NGUVU YA MSAMAHA -II - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Monday, January 8, 2018

NGUVU YA MSAMAHA -II



Kusamehe  ni kuachilia kile ambacho kimekuwa moyoni mwako kwa muda fulani

Mathayo 6:14-15 "Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe  hata ninyi hatowasamehe

Kama hukusoma makala ya jana ya NGUVU YA MSAMAHA  sehemu ya kwanza  Gusa hapa!

Hivyo tunaona dhahiri hapa kwamba tunasamehe ili nasi tupate kusamehewa makosa yetu na Baba yetu wa mbinguni

Biblia imeweka wazi kwamba wote tuna dhambi ya asili, iliyofanywa na babu zetu 1Yohana1:8 "Tukisema hatuna dhambi tunajidanganya wenyewe wala kweli haimo mwetu

Lakini pia tunaona kwamba moja ya kusudi la kuja kwa Yesu Kristo ni ili tuweze kupata ukombozi na msamaha wa dhambi Wakolosai 1:13-14

Tunahimizwa kabla ya kuanza kuomba tunapaswa kuhakikisha kwamba tumesamehe wote waliotuudhi Marko 11:25 , ni kosa kusimama kusali kama haujasamehe

Mungu anaelewa kwamba binadamu tuna mapungufu mengi na anajua kabisa hatuwezi kuishi bila kukoseana ndio maana anasema tuwe na roho ya rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana na kusameheana wala mtu asiwe sababu ya kumlaumu mwenzake Wakolosai 3:13

Tunapaswa kusamehe mara ngapi?

Mathayo 18:22 "Sikuambii mara saba, bali hata saba mara sabini maana yake ni kila wakati tunapaswa kusameheana 


Ni nini kinatusaidia kusamehe?

Upendo ndio nguzo muhimu sana kwenye msamaha, Mungu alitupenda tangu awali ndio maana alimtuma mwanaye wa pekee Yesu Kristo ili kuja kutuokoa na dhambi

1Wakorintho13:4-6 "Upendo huvumilia, hufadhili, hauhusudu, hautakabari, haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya......."

Unapokuwa na upendo huwezi kushindwa kumsamehe mwenzio ambaye amekukosea katika suala fulani kwa sababu upendo hubeba yote na hii ndiyo amri kuu kupita amri zote

Mara nyingi sana watu wanashindwa kusamehe kwa sababu kila jambo linalotokea au kujaji walichofanyiwa Luka 6:37 "Msihukumu nanyi hamtahukumiwa, msilaumu nanyi hamtalaumiwa, achilieni nanyi mtaachiliwa"


Kusamehe siyo...!

  • Kuruhusu wengine wakuonee na kukunyima haki zako, wote tumeagizwa kuishi kwa upendo pale ambapo unanyimwa haki zako ni lazima kusimama kuzidai ndio maana yapo maombi ya kisasi na Mungu huyasikia

  • Kuvumilia uovu Isaya 5:20 "Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema na wema ni uovu, watiao giza badala ya nuru......" Mtu yeyote ambaye anageuza mambo unapaswa kumchukulia hatua , uovu ni lazima ukemewe siyo tuu kusema nimekusamehe

  • Kuigiza kwamba hauna dhambi, Matendo 26:20 ".........Wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao"Kama umeokolewa  matendo yako na yasawiri kile unachokisema hapo ndipo utapata msamaha wa kweli

  • Kuigiza kwamba hakuna tukio lolote lililotokea, mtu amekukosea mfuate moja kwa moja mwambie sijapenda ulivyofanya jambo fulani na umenikwaza lakini nimekusamehe, hivindivyo wanavyoishi watu wanaojithamini na kulijua neno la Mungu na mambo hubadilika ukishasamehe kama hukusoma makala ya mambo hubadilika Gusa hapa

Itaendelea......

Mwanamke Thamani!

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana