Tunaweza kuona thamani ya uhai pale tu magonjwa, dhiki, njaa, ajali, ukame vinapotokea katika mazingira ambayo tunaishi
Tunapaswa kuthamini na kujali kile ambacho Mungu ametupatia kwa utukufu wake bure, mara zote utajiri haupo mbali na pale tulipo ni kitendo cha kutumia karama na vipaji tulivyopatiwa bure na Mungu
Kama hukusoma makala iliyopita ya maswali muhimu manne ya kujiuliza na unaweza ⇒ Kugusa Hapa! Kutizama kipindi cha kwanza cha mwanamke Thamani ⇒ GUSA HAPA!
Kama hukusoma makala iliyopita ya maswali muhimu manne ya kujiuliza na unaweza ⇒ Kugusa Hapa! Kutizama kipindi cha kwanza cha mwanamke Thamani ⇒ GUSA HAPA!
Isaya 43:7 "Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya"
Leo hii huwezi kuona thamani ya kuwa na macho mawili ni mpaka utakapokosa jicho moja na kuwa chongo
Unajua kati ya shukrani maalumu ambayo unapaswa kumpa Mungu ni kumshukuru kwa kukufanya jinsi ulivyo kila siku, wewe ni wa ajabu na wa pekee sana
Hakuna anayefanana na wewe, umeumbwa kwa namna ya pekee na una ukuu na uwezo wa ajabu ndani yako, wewe ni kazi njema na ya kupendeza machoni kwa Mungu
Nuru inaonekana ni kitu chema pale giza tororo linapotanda kila mahali, ili kuthamini Nuru ni lazima giza liwepo, ni mpaka giza litande ndio nuru huthaminiwa Yohana 1:5 "Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza"
Japokuwa tuliumbwa katika giza lakini ndani ya Kristo Yesu tumefanywa watu wa nuruni Waefeso 5:8, na siku zote tunda la nuru ni wema wote na haki na kweli
Tunaweza kuona umuhimu wa matatizo na changamoto pale tunapoweza kuyatatua na kuyageuza mtaji au wazo la biashara kwetu
Hauthaminiki kwa sababu hujaweza kutatua matatizo na changamoto zinazoikabili jamii na watu ambao wanakuzunguka
Ukiona changamoto na matatizo yamekuandama sana basi jua kabisa una uwezekano mkubwa sana wa kufanikiwa kuliko ambaye kila kitu kwake ni mteremko
Pia tambua kwamba unapofuatwa sana na changamoto ni kwamba zimeamini unaweza kuzitatua hivyo zinapokuja ziambie utazishughulikia kisawasawa.
Leo tunaweza kujiona mahodari sana kwa kuangalia kiwango cha matatizo tulichotatua, hebu fikiri kama kila vita tunayoenda kupigana tungekuwa tunajua tunaishinda ingekuwaje?
Ule mshawasha wa litakalotokea, utakalolifanya na matokeo utakayoyapata ndio unakupa amsha amsha ya kuenda vitani
Endeleza mapambano wala usikate tamaa, hii dunia ipo bize sana kukusumbua na kutafuta wewe ni mtu wa aina gani, na nakuhakikishia wakati wa njaa, manung'uniko, shida, ndio kipindi kizuri cha watu wa Mungu kuchanua
Kuanzia leo usiongee kama wao, usifanye kama wao, usiende kama wao, ili usiwe kama wao inuka na uangaze!
Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana