Nimewahi kumsikia mtu anasema "Kwa kile alichonifanyia sidhani kama nitaweza kumsamehe, aongelee mengine lakini siyo kile..."
Hayo maneno yanaonesha moja kwa moja kwamba mtu huyu ana uchungu ndani yake na huenda kila linapotajwa jina la huyo aliyemtendea kitu hicho moyo wake huuzunika
Msamaha siyo kitu ambacho tunajifunza binadamu kwa binadamu bali tunakiona kutoka kwa mwenyezi Mungu mwenyewe
Waebrania 8:13 "Kwa sababu nitawasamehe maovu yao na dhambi zao sitazikumbuka tena"
Mara nyingi kwa akili za kibinadamu huwa tunafikiri kwamba tunaweza kutomsamehe mtu kitu fulani na maisha yakaendelea kama kawaida kama haukusoma makala ya mlango bofya hapa
Lakini ukichunguza siyo kweli kuna vitu vingi tunakosa kutokana na kuwa na kinyongo mioyoni mwetu kwa mfano maombi ya mtu asiyesamehe ni kelele kwa Mungu
Tunasisitizwa kutengeneza na jirani zetu kabla hata ya kuingia katika maombi ndipo tunapoweza kubarikiwa na Mungu
Msamaha umegawanyika sehemu mbili, ya kwanza ni kujisamehe wewe mwenyewe na pili ni kumsamehe yule aliyekukosea
Ukifanya dhambi fulani au kukosea unapaswa kujiomba msamaha peke yako na kisha baadaye kumuomba Mungu msamaha pia
Usipofanya hivi mara nyingi utakuwa ni mtu wa kujilaumu na kujidharau na kujiona kwamba hauna thamani na hakuna kitu cha maana ambacho unakifanya
Ukiwa unajiomba msamaha unaweza kusali sala hii " Moyo wangu najua nimekukosea kwa kufanya ........ ninaomba nisamehe, ninatengeneza upya, ninakuahidi sitarudia tena kosa hili ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya
Tunauomba moyo msamaha kwa sababu moyo ndiyo unaooumia katika kosa lolote lile ndiyo maana Biblia ikaweka wazi kwamba linda sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo kwa sababu ndiko zitokako chemchem za uzima
Unapojiomba msamaha na kuomba msamaha amini imekuwa hivyo sababu wapo ambao huwa bize kumkumbusha Mungu maovu yao wakati Mungu ameshayasahau
Isaya 43:25 "Mimi,naam, Mimi ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako
Maana ya niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, ni kwamba Mungu hutusamehe ili aweze kutubariki, kama asingalitusamehe asingeweza kutubariki
Hivyo hivyo kama usiposamehe huwezi kubariki wengine kumbuka umeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, lakini pia wewe huwezi kubarikiwa
Mara nyingi mtu ambaye hasamei ana dhambi kuliko yule ambaye amekukosea kwa sababu huenda unayesema kakukosea hafahamu kama alikukosea ni suala la kumuambia ulinikwaza sehemu fulani na sikupenda lakini nimekusamehe
Hivyo ni muhimu sana kujisamehe na kusamehe wengine ili kumyima Shetani nafasi ya kukukumbusha mabaya yaliyopita
Inaendelea .......
Mwanamke Thamani!
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana