HATUANGALII BALI TUNAFANYA! - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Wednesday, July 11, 2018

HATUANGALII BALI TUNAFANYA!


Mambo huwa hayatokei tuu yenyewe, watu hufanya mambo kutokea na kila hatua unayochukua kwenye maisha yako inamaanisha mambo mawili muhimu ambayo ni ;-
Kukupeleka na kukusogeza karibu na kusudi lako au kukuondoa kabisa kwenye kusudi ambalo Mungu amekuweka ndani yako

Kwa sababu watu ndio wanafanya mambo kutokea kulingana na hatua wanazozifanya hupelekea wao kuanza kujisifu kwa kile kilichotokea

Pumzi nzima nyuma ya Mwanamke Thamani ni kukuonesha, kufungua na kukufundisha juu la kile ambacho Mungu kaweka/karama kwenye maisha yako

Kama haukusoma makala ya Sifa kwa binadamu ni kilevi sehemu ya kwanza ⇉⇉⇉ GUSA HAPA KUISOMA 

Nilichokiona, nilichojifunza na ninachoendelea kusikia ni hiki kama unataka kuwa wa kawaida fanya mambo ya kawaida, kama ukiamua kufanya mambo katika ukubwa ....

Kama ukitaka kupanua biashara zako, utumishi wako au kuchochea karama yako jiandae na kukataliwa na kupingwa na saa zingine kusingiziwa tena na wapendwa

Wanaohudhuria pale Victoria Sheli kila Jumamosi wengi wanaofunguliwa ni wale waliofungwa kwenye uimbaji, kwenye karama walizobeba na tumeshuhudia mara nyingi sana Mungu akifanya hivyo

Hatufanyi hivi kwa sababu ya sifa ila kwa sababu tunataka kuupeleka ufalme wa Mungu mbele sawa na Mathayo 6:33 "Bali utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na haki yake na hayo mengine yote mtazidishiwa"

Mithali 27:21 ".........Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake, sifa ndio zinaleta majaribu, sifa ndio zinafanya mtu mmoja kujiona bora zaidi ya mwingine
Hauna haja ya kutumia nguvu nyingi kuonesha kwamba unajua kitu fulani bali unapaswa tuu kukifanya kwa sababu Imani ya kweli ni lazima itaambatana na matendo Yakobo 2:14

Hatuangalii tuu, hatusubirii tuu, hatutamani tuu kisha tukaacha kuchukua hatua, tunachukua hatua na kuwa sehemu ya mambo makubwa yanayotokea

Tunatambua ya kwamba hakuna kitu cha thamani ambacho kinapatikana bure pasipo kukilipia gharama, kutoka nje ya aibu, umasikini, fedheha ni lazima ulipe gharama ya muda, kuomba, kujifunza, kumtumikia Mungu na kufanya kazi kwa bidii

Hatusaidii watu na kuwafungua kisha kesho tunasimama barabarani, tukasimama kwenye umati na kuwasema vibaya au kupinga kile wanachokifanya na kuona hakifai

Bali tunasaidia ili kuupeleka ufalme wa Mungu mbele sifa ya mwalimu ni kutengeneza walimu wengine na kamwe siyo idadi ya wanafunzi anaowafundisha

Yesu Kristo aliamua kutengeneza wanafunzi/mitume ambao ndio walioifikisha Injili ilipo sasa pasipo wao huenda Ukristo usingalienea sehemu zote hizo

Kitakachobaki baada ya wewe kuondoka ndio madhara ambayo utumishi wako umeleta, usifurahie kukumbatia wanafunzi bali furahia kutengeneza walimu, wachungaji, wainjilisti, wafanyabiashara, waimbaji n.k

Hawa watafanya kazi zaidi yako na kwa niaba yako hata wakati haupo na kama wanafanya sasa ungali hai watie moyo na wapongeze na furahia kwa kuwatengeneza

Tunapokuwa tunajisifu wenyewe kwa mambo fulani tuliyofanya au msaada au huduma fulani tuliyomfanyia mtu mara nyingi huwa tunamuondoa Mungu kwenye utendaji na kujiweka sisi

Ndio maana Mithali 27:2 ikasema "Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; Mtu mgeni wala si midomo yako wewe

Kama ni sifa na ziwe ni za Bwana Yesu Kristo, tuache kutumia muda mwingi kujisifia kwa tuliyofanya sababu siyo mapenzi ya Mungu na hata ukisema katikati ya ushuhuda usisahau ni Mungu kakuwezesha

Haya mayowe tunayoyapiga juu ya kazi za watu, biashara za watu, utimishi wa watu, huduma za watu au karama za watu waacheni watu wayaone wenyewe

Bado unaweza kujiunga na masomo ya whatsup kwa kuandika ujumbe kwenye whatsup namba 0715113636 pia unaweza kuwa mwanachama wa Mwanamke Thamani na kuanza kumtumikia Mungu pamoja na sisi wakati wote

Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana