni mbegu yanapandwa katika akili, yanakuwa na kuleta ufahamu na maarifa baada ya muda huonekana katika matendo, kisha matokeo hudhihirisha mabadiliko, kitu cha kwanza kabisa kudhihirisha mtu kabadilika ni matendo yake

Itaendelea kesho...

Kumbuka hakuna kitakachofanya kazi kama usipomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi ya maisha yako leo, anayeleta mabadiliko halisi na ya kweli ni Yesu peke yake ndiyo maana leo anakuambia Hebr 3:15 "Leo kama mtaisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama wakati wa kuasi,

Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote


Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;



SALA YA TOBA

Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa


Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani


Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.


Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu 


Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana



Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa
whatsup nambari 0715113636

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana