CEO of MT Sialove Lukumay |
Time is money ( Muda ni fedha) Time is precious (Muda ni kitu cha thamani), Mungu ametupa vitu vingi sana bure na ambavyo kimsingi ndio vya thamani na pindi unapovipoteza vitu hivi vya bure uwezekano wa kuvipata tena haupo au itakuchukua nguvu nyingi sana kuvipata na kuweza tena kuvitumia ipasavyo
Moja ya vitu hivyo ni marafiki, idea/wazo, akili zetu, viungo vya miili yetu na hata muda leo hii ukipoteza masaa mawili kwenye maisha yako kufanya mambo ambayo hayakupelekei kufikia malengo yako jua kabisa hakuna namna yoyote ile utakayoweza kurudisha muda huo maishani mwako
Kama haukusoma makala ya jana ya tengeneza muda wa kitu unaweza ⇉⇉⇉KUBOFYA HAPA KUISOMA YOTE
Mambo yote ambayo tunayafanya hapa duniani yatapita baada ya muda fulani na ndio maana kuna kufa, muda ambao Mungu ametupatia ni kwa kusudi la kutenda mapenzi yake ili tuweze kuurithi uzima wa milele 1Yoh 2:16 "Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.
Mambo mengi tunayohitaji katika dunia hii ni ya kimwili na mwili umeumbwa kwa ajili ya tamaa, ndio maana binadamu hawezi kutoshekwa na mali au utajiri au chochote kile kama hatakuwa na hofu ya Mungu ndani yake
Kwa sababu asili ya Mungu ni ya umilele yaani hana kikomo cha muda hatuna budi kuukomboa wakati wetu kwa kuhakikisha tunapokuwa hapa duniani tunamtumikia Mungu katika roho na kweli ili tujihakikishie uzima wa milele
Mungu ana wakati ambao ameutengeneza kwa ajili ya kila mtu, wakati huo ndio unaomwezesha mtu kufanikisha kusudi ambalo Mungu amekusudia kwa kila mtu, wokuvu unatupeleka katika wakati ambao Mungu ameuandaa kwa ajili yetu 2Kor 6:2 "Kwa maana asema kwa wakati uliokubalika nalikusikia, na katika siku ya wokovu nalikusaidia; tazama wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ndio sasa.
Tunapomtumikia Mungu sasa tunajitengenezea nafasi nzuri zaidi katika ufalme wake, Wakristo ndio wanaochelewesha ufalme wa Mungu kuja kwa sababu hawataki kuvuna nafsi na kuhakikisha watu wanamfahamu Kristo, neno la Mungu linasema Yesu hatarudi mpaka Injili ihubiriwe kote
Mathayo 24:14 "Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Wakati haujawahi kurudi nyuma, wenyewe unachanja mbuga mbele kwa mbele hivyo tuna jukumu la kutumia muda wetu vyema ili tuweze kutimiza mapenzi ya Mungu na yetu pia kwa ajili ya utukufu wake, mafanikio yetu ni sifa kwa Mungu wetu, Mungu hapendi kuona mtu yeyote anaangamia katika uovu na ndiyo maana katika 1Pet 5:7b ........anasema Yeye Mungu hujishughulisha sana na mambo yetu
Tunaukomboa wakati sasa kwa sababu kuna nyakati zinazokuja ambazo hatutaweza tena kumtumikia Mungu, tungali vijana na tuna nguvu tunayo nafasi nzuri zaidi ya kumtumikia Mungu katika roho na kweli, tunao wakati wa kuvuna nafsi nyingi na kuzileta kwa Kristo
Yoh 9:4 "Imenipasa kuzifanya kazi zake Yeye aliyenituma maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi
Wapo wengi ambao wanatufuatilia katika maisha yetu, wamenuia mabaya na hawataki kabisa tufanikiwe katika suala lolote lile, tunapojishughulisha na mambo ya Mungu tunamlazimisha ajishughulishe na mambo yetu kwa sababu hata nyakati zetu zipo katika mikono yake mwenyewe Zab 31:15
Tunapojishughulisha sana na mambo ya Mungu, hutufundisha namna ya kuzihesabu siku zetu na tunaweza kufahamu kwamba sisi ni binadamu ambao tunapita katika dunia hii na Mungu ni wa milele, hivyo tunajazwa na moyo wa hekima Zab 90:12
Binadamu kwa sababu ya mwili ana chembechembe za uvivu, yaani uvivu upo tuu ndani yake na huwezi sema unatokea wapi lakini kuna muda mtu hujisikia uvivu ( hii ni asili)
Mungu alilijua hili ndio maana akasema asiyefanya kazi na asile, saa zingine huwa nasema kungekuwa hakuna kula watu wasingekaa wafanye kazi
Na uvivu ndio unaosababisha watu kuairisha mambo na kusema ntafanya kesho au baadae au subiri kidogo wakati kuna uwezekano wa kufanya jambo hilo muda huo husika
Mithali 27:1 usijisifu kwa ajili ya kesho kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja, kuna haja ya kujifunza namna ya kujipa hamasa pindi ambapo unapopatwa na uvivu ili uweze tena kufanya kazi zako kwa bidii
Tunapaswa kuishi zaidi katika ulimwengu wa sasa hivi (yaani sasa) kuliko ulimwengu ujao, hakuna mtu anaejua ni nini kitamtokea saa moja mbeleni, hivyo ni sahihi kutenda mambo yetu kwa wakati na kujituma zaidi
Huu ndio wakati wa kwenda kuanza kufanyia kazi ndoto yako uliyoiairisha mwaka jana, fanya tuu hata kama ni kidogo jambo la msingi ni kuhakikisha unaanza kufanya
Usidharau mchango mdogo unaoufanya kwenye ndoto yako leo sababu kidogo kidogo hujaza kibaba, siku zote kumbuka mambo makubwa yalianzia kwenye mambo madogo. Hakuna kubwa lolote linaloanzia kwenye ukubwa.
Kuanza kidogo ( To start small is always beautiful ) sababu utajifunza mambo mengi, utajifunza uvumilivyo, ukifanya makosa kuna uwezekano mkubwa wa kuyarekebisha na kuanza tena n.k
Ni siku ya leo inatupa habari ya kuongea kesho, kesho yako utaongea nini kama hutatumia vyema siku ya leo? Tumia siku ya leo vyema ili uwe na la kusema kesho
Kumbuka Neno hili la uzima wa milele haliwezi kufanya kazi kwako kama hujampokea Bwana Yesu na kumfanya awe mwokozi wa maisha yako kama hujafanya hivyo tafadhali kwa moyo wa imani sema maneno haya;
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa, lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani, ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana