Tupo kwenye
majira ya kwa resma ambayo Wakristo hufunga na kuomba kwa sababu tunakumbuka kipindi
ambacho Yesu mwana wa Mungu aliteswa na kusulubishwa kwa ajili ya dhambi zetu
Kipindi hiki
kinatukumbusha majira ya mwisho wa safari ya Bwana wetu Yesu Kristo katika kuhubiri
habari njema ya wokovu na kukombolewa kwa watu wenye dhambi kutoka kwenye maovu yao, katika kipindi hiki
tunajutia dhambi zetu, tunaungama na tunajitakasa
Kama haukusoma makala ya Upepo hauamui uelekeo wa meli unaweza Kugusa Hapa ukaisoma yote
Kama haukusoma makala ya Upepo hauamui uelekeo wa meli unaweza Kugusa Hapa ukaisoma yote
Tunakumbuka
kwamba Wanawake ndio walikuwa mstari wa mbele kwenye safari hii ya mateso
ambayo Yesu aliiendea kipindi kile na hata wakati anateswa na kusulubishwa bado
walikuwepo hata alipokufa na kufufuka walikuwa wa kwanza kuona kwamba jiwe
lililokuwepo kaburini mwa Yesu halipo tena
Team ya
Mwanamke Thamani nasi tumeamua kutumia
kipindi hiki vyema kwa kufunga, kuomba na
kujitakasa tukiungana na Wakristo wengine
ulimwenguni kote ambao nao wanafanya
vivi hivi, hii ni moja ya sababu ya kwa nini tumekuwa kimya mwezi huu
Pia
tunajiandaa kwa ajili ya tamasha la BINTI JITAMBUE linalofanyika Mwanza kuazia
tarehe 8-10 mwezi wa tatu, Mwanamke Thamani ikishirikiana na Ev.Tedy Stephen
tunaandaa Kongamano la maombi na maombezi ambalo litafanyika tarehe 30 na 31
mwezi wa tatu jijini Dar
Wengi
watafunguliwa na kupona, watauona ukuu na uweza wa Mungu katika maisha yao,
tunakukaribisha katika Kongamano hili la kipekee na litakalokuwa na mguso wa
aina yake, njoo na wewe na familia yako, ndugu, jamaa, rafiki taarifa juu ya
eneo tutasema hapo baadae ili kwa muda huu unaweza kuwasiliana na timu nzima ya
maandalizi kwa ..
Ev.Tedy
Stephen 0754-563-253 ⇣⇣⇣⇣⇣⇣⇣
Mwl. Sialove
Lukumay 0715-113-636 ⇣⇣⇣⇣⇣⇣
Mwl .Pendo Emmanuel 0755- 715-715 ⇣⇣⇣⇣⇣⇣
Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"




No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana