Jana tuliangalia umuhimu wa kuwa na umoja katika familia, leo tunaenda kuangalia uponyaji katika familia
Kama hukusoma sehemu ya nne ya mfululizo wa makala hii ya familia juu ya umuhimu wa umoja ⇉⇉⇉⇉ GUSA HAPA KUISOMA
Ninaposema uponyaji usiyeyushe au kufupisha maana uponyaji ni neno pana siyo lazima iwe ni ugonjwa katika mwili inaweza kuwa ni uchumi, ndoa, vifungo, ugonjwa n.k lakini kwa mada hii niongelee uponyaji kwenye magonjwa
Katika kanisa leo hii kuna wagonjwa na watu waliofungwa katika vifungo mbalimbali, hatuwezi kulilaumu kanisa au uongozi ndio maana karama zikawepo mbalimbali zinazosaidia kanisa katika kutimiza kusudi la Mungu
Upungufu wa watumishi na wingi wa vifungo na hila za Shetani ni moja kati ya sababu inayopelekea kuongezeka kwa watu wengi waliofungwa na wanaokwenda huku na kule kutafuta uponyaji
Lakini pia kutokuelewa mpango wa Mungu na asili ya Mungu imekuwa ni moja ya sababu kubwa ya magonjwa na vifungo kwa Wakristo wengi
Uponyaji ni fungu letu na ndio kusudi la Yesu Kristo kufa lakini Shetani amebadilisha maana na kuwaaminisha watu kuumwa au kufungwa katika sehemu fulani ni sehemu ya maisha
Kuwa na afya ni bora kuliko kuponywa ukumbuke sisi ni mfano wa Mungu na kama ni hivyo na unaamini basi unao uwezo wa kuidai afya yako ya kiungu
Mungu anataka kila mtu awe na afya yake kuliko kuponywa ndio maana akasema
3Yohana1:2 "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
3Yohana1:2 "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
Shetani baba wa hila hajawahi kuumba kitu uzima na afya viliumbwa na Mungu yeye akapindisha kwa sababu ya hila akaleta magonjwa na vifungo
Ugonjwa au vifungo siyo fungu letu kwa sababu yupo Simba wa Yuda ambaye alishalipia gharama ya mateso yote ambayo yanamuandama binadamu ndio maana neno la Mungu linasema katika Isaya 53:5 "Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona
Wakati fulani mtumishi mmoja alikuwa akihubiri na akasema watu wote ambao ni wagonjwa ni wezi, hii sentensi ilinishangaza lakini aliendelea kuelezea hoja yake na kuonesha kusudi la Yesu kuja akasema kama Yesu aliyachukua maovu yetu na tabu zetu na kwa kupigwa kwake sisi tumepona sasa magonjwa watu wanayapatia wapi kama siyo wezi?
Mungu anasema kwamba tukimtumikia Kutoka 23:25 "Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
Je magonjwa yanatoka wapi?
Tumeona Shetani hajawahi kuumba kitu chochote Mungu aliumba afya na uzima Shetani akapindisha akaleta magonjwa na kifo
Magonjwa kifupi yanatokana na mambo makuu matatu
Jambo la kwanza ni Uovu, uovu ni dhambi ambayo imekomaa hata ikapita kutoka kizazi kimoja hata kingine dhambi hii hufungua milango ya magonjwa na mahangaiko mf babu zako wanaweza kuwa sababu ya magonjwa ulionayo
Uovu unaweza kusafiri kupitia cheneli zifuatazo inawezekana kwenye dhambi inayojulikana au isiyojulikana, nadhiri, viapo vinavyohusisha damu, nchi kwa watu wake kwa mfano Jer 3:6-10, kuasi, kurithi kwa wazazi mwanz 16:1 pia inawezekana kupitia majina 1Nyak 4:9-10
Jambo la pili ni Laana, laana ni tamko hasi ambal husemwa kwenye maisha ya mtu, familia, kundi la watu au nchi ukisoma Biblia kuna mtu alikuwa anaitwa Baalam huyu alikuwa kazi yake ni kutamka laana kwa Watumishi wa Mungu
Jambo la tatu ni dhambi, hii ni kwenda kinyume na neno la Mungu siri ni hii laana na uovu unaendelea kuwepo kwenye maisha ya mtu au familia fulani alimradi tuu wanafanya dhambi
Unapotubu na kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako unajiweka katika nafasi nzuri ya kuiondoa laana na uovu na ndio maana wokovu ni jambo la kwanza kabisa kwa binadamu
Tufanyeje sasa kama tunaumwa?
Tunapaswa kuidai afya yetu kwa nguvu suala la kudai haki na stahiki zako siyo lelemama ni mapambano ndio maana Mathayo11:12 inasema "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
Haukai kuongea maneno na kutangaza kwamba naumwa naumwa kwa kila mtu bali unazivaa silaha unaingia kwenye ulimwengu wa Roho unapigana kuidai afya yako ya kiungu
1Kor 4:20 "Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu, hizi nguvu siyo za mwili ni za Kiroho hivyo ni lazima kujijenga katika eneo la Kiroho hata Kiuchumi
Instagram @Mwanamkethamani
Kama una shauku na hamu ya kujifunza neno la Mungu pamoja na kujiunga na network ya wanawake ambao kwa pamoja tunamtumikia Mungu na kujifunza juu ya kusudi ambalo Mungu ameweka maishani mwetu unaweza kuwasiliana nasi kwa simu nambari 0715113636
Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"
©mwanamkethamani articles gallery use under permission only

No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana