KWA NINI KUNA MIGOGORO KATIKA FAMILIA? - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Monday, July 16, 2018

KWA NINI KUNA MIGOGORO KATIKA FAMILIA?


Jana tuliona kwa nini Mungu alianzisha taasisi ya familia na tukaona sababu kadha wa kadha za kwa nini familia/ndoa ni muhimu na kwa nini Shetani anashambulia taasisi ya ndoa/familia

Kama haukusoma sehemu ya pili ya mada hii inayosema kwa nini familia ⇉⇉⇉GUSA HAPA KUISOMA YOTE

Leo tugeuze somo tuangalie kwa nini kunakuwa na migogoro katika ndoa/katika familia, japokuwa zipo baraka nyingi sana katika familia lakini bado kuna migogoro mingi sana katika taasisi hii

Ndio maana viongozi wa dini, wasimamizi wa ndoa, washauri, wanasaikolojia na makungwi wapo kusuluhisha au kukumbusha wajibu wa kila mtu katika familia

Unaweza kutaja au kuelezea mamia ya sababu za migogoro katika familia jinsi ambavyo wewe unaona lakini kama nilivyovuviwa mimi ninaweza kuzigawanya sehemu tano tuu

I/ Vifungo inaweza kuwa ni kwenye ardhi, kazi, elimu, ugomvi, ulevi, uzinzi n.k na katika mada hii nitaongelea kifungo kimoja tu cha kwenye ardhi

Kifungo cha kwenye ardhi, binadamu ametokea kwenye mavumbi na siku zote mtu hufungwa na kulaaniwa alipotokea tuliliona hili mada ya juzi ya tumetokea wapi

Kaini baada ya kumuua nduguye Abeli alilaaniwa katika ardhi maana nyingine ni alifungwa katika ardhi Mwanzo 4:11 "Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofungua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kutoka kwako"

Kitu kingine cha kujifunza hapa ni kwamba ardhi ina kinywa inameza na kutema ndio maana wachawi huchimbia vitu chini na kuvifunga

Ni lazima tukubaliane kwamba kila kitu kinafanyikia kwenye ardhi iwe ni kilimo, ufugaji, uzalishaji n.k hivyo ardhi ni ya muhimu kwenye ulimwengu wa Kiroho kuliko unavyofikiri

Mchawi akikufunga katika ardhi utakwisha ndio maana ni lazima kujipatanisha na ardhi kila mahali unapokwenda, tulimuona TB Joshua alipokuja Tanzania alitembea peku alichokuwa anakifanya ni kujipatanisha na ardhi ya nchi hii

Huenda kama asingeisemesha ardhi na kujipatanisha nayo labda kuna vitu vingalitokea, mimi na wewe hatujui lakini Yeye anafahamu

Matambiko na kafara zinazohusisha umwagaji wa damu hufanyika kwenye ardhi hata unaponunua kiwanja huna budi kukitakasa kwa damu ya Yesu inayonena mema maana hujui kilifanyika nini

Huna budi kuwa wa kwanza kuisemesha ardhi kabla ya wakuu wa giza na kumiliki milki zako Mfalme Daudi alikuwa na maana aliposema Zab 69:15 "Mkondo usinigharikishe wala vilindi visinimeze, wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.

Hii mada ya ardhi ni ndefu na hatuwezi kuimaliza kwa somo hili tuendelee na jambo la pili linalosababisha migogoro kwenye familia

ii/Kutokujua kusudi lako hasa ni kwa WanaumeWaef 1:11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.

Mungu ana kusudi na kila mtu aliyemuumba kwa sababu ukitizama tangu uumbaji kila alichokiumba alikuwa na kusudi nacho, hivyo haujaumbwa kwa majaribio ila ni ili utimize kusudi fulani

Unajua mke ni msaidizi kama kitabu cha mwanzo kinavyosema unaoa ili aje kukusaidia kusudi ambalo Mungu kaliweka ndani yako

Kusudi siyo ajira wengi hufikiri wakipata ajira au kazi fulani wamepata kusudi hapana, kusudi ni wito ni kile ambacho Mungu kakiweka ndani yako hakihitaji shule ili kukifanya unaweza kwenda tuu kujiweka vizuri zaidi na kujiimarisha

Unajua kabla ya Yesu kuanza kusudi lake aliishi kama binadamu wa kawaida kabla ya miaka 30 alifanya kazi ya useremala na baba yake lakini kusudi alianza kulifanya baada ya miaka 30 na alilifanya kwa miaka 3 tu

Paulo alikuwa akitengeneza mahema hii ilikuwa ni kazi yake lakini alikutana na kusudi lake baada ya mguso wa Mungu

Petro na nduguye walikuwa wavuvi tena waliosomea hii ilikuwa ni kazi yao lakini walikutana na kusudi baada ya Yesu Kristo kuanza huduma na kuwafanya mitume

Daudi rafiki wa Mungu alikuwa kazi yake ni kilimo katika sekta ya ufugaji alikutana a kusudi lake baada ya kupakwa mafuta na kuwa mfalme wa Israel

Hiyo ni baadhi ya mifano na wengine wengi ambao unawafahamu Warumi 12:6-8 imezielezea karama hizo ambazo ni Unabii, huduma, kufundisha, kuonya/kushauri, kutoa, uongozi na kurehemu

Kila mtu hapa duniani yupo katikati ya moja kati ya karama hizo hivyo ni kumuomba Mungu kukuonesha sehemu yako ni ipi

iii/ Kukosekana kwa maono, kama hujajua kusudi basi hata maono huwezi kuwa nayo maono ni jinsi ambavyo kusudi lako litakavyokuwa mbeleni ni jinsi ambavyo Mungu atakufanikisha na maono yapo kwa njia ya picha

Maono ni kuuona wakati wako ujao sasa kwa sababu Mungu hutangaza mwisho tangu mwanzo ina maana kama umeshalijua kusudi Mungu atakuonesha maono ya namna mwisho wa kusudi lile utakavyokuwa

Utajiona ukitenda kusudi lile, kama vile ni sasa, imani yako itabadilika na utajiona kuwa mtu mpya kabisa usishangae kwa nini watu wanaanzisha vitu na kila kitu kinaonekana kiko kinyume nao lakini bado wanakomaa tuu ni kwa sababu wameshauona mwisho

Hivyo jambo lolote linalotokea sasa haliwahusu ni la muda tuu ila Mungu kashaonesha mwisho wao wanakomaa kuuona mwisho wake

Na ukishaoneshwa maono unayaandika chini Mungu alimuambia Habakuki aiandike njozi ili kuisoma kama maji Habakuki 2:2 BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.

Hivyo kama haujaona maono ni wapi unaelekea hata mke uliekuwa naye utamchanganya ni lazima uwe na picha halisi na umshirikishe mnapokwenda

iv/ Kukosekana kwa mipango thabiti, ukikosa maono huwezi kuwa na mpango kwa sababu mpango unatokana na maono ambayo yametokana na kusudi hivyo ukikosa kusudi umekosa maono na umekosa mpango

Yer 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho, English version imeelezea vizuri mstari huu haijatumia neno Mawazo bali Plan ambao kiswahili ni mpango

Mungu ana mpango na kila mtu tena mzuri lakini ni mpaka utakapojishika naye ndipo atakuonesha kile alicho nacho kwa ajili yako

Mara nyingi kwenye familia kunakosekana mipango ya nini cha kufanya miaka miwili au mitatu au mmoja na matokeo yake ni matatizo hasa ya kifedha

NB:Hakuna uhusiano kati ya picha na mada iliyoandikwa

Kama unatamani kuwa mmoja wa wanawake ambao wanamtumikia Mungu kwa pamoja unaweza pia kuwa mwanachama kwa kutupigia simu 0715113636 au kuandika sms whatsup 

Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"


No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana