WOGA UNAONDOA UWEPO -V - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Thursday, January 4, 2018

WOGA UNAONDOA UWEPO -V




Ilipoishia....

Hivi ndivyo tunapoishinda hofu inayotusababishia woga katika maisha yetu, tupo hapa kwa muda mchache uwepo wetu lazima uwe wa utukufu na wa kustareheshwa pande zote


Kama hukusoma sehemu ya nne ya makala hii ya woga unaweza kubofya hapa kuisoma
Twende sasa!


Ulishawahi kukaa chini ukafikiri juu ya huu msemo wa wahenga "Woga wako ndio umasikini wako"?
Unafikiri aliyeusema msemo huu alikuwa anafikiri nini? Kila neno lina maana na ujumbe fulani uliokusudiwa

Anachojaribu kutueleza ni kwamba kuna umasikini mwingine unatokana na woga na sio kukosa elimu au kufahamiana na watu kama wengi wanavyodai

Aina hii ya umasikini huwakumba sana wasomi kwa sababu hutaka kutafuta/ kufanya vitu fulani vinavyoendana na hadhi yao

Wapo wasomi wengi leo hii wangeamua kukaanga chipsi au kuanzisha migahawa wangefika mbali zaidi kuliko kazi za kuajiriwa wanazozisubiri

Ila kwa sababu ya woga na kufikiri watu watawaonaje pindi watakapojikita katika biashara za namna hii wanaishia kuwa na maisha duni na wasiyoyapenda 

Ukiwa muoga anza kujichunguza vitu unavyoangalia, unavyosoma na unavyosikia kwa sababu vina uwezo wa kukuletea woga

Mtu anayesikiliza, kusoma na kuangalia kila wakati habari za vita, ajali, kuporomoka kwa uchumi n.k hatakawia kuingiwa na hofu juu ya maisha na uhai wake

Husahau kabisa maneno yaliyoandikwa katika 1Wakoritho14:33 Kwamba "Kwa maana Mungu si wa machafuko bali wa amani, kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu"

Ni lazima kuwa makini na vitu tunavyoingiza katika akili zetu vinayo uwezo wa kutubomoa au kutujenga 

Woga ni uchaguzi ni kama vile mtu anavyokwenda Kariakoo au Karume kuchagua nguo na kusema nataka hii na ile siihitaji

Ndivyo ilivyo kwenye woga na ujasiri unao uwezo wa kuamua kuchagua woga au ujasiri hili ni juu yako, wala siyo jukumu la Mungu wala mzazi wako

Japokuwa woga siyo kitu kinachotokea chenyewe lakini wengi ni wepesi kuchagua woga kwa sababu mtu haitaji nguvu ya ziada kuwa mwoga

Pale woga unapokujia pambana nao wazi wazi kwa kufanya kile unachokiogopa mara nyingi kadiri uwezavyo

Utakapoweza kufanya hivyo woga juu ya kitu hicho hupungua na unavyoendelea kukifanya zaidi hufikia sehemu woga huo unaondoka na kinakuwa kitu cha kawaida kabisa kwako

Sijui ni nini kinakupa woga sasa hivi, inawezekana ni familia, kazi, afya yako au pengine ni elimu yako

Napenda nikutaarifu kwamba woga hauwezi kukupatia kitu chochote kile kizuri unachotamani kuwa nacho maishani

Isitoshe huo mzigo uliokuwa nao mtwike wote Bwana naye atakuegemeza na hatokuacha udondoke milele zaburi 55:22
Mwanamke Thamani!

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana