Jana tuliona muasisi wa familia ni Mungu peke yake na siyo mwanadamu na leo tuangalie kwa nini Mungu aliamua kuwa na familia
Mungu alianzisha taasisi ya familia ili aweze kutubariki ndiyo maana baada tu ya kumuumba Adamu na Hawa kitu cha kwanza kukifanya aliwabariki, ndoa/familia ipo kwa ajili ya kubarikiwa Mwanzo 1:28 "Mungu akawabariki.....
Kama hukusoma makala ya jana ya binadamu tumetokea wapi ambayo ni sehemu ya kwanza ya makala hii unaweza ⇒⇒⇒KOBOFYA HAPA KUISOMA
Lakini pia familia ipo kwa ajili ya uzao na kuongezeka Mwanzo 1:28........."Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke......, Mungu ni wa maongezeko haupaswi kukubali hila za Shetani za kukuzuia kupata uzao au maongezeko katika kitu chochote kile
Kama ndege Mungu aliwabariki na kuwaambia wakazae na wakaongezeke, Je si zaidi kwako wewe binadamu kuongezeka kiuzao kwa sababu kiwango cha juu kabisa cha uumbaji wa Mungu ni binadamu tizama..
Mwanzo 1:22 "Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi". Leo hii ndege hawaangaiki uzao wanaongezeka tuu
Hata binadamu amebarikiwa ni adui anakushambulia na hataki upate kwa sababu utakapopata yeye hafurahii siku zote Shetani amejawa wivu na hajaanza leo alianza tangu awali ndio maana alitaka pia kuiba nafasi ya Mungu
Ni lazima kumtizama Shetani katika namna hii ili kuzitambua hila zake pindi ambapo anakutegea mitego katika suala fulani
Familia pia ni kwa ajili ya kuijaza nchi na kuimiliki, Mwanzo 1:28........mkaijaze nchi, na kuimiliki ......furaha ya ufalme ni ongezeko la watu, karamu, sherehe huwa na maana pale watu wanapokuja na kufurahia nao kwa pamoja
Sisi ni wana wa Mfalme ndio maana anataka tuongezeke ili tuzidi kumtukuza, kumsifu na kumuabudu kwa sababu Yeye ni Mungu wa maongezeko alimuapia Abrahamu kwamba ataongeza uzao wake kama nyota za angani
Mafanikio makubwa huja baada ya kuoa kwa sababu unapooa unapata kibali mbele za Mungu, Mithali 18:22 "Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.
Kuna baadhi ya mambo ambayo huwa hayasogei mpaka upate mke, kuna baadhi ya fedha ambazo hutakaa uzione mpaka utakapooa haya siyo maneno yangu ni Biblia inasema Mithali 31:10 "Mke mwema ni nani awezaye kumuona,.........
Mstari wa 11 "Moyo wa mumewe humuamini wala hautakosa kupata mapato" maana nyingine ni hakuna njaa baada ya ndoa, ndoa ni baraka
Tena Mungu akaona haitoshi akasema Waebrania 13:4 " Ndoa na iheshimiwe na watu wote........." unashangaa kwa nini huheshimiwi sababu ni haujaoa au kuolewa
Kati ya vitu vya kukataa na kupambana navyo kwa nguvu na kuhakikisha Mungu anakupatia ni ndoa, uzao na maongezeko ( katika afya, roho, uchumi, kazi na karama) usikubali kutokuoa nawe siyo toashi, usikubali kutokuolewa nawe siyo sister
Kama Mungu alikuumba na alimuumba mwenzako jamani tupo wawili wawili duniani hili ni jambo la ukweli mtafute wa kwako kwenye maombi mpaka umpate sababu yupo na hana budi kuja
Ndoa haipo baina ya watu wanaofanana jinsia Walawi 18:22 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo" na kinyume chake ni kweli pia
Mhubiri 4:9 "Wawili ni bora zaidi ya mmoja kwa sababu wana tuzo njema katika kazi yao" mkiwa wawili hata ukijikwaa mwenzio atakuinua, ukikosea mwenzio atakusahihisha n.k ndio maana ndoa ni jambo la baraka
Kuna mtu aliyekuwa na hekima akasema ukitaka kufahamu unakoelekea muulize aliyetoka lakini siyo kila mtu aliyetoka anapaswa kuulizwa leo nitakuambia kwa nini.....?
Mtu yeyote ambaye ndoa imemshinda, alikosea kuoa au kuolewa sababu hii ipo ni lazima kabla ya kuoa au kuolewa uwe na uhakika huyo ndiye namna ya kujua ni somo jingine
Ukimuuliza mtu aliyeshindwa au anayetapatapa kwenye ndoa juu ya baraka za ndoa na raha yake unategemea nini?
Ni kukatishwa tamaa, kuaminishwa uongo na shuhuda za walioshindwa na mwishowe utaairisha kuolewa lakini mfuate ambaye amefanikiwa akupe tamu ya familia na ndoa utaelewa
Wakati mwingine kweli nakuhakikishia taasisi ya ndoa ina vikwazo na migogoro kwa sababu ya baraka ambazo Mungu ameziachilia huko hivyo Shetani na vibaraka wake wako bize kweli kutega mitego na kuharibu kila baraka Mungu alizozieka
Kabla hujaanza kula asali lazma uchome msitu nyuki waondoke ndiyo ushushe mzinga urine asali usitegemee ukiolewa au ukioa utastarehe tuu hauombi wala hausomi neno la Mungu wala haufungi kwa ajili ya familia yako na Shetani akuchekee kaa apo uone!!
Silaha zote za kumshinda adui unazo ni kiasi kidogo cha kuamka na kuzitumia kumlipua mama ukiolewa jiandae kuilinda familia yako kwa maombi tena haswaa maana ukilegea unatunguliwa vizuri tuu inaitwaga kill me soft
Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa hili lililoandikwa hapa na akupe neema ya kulifanyia kazi katika Jina la Yesu Kristo aliye hai
Kama unataka kujiunga na mtandao wa Mwanamke Thamani ambao tunajifunza neno la Mungu kwa pamoja na kujifunza namna ya kuweza kutambua kusudi letu katika maisha unaweza kuwasiliana nasi wa whatsup number 0715113636
Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"

No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana