MAMBO HUBADILIKA - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Monday, January 8, 2018

MAMBO HUBADILIKA

Turn off for: Swahili


Kipindi cha nyuma watu walikuwa wakihubiri Injili nakuutukuza umasikini, ilikuwa kama vile ukiwa masikini ndio unaenda mbinguni

Hali hii iliwadumaza Wakristo wengi wakawa hawafanyi kazi sababu hawafundishwi hivyo na pia walikuwa wakiwaona matajiri kama vile wana dhambi au wakosaji

Lakini pia ilikuwa ikiwafundisha watu waikimbie dunia waende mbinguni, sala ya Baba yetu inasema "Ufalme wako uje mapenzi yako yatimizwe"

Hivyo Mungu na ufalme wake unapaswa kuja hapa duniani, siyo sisi tuufuate tunapaswa kuwa watakatifu ili kuona hili likitimia

Katika maisha unaweza kupitia kipindi kigumu sana, ukakata tamaa ukaona giza tuu au pengine kufikiri hata kujiuwa

Lakini unapokuwa katika hali hii unapaswa kutengeneza zaidi mahusiano yako na Mungu kwa sababu Mungu habadiliki

Ukiweka imani na tumaini lako kwa mwanadamu utaishia kuumia roho yako sababu hubadilika wakati wowote ule

Hii ndio maana unamsikia mwanasiasa leo anapondea jambo hili chama hiki kesho anahama na kuenda chama kile kile alichokuwa anakipondea

Ukiwa kama mkristo mwenye amri na mamlaka unapaswa kuwa na misingi na misimamo yako kwenye maisha

Ukitenda mambo mazuri hukulinda wapo watu ambao hawatakufa  mapema sababu ya kubeba hatma za wengine

Matendo mema humfanya hata Mungu kubadili mipango yake kwa wakati fulani, Hezekia alimkumbusha Mungu juu ya wema aliomfanyia

Mungu alibadili kifo chake ambacho alikuwa kashamtuma nabii akampe taarifa kikawa uhai wa kuongezewa miaka 15 zaidi

Tunapaswa kufahamu katika dunia hii siyo kila mtu atakupenda, hivyo usipoteze muda wako kutafuta kukubaliwa na wanadamu bali tafuta kutenda yaliyo mema

Hata ukiwa na shida jua siyo kila mtu atataka kukusaidia, wengine hufurahia kwamba umekumbwa na mabaya hivyo mkabidhi Bwana njia zako

Kumbuka hakuna jambo lolote lile ambalo Mungu anashindwa, kila kitu hubadilishwa  na Mungu, kushindwa hugeuka ushindi, kifo huwa uhai, kuumwa hugeuka afya nk

Mwanamke Thanini!

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana