CO-Founder at MT, Sialove Lukumay |
Ninakusalimu katika Jina lenye uweza la Yesu Kristo, sina shaka moyoni mwangu kwamba wewe ni mzima wa afya na unaendelea vizuri na shughuli zako, baada ya mapumziko ya wiki leo tena ni siku njema ya ambayo Mungu ameiandaa kwa ajili yetu ili tumtumikie na kumtukuza
Tumekuwa na kichwa cha somo malango ya kiroho ambacho tumeenda nacho kwa muda wa takribani majuma mawili sasa na bado ninashhudiwa ndani ya moyo wangu kuendelea na somo hili japo kidogo kwa sababu ni somo refu sana na ninamuomba Mungu anipatie hekima ya kiungu ya kulifupisha ili tuweze kuanza somo jingine
Tulipoishia.....
Ukaribu wetu na Mungu ni kama mtu na mboni ya jicho lake, tunaanza kuzishika amri zake kama mboni ya jicho letu Mithali 7:2 “Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako, kisha tunamuomba atulinde kama mboni ya jicho lake Zaburi 17:8 “Unilinde kama mboni ya jicho na Mungu anatujibu mwenyewe Zakaria 2:8 ….Maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake
Juma lililopita tulianza kipengele cha njia ambazo Shetani anatumia kuvamia malango yetu ya kiroho na tulitizama njia ya kwanza ni kumwingiza mtu katika vishawishi na ya pili ni kugandamizwa, katika njia hii ya pili nayo imegaanyika katika vipengele tofauti ambavyo
kama tukichambua kimoja kimoja itatuchukua tena zaidi ya majuma mawili
Nataka ufahamu kwamba Mungu tunayemtumikia ni mwema na mwaminifu sana, anamtumia Roho Mtakatifu kutufundisha na kutuonesha mafunzo mbalimbali maalumu kwa ajili yako na yetu, hivyo kila funzo ambalo linafundishwa hapa lina pumzi ya Mungu
Ninamshukuru sana Mungu kwa ajili ya shuhuda za watu waliopona kwa kusoma neno la Mungu katika mtandao huu, wale ambao wametuambia binafsi na hata kama haujasema pia ninamtukuza Mungu kwa ajili yako kwa sababu shuhuda ni nyigi na zinadhihirisha matendo makuu ya Mungu
1Kor 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Kama haukusoma neno la Mungu lililopita la malango ya kitoho sehemu ya tisa ⇒⇒GUSA HAPA UWEZE KUSOMA
Endelea......
Kugandamizwa kunafanya nira kuwa ngumu na mzigo kuwa mzito hii ni kwa sababu roho chafu humvaa mtu na kuishi katika mwili wake na hali hii humfanya mtu kuwa mtumwa wa mwili wake ndiyo maana Yesu Kristo akasema maneno haya;
Mathayo11:28-30 "Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha, Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu, Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi
Kugandamizwa kunamuondoa mtu katika hamu ya kufanyia kazi mipango yake, kunamfanya mtu kushindwa kujisamehe mwenyewe na kusamehe pale ambapo anapokosewa, kunamfanya mtu kuhangaika katika maisha na kuwaondoa kabisa watu ambao Mungu aliwaandaa kwa ajili yake na pia kugandamiza kunaingiza roho ya woga ndani ya mtu
Nikiongelea kugandamizwa usifunge akili yako naomba Roho mtakatifu akufunulie zaidi ninamaanisha kugandamizwa ambako unawezaukakushuhudia kimwili, kunaweza kuwa kisaikolojia, kunaweza kuwa kiuchumi, kunaweza kuwa kielimu lakini zaidi sana katika ulimwengu wako wa kiroho kwa sababu ili kuweza kuona vitu katika ulimwengu wa nyama lazima yaanzie ulimwengu wa kiroho
Kugandamizwa ni umateka wa kiroho ambao mtu ili aweze kufanikisha mambo yake ni lazima amtegemee adui na hili ni chimbuko kubwa la ugumu katika maisha, kuchanganyikiwa na mahangaiko yasiyokuwa na kikomo, lakini mpaka uwe chini ya utawala wa adui ni lazima kuna mambo umefanya au yalifanywa ukifahamu au ukiwa haufahamu
Nina matumaini unaendelea kutengeneza hasira ya kiungu kwa ajili ya kugandamizwa ili tutakapoanza maombi haya maalumu uweze kuondoka katika hila za mwovu kirahisi, ninapenda ufahamu kwamba kuna mambo kwenye maisha yako hayawezi kuondoka kama hujachochea hasira ya kiroho kuyaondoa
Mara nyingi watu wanateseka katika vifungo mablimbali kwa sababu ya kukubaliana na kile ambacho adui amekipanda katika maisha yao, pando lolote ambalo halitokani na Mungu ni lazima likatwe na kuangamizwa kabisa ili kuweza kuufurahia utukufu ambao Mungu ameandaa kwa ajili yako mbeleni
Luka 3:9 "Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa kwenye mashina ya mti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni
Kwa sababu njia hii ya kugandamiza ni moja kati ya njia maarufu anazozitumia Shetani kutesa na kuharibu hatma za wana wa Mungu ninaomba nitumie fursa hii kukutajia njia zilizo ndani ya kugandamiza/ kugandamizwa na tusizichambue sana ili kufupisha somo hili;
i/Kugandamizwa kindoa kunakuwa na vitu kama hivi; umeoa au umeolewa hakuna amani katika nyumba, hakuna mafanikio wala matumaini, mume au mke anashinda bar kunywa pombe na kutembea na watu wengine, watoto wanarudi nyuma kimasomo na kuumwa pasipo sababu za msingi, hakuna mpango unaopanga na menza wako juu ya mafanikio ukafanyika, kila mkipanga mpnago wa biashara au maendeleo fulani kunatokea tatizo linawagharimu kutumia fedha zote mlizohifadhi
ii/Kugandamizwa kindoto kunakuwa namna hii; unaota ndoto za kutisha zinazokufanya uogope kulala, umepoteza kabisa hamu ya kuwa karibu na Mungu, unalishwa vyakula usiku wa manane au unajiona unapita sehemu usizozielewa, unakimbizwa na watu usiowafahamu, unatokewa na mizimu na watu wa kale, hauoni maono wala hauoti ndoto inayohusu hatma yako, n.k
iii/Kugandamizwa kiuchumi kunakuwa namna hii; kila ukikaribia kuanzisha mradi au kupata kazi kunatokea changamoto; kila ukiongea na mtu juu ya jambo linalohusu fedha mnatofautiana mwishoni; unashindwa kabisa kuhifadhi hela kama akiba yako; unapatwa na sababu zisizo na maana za kutumia fedha; ukikopesha watu hawakulipi; ukianzisha biashara inakufa baada ya muda; unakata tamaa hatua za mwisho haswa masuala ya uwekezaji n.k
iv/Kugandamizwa kihisia kunakuwa namna hii; unanuna na kukasirika bila sababu; unashindwa kusamehe mambo madogo; unatafuta sababu za kugombana na watu; unadharau wengine na kuona wewe ni bora zaidi; unakosa furaha na haujui sababu; unahisi tuu ndani yako kuna vitu haviko sahihi hata kama vinaonekana sahihi; hujisikii kuambatana na wenzako nk
v/Kugandamizwa kimwili kunakuwa namna hii; unahisi kuna vitu haviko sawa ndani ya mwili wako; unapatwa na maumivu yasiyo na sababu; unakosa kuona japo ni mdogo kiumri; unaumwa hovyo bila sababu; unakosa afya na kudhoofika hata kama una fedha; unatupiwa magonjwa na vimbe katika mwili wako; unakuwa rafiki na hospitali; unazeeka kabla ya wakati wako; unapenda kuambatana na watu ambao hamuendani kiumri pasipo sababu za maana; unajihusisha na moja au zaidi ya matendo ya kimwili kama yalivyoelezwa wagalatia 5:16-21 (soma tafadhali)
Tutaendelea tena na somo hili kesho......
Kumbuka hakuna kitakachofanya kazi kama usipomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi ya maisha yako leo, anayeleta mabadiliko halisi na ya kweli ni Yesu peke yake ndiyo maana leo anakuambia Hebr 3:15 "Leo kama mtaisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama wakati wa kuasi,
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
Baba/kaka / mama/ dada/ Yesu Kristo anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari/ Whatsup 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana