Gospel Singer and MT member ANGEL BERNAD |
Kama unataka kukua katika eneo lolote lile liwe ni la afya, kifedha,kiimani,kimahusiano, kibiashara unachopaswa kufanya ni kuacha kabisa tabia ulizo nazo sasa, tabia na mazoea uliyojitengenezea ndiyo yamekufikisha hapo ulipo, ukitaka kwenda mbali zaidi ya hapo ni lazima kubadili tabia na mazoea uliyonayo sasa
Wakati mwingine kuacha njia za zamani huwa ni kitu kugumu zaidi kufanya na hii ni sababu huwa tunahofia vitu vilivyo mbeleni, ni hofu ya kushindwa inayosababisha watu wengi wasianzishe biashara zao, ni hofu ya kuona nitaonekanaje inayowafanya watu wasiokoke na kumtumikia Mungu
Kuna kitu kimoja tu cha uhakika kwa mwanadamu yeyote ambacho ni kubadilika, kama ulizaliwa ukiwa kichanga, umekua, umeoa, una watoto ni uthibitisho kwamba mabadiliko yanatokea katika maisha yako na hayatakaa yaache kutokea
Kama haukusoma makala ya jana ya kubali kubadilika sehemu ya kwanza⇉⇉⇉ BOFYA HAPA KUISOMA YOTE
Mungu pekee ndiye habadiliki ndiyo maana anasema Heb 13:8 "Yesu Kristo ndiye yeye yule, na leo na hata milele, maadamu upo katika mwili ni lazima utabadilika baada ya muda ndiyo maana ni muhimu kuwa sehemu ya mabadiliko tunayotaka
Hatutafuti mabadiliko nje yetu bali ndani yetu 1Yoh 4:13 "Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake, ndiyo maana Mungu hazungumzi na makundi ya watu bali huzungumza na mtu
Mungu hugusa mioyo yetu kupitia roho wake aliye ndani yetu, hugusa mioyo ya mtu mmoja mmoja, Mungu huchagua mtu mmoja kuongoza kundi la watu, siyo makundi ya watu yanaongoza bali ni mtu mmoja
Kila jibu la swali linalotutatiza liko ndani yetu wenyewe kama tukimruhusu Mungu azungumze nasi kupitia Roho wake, hivyo mabadiliko ni mguso ni kitu kinachotokea ndani kupitia uweza wa Roho Mtakatifu
Tunapoiandaa mioyo yetu kwa ajili ya neno inakuwa rahisi kukutana na mguso wa Mungu inakuwa ni rahisi kuona uthihirisho wa nguvu za Mungu maishani kwetu na kuweza kulisifu na kulitukuza jina lake
Kubadilika ni kuwa tayari kumsikiliza Mungu, ni kuwa tayari kulifuata neno lake, ni kuwa tayari kusimama katika kusudi la Mungu, binadamu ni vigeugeu ndiyo maana hatuna budi kumsikiliza Mungu na kulishika neno lake kila wakati Malaki 3:7 "Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika
Kubadilika kuna maana tuu pale unapobadilikia upande wa Mungu na kutenda maagizo ya Mungu, siyo kila badiliko ni jema, mabadiliko mengine hutokana na Shetani
Kuacha mazoea na tabia za awali ndio njia ya kufungua njia mpya na kukupeleka sehemu nyingine na pia kufungua milango mingine kwa ajili yetu, ni vitu ambavyo huvifahamu ndio vina uwezo wa kukufungulia utele na kukupatia vitu vya thamani maishani mwako
Na hiki ni moja ya kitu rahisi na chepesi sana lakini wengi wetu hatudhubutu kufanya kwa sababu tunaridhika na hali tulizonazo na pia tunakuwa na hofu ya tunakoendea, hali hii imetuzuia kuwa na mafanikio zaidi lakini mwisho wa siku ni nani wa kumlaumu katika kila kitu maishani mwangu? Ni mimi peke yangu!!!
Nimejua mtu wa kwanza kabisa ninaepaswa kumteka ni mimi Plato akasema "For a man to concquer himself is the first and nobest of all victories"
Ili mambo yabadilike ni lazima nibadilike, mabadiliko yanaanza na mimi na hiki ndicho ninakiita majukumu, ni pale ambapo unakubali kwamba wewe unahusika na kila kitu kinachotokea katika maisha yako, ni pale unapokubali kwamba ni lazima utumie nguvu ulizopewa na Mungu kumwondoa Shetani maishani mwako
Luka 10:19 Tazama nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru
Uwezo wa kubadilika na kukubali kwamba ni jukumu langu kwa asilimia 100% kubadili maisha yangu, badala ya kulaumu, kuangalia sababu za nje, nachukua hatua na kuongeza bidii zaidi
Sasa tambua kwamba una ujuzi na unao uwezo ndani yako uliowekwa na Mungu na unaweza kujisaidia ukakua, ukabadilika na kupata maarifa mapya, hili linawezekana tuu pale unapokuwa na maarifa sahihi ndivyo ambavyo kazi yako itakuwa ya kipekee, biashara yako itakuwa, mshahara wako utabadilika.
Hakuna kinachoweza kubadilika maishani kama mimi nisipobadilika, na kubadilika ni kuzishika amri za Mungu na kuziishi, ni kuzishika sheria za Mungu kama mboni ya jicho lako Mith 7:2
Kumbuka hakuna kitakachofanya kazi kama usipomkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi ya maisha yako leo, anayeleta mabadiliko halisi na ya kweli ni Yesu peke yake ndiyo maana leo anakuambia Hebr 3:15 "Leo kama mtaisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama wakati wa kuasi,
Baba/kaka / mama/ dada/ Mungu anakuita tena leo anakuambia njoo uisikie sauti yangu nami nitakuponya na kukuondolea maangamizo yote
Kama amenibadilisha mimi na wengine wengi nina uhakika hata wewe anaweza kukubadilisha, haijalishi unapitia magumu gani muda huu lakini wakati wa uliokubalika ni sasa na ni kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, kama unakubaliana nami fuata sala hii fupi ya toba sema;
SALA YA TOBA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako mimi....................(taja jina lako) ninakiri kwamba nimekutenda dhambi na ninastahili kuhukumiwa
Lakini kwa sababu wewe ni Mungu mwenye rehema na neema naomba unisamehe, unioshe na kunisafisha kwa damu yako ya thamani uliyoimwaga pale msalabani
Ninaomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima, karibu Yesu ndani yangu ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Ahsante Yesu kwa kuniokoa Amen.
Hongera, kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, huu ni mwanzo mpya wa maisha yako ndani ya Kristo Yesu
Na kwa kuwa umetamka maneno hayo kwa imani wewe ni kiumbe kipya kumbuka unahitaji kujijenga kiroho zaidi tuna mafunzo maalumu kwa ajili yako wasiliana nasi kwa simu nambari 0715113636 ili tuendelee kukuombea na kukushirikisha neno zaidi, Mungu akubariki sana
Kama unatamani kuwa mmoja wa wanachama wa Mwanamke Thamani (MT) na kujiunga nasi kuomba, kujifunza neno la Mungu kwa pamoja kama familia moja tunakukaribisha sana waweza kuwasiliana nasi kwa whatsup nambari 0715113636
Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana