KUBALI KUBADILIKA- SEHEMU YA TISA - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Monday, August 27, 2018

KUBALI KUBADILIKA- SEHEMU YA TISA

Co- Founders at MT Sialove & Pendo

Ninakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, sina shaka moyoni mwangu kwamba wewe ni mzima wa afya na unaendelea vyema, leo tena ni siku njema ambayo Mungu ameifanya kwa ajili ya kila anayemwamini ni siku yenye furaha na baraka tele.


Nikupongeze unayeendelea na mfungo kama unataka kujumuika nasi ⇒⇒BOFYA HAPA KUPATA MAELEKEZO yote ya mfungo, jana tulikuwa na somo maalumu la maana ya namba saba kiroho na ninaona katika takwimu lilikuwa na wasomaji wengi sana kama hukulisoma⇒⇒ BOFYA HAPA KUSOMA



Tulipoishia...


Roho za udini ndizo zilifanya Yesu kusulubishwa na kuuwawa, ni vyema ukafahamu kwamba dini haitupeleki mbinguni, ila siku ambayo utagundua siri hii kubwa ya Yesu kuja duniani na kuiishi Injili utakuwa na uhakika wa kwenda mbinguni pamoja naye


Kama majuma mawili yaliyopita tulikuwa tunajifunza kwa pamoja somo lenye kichwa cha habari Kubali kubadilika, nilikatiza somo lile na nikasema nitakuja kuendelea mbeleni, leo nimepata kibali cha kuliendeleza, kama hukusoma sehemu ya nane ya kubali kubadilika ⇒⇒bofya hapa kusoma


Tunaendelea...


Mara ya mwisho tuliona siyo dini inayompeleka mtu mbinguni, dini ni utaratibu maalumu uliowekwa na watu wa kumwabudu Mungu ndiyo maana unatofautiana kutoka thehebu moja hadi dhehebu jingine, lakini utaratibu huu siyo sifa ya kukupeleka mbinguni


Watu kwa kutokufahamu wamekuwa wanawatenga, wengine wanawauwa kabisa ndugu zao wanapobadilika kutoka dhehebu moja kwenda jingine, wanafikiri kwamba pale walipo ni sahihi na hawapaswi kujifunza zaidi


Nenda kasome tena habari za kifo cha Yesu, vifo vya mitume kisha uangalie kama watu waliowauwa siyo watu wa dini, ukiwa unafikiri dini yako ni sahihi zaidi ya wengine utakuwa unakosea na ndiyo maana utaanza kuwachukia wengine


Katiba yetu ni neno la Mungu kle ambacho Biblia inakisema ndiyo sahihi, dini zimejawa na demokrasia zaidi ndiyo maana wanapiga kura hata kwa mambo ambayo majibu yapo moja kwa moja kwenye Biblia


Unapoona watu wa dini wanapiga kura juu ya ndoa za jinsia moja na kushindwa kuona nini ambacho Biblia inasema juu ya jambo hili jua kabisa dini zimegeuka demokrasia, Mungu siyo wa demokrasia, Mungu ni mfalme neno na Mungu ni katiba hakuna wa kulibadilisha


Kama upo kwenye dhehebu ambalo mwisho wake halikupeleki kwa Yesu kama njia ya uzima ya kumfikia Baba jua umepotea, sababu hakuna njia ya kufika kwa Baba isipokuwa ya Yesu Kristo Yoh 4:6 "Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi


Tupo kwenye nyakati za mwisho wa dunia, kunazuka kila aina ya madhehebu ya ajabu na pia manabii wengi wa uwongo wamejitokeza, nyakati hizi zilitabiriwa katika Biblia Mathayo 7:15 "Jihadharini na manabii wa uwongo, watu wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali


Wengi wanafikiri manabii hawa watakuja wakimpinga Yesu, hapana! wanatumia Jina lake kufanya miujiza mingi ndio maana Mathayo 7:22-23 "Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitakapowaambia dhahiri sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu


Manabii hawa hawadanganyi wale tuu ambao hawajaokoka bali hata wale ambao wameokoka Mathayo 24:24 "Kwa maana watatokea Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao wanatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, ikiwezekana, hata walio wateule


Mungu anatuasa kwamba haya ambayo wanayasema tunapaswa kutoyasikiliza wala kuyatilia maanani kwa sababu yanapotosha, Jer 23:16 "BWANA wa majeshiasema hivi, msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka kutoka katika kinywa cha BWANA


Kwa nini leo nimeongelea dini na manabii wa uongo?


Nimetambua kitu kimoja kikubwa sana, Wakristo wengi ni wavivu kusoma, kama hutaki kujifunza neno la Mungu kuna vitu vingi sana utadanganywa, hebu jiulize ni mara ngapi unasoma Biblia? Ni mara ngapi unanunua vitabu vya kiroho na kujifunza?

Sehemu ya kwanza kabisa ya kuanza kubadilika katika kipindi hiki ni kuanza kusoma neno la Mungu peke yako, siyo mpaka Mchungaji au Mwalimu aje kukufundisha ndiyo maana watu wengi wanafundishwa vitu ambavyo havipo kabisa kwenye Biblia na hawafahamu kwa sababu hawataki kujifunza


Mtu atakayepona katika kipindi hiki ni yule ambaye anatenga muda wake binafsi wa kujifunza neno la Mungu na kumuomba Roho Mtakatifu amfafanulie pale anaposhindwa kulielewa, ninamsikitikia sana mtu ambaye hataki kujifunza na hawa ndio wanaokimbilia zaidi miujiza wakifikiri miujiza ndiyo kithibitisho nambari moja cha Yesu


Ukiwa mdadisi wa kutosha hutaona miujiza ni kitu ch ajabu, kwa sababu wewe mwenyewe ni muujiza tosha unaweza kufanya muujiza unaotaka pasipo hata ya nabii au mtume au mtumishi yeyote yule, unachopaswa kufanya ni kusoma neno vya kutosha 


Ukishiba neno utashangaa imani yako inabadilika, baada ya hapo muujiza unakuwa jambo la kawaida maishani mwako, chunguza utaona watu ambao wanakimbilia miujiza ni wale ambao hawataki kujifunza neno la Mungu


Mungu anashangaa mtu ambaye hataki maarifa, laiti ungejua nguvu ambayo Mungu ameiweka ndani yako usingekaa uangaike kwenda kwa waganga, au wachawi au kutabiriwa uwongo tenga muda wa kujifungia mwenye soma tena neno utaona ninachokuambia


Hosea 4:6 "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, Mungu anasema maneno hayo, kuangamizwa inamaanisha kuna kitu kinachofanya maangamizi, na tambua kwamba Mungu amekupatia neno lake kama hutaki kusoma na kujifunza lazma utaangamia kwa sababu Shetani atatumia fursa hiyo kukuharibu


Biblia imeandikwa ili sisi tuweze kubadilika, ndiyo maana hakuna kitu ambacho hakipo kwenye Biblia, Mungu ameweka kila kitu ili ujifunze na uweze kupata maarifa, kama unataka hekima kuanzia sasa fanya kiapo cha kusoma neno la Mungu kila siku


Itaendelea.....


Kumbuka hakuna kitakachofanya kazi kama usipomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi ya maisha yako leo, anayeleta mabadiliko halisi na ya kweli ni Yesu peke yake ndiyo maana leo anakuambia Hebr 3:15 "Leo kama mtaisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama wakati wa kuasi,

Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote


Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;



SALA YA TOBA

Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa


Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani


Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.


Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu 


Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana



Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa
whatsup nambari 0715113636



Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote":

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana