Kitabu cha Mwanzo katika sura kwanza kinaelezea uumbaji wa dunia, sura ya pili ni namna ambavyo Mungu alifanya uumbaji Mwanzo 1:27 "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba mwanamke na mwanaume aliwaumba"
Lakini ni vema pia kufahamu kwamba jina la Adamu lilikuwa siyo jina la mwanaume peke yake bali lilikuwa jina la wote yaani mwanamke na mwanaume, Mwanzo 5:2 "Mwanaume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa"
Kama haukusoma makala ya jana ya Hatuangalii bali tunafanya tafadhali unaweza kuisoma tena yote kwa ⇒⇒⇒⇒KUBOFYA HAPA
Jina la Hawa ni Mwanamume alimuita Mwanamke kwa sababu alitwaliwa katika Mwanaume na maana ya Hawa ni mama yao wote walio hai Mwanzo 3:20
Moja ya tofauti kubwa kati ya mwanaume na mwanamke ni kwamba mwanaume ameumbwa kwa mavumbi ya ardhi Mwanzo 2:7 "Bwana Mungu akamfanya mtu (mwanamume) kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai"
Na hii ndio sababu mwanamume alilaaniwa katika ardhi baada ya kula tunda la mti wa mema na mabaya Mwanzo 3:17 "Akamwambia Adamu kwa kuwa umesikia sauti ya mke wako............ ardhi imelaaniwa kwa ajili ya kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako"
Mwanamke hakuumbwa kutokea kwenye ardhi bali kutokea kwenye ubavu Mwanzo 2:21"........kisha akatwaa ubavu wake mmoja akafunika nyama mahali pake. Ule ubavu aliutwaa katika Adamu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu"
Hii ndio sababu mwanamke baada ya kuasi alilaaniwa katika mwili sababu alitwaliwa kutoka kwenye mwili Mwanzo 3:16 "Akamwambia mwanamke hakika nikakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala"
Hivyo kimsingi mtu analaniwa sehemu alipotokea iwe ni ukoo, familia, nchi au mkoa ndio maana ni muhimu kujitenga na madhabahu ambazo zipo kinyume na mpango wa Mungu kwenye maisha yetu ya kila siku.
Nani alianzisha Familia?
Kamwe asikudanganye mtu familia ni jambo jema na ndio maana muasisi wa kwanza wa familia naam yani ndoa alikuwa ni Mungu mwenyewe
Mwanzo 2:16 Bwana Mungu akasema, Si vema mtu awe peke yake nitamfanya msaidizi wa kufanana naye. Hivyo kimsingi kuwa peke yako siyo suala jema na Mungu aliliona hilo
Makala hii inaendelea usikose kuifuatilia tena siku ya kesho.......
Kama unataka kuwa mmoja wa wanawake ambao wanatamani kujiunga katika mtandao wa mwanamke thamani ambapo tunashirikishana habari mbalimbali juu ya neno la Mungu na kutambua kusudi letu unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba/ whatsup 0715113636
Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"

No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana