Zipo nyakati katika maisha unaweza kupitia mambo magumu, unaangalia nyuma unaona giza totoro unaangalia mbele unaona giza inakuwa kama huoni unakoelekea
Haupaswi kuogopa maana Biblia inasema Isaya 41:10 "Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu"
Kama hukusoma makala iliyopita ya Tujifunze kushukuru tafadhali Gusa hapa
Kama hukusoma makala iliyopita ya Tujifunze kushukuru tafadhali Gusa hapa
Jambo jingine kubwa nililojifunza kipindi hiki ni kuhakikisha unaimarisha zaidi mahusiano yako na Mungu
Anasema katika 1Petro 5:6-7 "Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu
Haijalishi ni jambo gani unapitia wewe nyenyekea chini ya mkono wake sababu yeye ni hodari na yupo kwa ajili yako
Wakati ambao hujui ni nini cha kufanya wewe msifu Mungu, haijalishi ni jambo gani gumu unapitia hakikisha unamsifu Mungu, unapata muda wa kutosha kusoma neno lake na kuomba
Mungu anasema katika 1Mambo ya walawi 16:25 " Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote."
Katikati ya giza tororo watu wote wamelala Daniel, Meshaki na Abelnego wanaanza kumsifu Mungu na hawakuuwawa asubuhi iliyofuata
Unapomsifu Mungu tegemea Mungu kupigana kwa ajili yako, ukitaka kumuona Mungu akiwa kazini msifu na kumwabudu kutokea moyoni
Mungu anapenda kusifiwa na kupewa namba moja katika kila kitu tunachokifanya sababu ametuumba ili tumuabudu,tulisifu na kulitukuza jina lake
Siyo kila vita unapaswa kupigana wewe, vingine siyo saizi yako hivyo utapigwa tuu, unapaswa kumsifu Mungu na kumuomba aingie katikati ya vita vyako
Ninaposema Mungu kupigana kwa ajili yako usifikiri atashuka na kuchukua upanga au bunduki la hasha! Mungu atainua watu ambao watakuwa upande wako, Mungu atakupa Idea mpya za kutatua changamoto unazozipitia, Mungu atakuheshimisha mbele za watu
Unamkumbuka Mfalme Jehoshafati 2Mambo ya Walawi 20:19-- alishinda vita pasipo hata kupigana waaza kusoma habari yake zaidi ukiwa faragha na neno la Mungu
Sababu kubwa ya Mungu kupigana kwa ajili yetu ni kwamba maadui wetu ni wengi sana, vita havijaisha mpaka Mungu aingie katikati ya vita kwa ajili yako
Unapomruhusu Mungu kuingilia vita vyako anakuwa adui wa adui zako Kutoka 23:22 " Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao"
Pindi Mungu anavyopigana kwa ajili yako vita huisha anasema Kumb la Torati 20:4 "Kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi
"
Mungu anapoingilia vita vyako wewe unakuwa mtazamaji na siyo mpiganaji
Anakuinua kutoka utukufu mpaka utukufu na analifanya suala lako kuwa la tofauti
Siyo lazima upigane ndio ushinde, acha Mungu apigane kwa ajili yako jua kwamba siyo wapiganaji wote hupigana, wenye hekima pindi vita vinavyokuwa vigumu sana kwao humuacha Mungu kupigana kwa ajili yao
Kuna watu wanayaangalia matatizo wanayavaa mpaka wao wenyewe wanakuwa matatizo
Kumsifu na kumtukuza Mungu kunaondoa vizuizi vyote vya sisi kufikia mafanikio yetu
Jikabidhi kwa Mungu mwache aingilie kati vita vyako nawe utakuwa umevipiga vita vizuri na kuumaliza mwendo salama
NB: Maneno Vita / adui kama yalivyotumika yaweza kuwa ni matatizo, ugumu, changamoto ambazo tunazipitia katika maisha yetu
Kama bado hujasubscribe you tube chanel ya MWANAMKE THAMANI Gusa hapa Tafadhali kumbuka leo saa kumi na moja kamili jioni ndio tunaweka kipindi cha kwanza hivyo ili usipitwe hakikisha unasubscribe mapema
Mwanamke Thamani! "Wewe umewazidi wote"
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana