Ili uweze kuingia sehemu yeyote unahitaji kutafuta mlango wa kuingilia ulipo
Binadamu naye ana milango ambayo vitu hupita kupitia hiyo, milango mikuu ni miwili ambayo ni macho na masikio
Kitu chochote huingia akilini kupitia macho (kuona au kusikia), kadhalika kitu huingia mwilini kupitia mdomo
Hivyo tuna milango mbalimbali ulimwenguni ambayo ni;
a) Milango ya kiroho
b) Milango ya kidunia
c) Milango ya kimwili
Biblia inaposema mlango mwembamba ina maana mtu asiyekuwa na mambo mengi, mpana mtu mwenye mambo mengo 1petro 3:6
Yesu Kristo ndiye njia ya kweli na uzima (ndiye njia nyembamba itupelekayo uzimani)
Unapokuwa kwenye mlango mpana unakosa hekima na maarifa sababu ni mlango unaoruhusu kila kitu hauchagui kila linalokuja unapokea
Tunapaswa kuishi kwenye mlango mwembamba tukimuogopa Mungu maana yeye ana majibu ya mambo yote
Mtu anayefanya maombi siyo wa kucheza naye kwa sababu anafanya mawasiliano na Mungu moja kwa moja
Mungu huangalia ni mlango gani umejifunga na kusababisha maisha yako kuharibika naye huufungua tena na kuachilia baraka zake
Huwa kuna chati za maombi kadiri unavyoomba chati yako hupaa hivyo tunapaswa kuomba zaidi kila iwapo leo
Maombi ni mtaji, biashara pamoja na kazi huaribika na huweza kufa pasipo maombi
Hatuwezi kuuteka ulimwengu wa kiroho pasipo maombi, watu wengi hupenda kuombewa badala ya kujiombea wenyewe
Tunapaswa kuhama kutoka kiwango cha kupenda kuombewa na kujiombea wenyewe hapa ndipo tunapokuwa wana wa Mungu na siyo watoto wa Mungu
Watoto wanapofanya vibaya shuleni, usiwapige wala kuwalaumu jiulize mara ngapi umewaombe wao na rafiki zao
Wakati mwingine maombi yetu huzuiwa angani, unakumbuka wakati Daniel anasali Mungu alimwambia maombi yako Shetani aliyezuia yasinifikie?
Hivyo tunapaswa kupanda viwango vya kuomba ili tumshinde yule mwovu na hila zake
Kuna vijana watatu huwa napenda sana habari zao Shedraki, Meshaki na Abelnego, hawa watu walibadilisha nchi
Unajua haijalishi una elimu gani, urefu au ufupi gani, mnene au mwembamba lakini ukimtumikia Mungu anakuwezesha kufanya mambo makubwa na ya ajabu
Tunataka kuona nchi yetu inabadilika na milango mingine ya mafanikio ikitokea wa kuibadilisha na mimi na wewe
Usikae ujidharau wala ujione si chochote wewe ni mtu mkubwa na mwenye uwezo na maajabu
Mwanamke Thamani
yeah thank you
ReplyDelete