Hakuna mtu aliyezaliwa bahati mbaya, inawezekana wazazi wako walikupata bahati mbaya ila kwa Mungu hukuzaliwa bahati mbaya alikujua kabla hujazaliwa
Kama hukutizama kipindi cha kwanza cha Mwanamke Thamani Gusa Hapa Kukitazama
Kama hukutizama kipindi cha kwanza cha Mwanamke Thamani Gusa Hapa Kukitazama
Jeremia 1:5 "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa nayo Wagalatia 1:15 "Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,
Hivyo Mungu anaijua kila mimba ambayo inatungwa haijalishi ilitungwa katika mazingira gani na Mungu huweka kusudi katika kila mtu kwa ajili ya utukufu wake, kiufupi mimba inapoanza kutungwa tuu pale pale Mungu hukuwekea kusudi
Unakumbuka kipindi Mariam mama yake Yesu alipomtembelea ndugu yake ambaye ni mama yake Yohana Mbatizaji walipoonana Yohana alianza kuruka na kucheza cheza ndani ya tumbo la mamaye Luka 1:41
Tukiwa katika mwanzo wa mwaka ndio kipindi kizuri sana cha kutengeneza picha halisi ya mambo unayoyataka miaka ijayo na mwaka huu, ni kipindi cha kutunga mimba ya ndoto na mipango ambayo tunataka kuifanikisha mwaka huu wa 2018
Lakini ni vigumu sana kupata kitu ambacho hujakipanga na hujui utakipata vipi, hivyo kupanga ni muhimu sana kuliko unavyodhani Biblia inasema Mithali 21:5 "Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji"
Ukichaa wa mwaka huu ni kuishi kama ulivyoishi mwaka uliopita halafu ukategemea kwamba utapata matokeo tofauti, ukweli ni kwamba ili mambo yabadilike ni lazima wewe ubadilike
Kubadilika inaweza kuwa ni kuanza kumtumikia Mungu, kuanza kufanya zaidi kazi, kusoma zaidi, kubadilisha aina ya marafiki ulionao hata hivyo Biblia imeonya juu ya marafiki wabaya wanaotupotosha
Nilivyokuwa Kanisani niliangalia namna ambavyo waimbaji walikuwa wakitumia vyombo mbalimbali vya mziki kama gitaa, ngoma, tarumbeta na kinanda ili kutengeneza muziki, lakini nikajifunza kitu kimoja japokuwa niliona vyombo vyote hivi ni tofauti ila vyote vinapopigwa kwa pamoja vinatengeneza muziki mzuri
Kadhalika na binadamu tunatofautiana sana kwa rangi, makabila, sura, kimo, utaifa , lakini wote ni binadamu na Mungu kaweka kwa kila binadamu kusudi fulani la kulifanya hapa duniani
Nataka nieleweke kwamba hakuna mtu aliyezaliwa bahati mbaya, au kwa ajali hata kama wazazi wako hawakupanga uje ila kwa Mungu kuna sababu kuu ya kuruhusu wewe kuwepo.
Natamani ujiulize maswali haya manne muhimu, kisha yajaze kwenye diary yako mwanzo huu wa mwaka na uyatendee kazi kama ulikuwa hujui unapaswa kufanya nini.
SWALI 1: Ikitokea umekufa sasa hivi na ukawa umesimama mbele ya Mungu, Je utataka Mungu akupongeze kwa suala gani au kitu gani ulichofanya?
Hii inaleta umuhimu wa maneno haya Zaburi 39:4 " BWANA, unijulishe mwisho wangu, Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani; Nijue jinsi nilivyo dhaifu.
SWALI 2: Kama ungekuwa unapaswa kufanya kitu kimoja tu katika maisha yako, kitu hicho kingekuwa kitu gani?
Moja ya tatizo kubwa la watu ni kwamba hawawezi kusimama na kitu kimoja wao wanafanya kila kitu alimradi wapate fedha basi hata ukiwaambia waue watauwa kama wanapata hela, ni lazima uwe na kitu kimoja cha kusimamia Yesu ilikuwa Injili wewe ni nini?
SWALI 3: Kama kungekuwa hakuna kizuizi cha aina yoyote, ungefanya nini kwenye maisha yako?
SWALI 4: Ni kitu gani kitakufanya ukumbane na changamoto kubwa zaidi yako?
Ukiwa mkweli na ukajijibu maswali hayo kwa usahihi tayari utakuwa umeshapata jibu kwamba unapaswa kufanya jambo gani katika maisha yako
Tunaishi mara moja tuu hapa duniani, usikubali kupoteza sana muda wako kufanya vitu usivyovipenda na kuishi maisha ya watu wengine, pangilia maisha unayoyataka wewe
Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana