TUNAKOELEKEA NI KWEMA ZAIDI - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Thursday, January 4, 2018

TUNAKOELEKEA NI KWEMA ZAIDI


Kuna wakati huwa ninakaa na kufikiria nilikotoka ninabaki namshukuru Mungu kwa sababu amenitoa mbali sana
Sio kwa uwezo wangu bali ni kwa uweza wake yeye ambaye hunitia nguvu kila wakati
Kuna kipindi mtu unapitia changamoto nyingi na pengine unaona huenda hata watu wamekutenga au Mungu kakusahau
Katika kipindi hiki kama uliwahi kuwa na kitu kizuri kipindi cha nyuma mfano kazi au biashara halafu ikafa ndipo unapoanza kuvikumbuka
Ila wakati wazo la namna hii linakujia unapaswa kufahamu kwamba Mungu siyo wa mambo ya kale tuu bali ni wa sasa na milele
Ninataka kukuambia kwamba yaliyopita achana nayo weka tumaini lako kwa Mungu na mambo yajayo
Hii ni kwa sababu hauendi nyuma kwenye maisha bali unaenda mbele na ili kuweza kwenda mbele ni lazima usahau maumivu ya nyuma
Mtu mmoja akasema akikumbuka changamoto aliyopitia kipindi cha nyuma ni kwa lengo la kujifunza tuu na si vinginevyo
Inawezekana umeumizwa sana katika ndoa, mahusiano, kazi , biashara haziendi au pengine watu wanakudharau
Mungu leo anakuambia "Ninajua mpango nilionao juu yako ni mpango wa kukufanikisha na siyo kukuumiza"
Mungu anao mpango na maisha ya kila mmoja na mpango wake ni kutupa tumaini jema na kunyoosha kusudi letu
Huenda wewe ni mtumishi mzuri, lakini thamini sehemu uliyopo sasa ndipo Mungu atakuinua na kukupandisha sehemu nyingine
Aliye mwaminifu katika vitu vidogo Mungu humuongezea na vikubwa kwa sababu mambo makubwa ni matokeo ya mafanikio ya mambo madogo
Usidharau kabisa sehemu uliyopo mshukuru sana Mungu kwa sababu ni sehemu njema na ya kupendeza, kila asubuhi unapoamka mpe shukrani kwa jinsi ulivyo
Unajua Mungu kakuumba kwa namna ya ajabu sana unapendeza, unavutia na ni wa pekee ndio maana upo hivyo ulivyo
Siku zote kumbuka mtu anayekudharau anamdharau Mungu na siyo wewe kwa sababu wewe ni mfano wa Mungu
Sikio la Mungu siyo zito kiasi hicho asisikie wanayokusema, macho ya Mungu hayajajifunga asione wanaokung'ong'a
Mungu ni wa pekee na wa ajabu kila amtumainiye na kuliamini neno lake huthibitika kwake, amini naye atafanya
Chunguza utagundua Mungu hupenda kuwainua wanyonge na kuwaketisha na wafalme kwa ajili ya utukufu wake
Ni furaha zaidi masikini akitajirika kuliko tajiri akizidi kujiongezea mali na ndio maana Mungu hupenda kuwainua wanyonge
Lipo tumaini jipya, lipo pambazuko jipya Mungu hajaacha kusema na wewe hata sasa, amka uangaze muda wako umefika!

Mwanamke Thamani

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana