Ilipoishia.....
Kubwa kabisa usisahau kumtafuta Bwana Mungu akuponye na hofu zako zote Zaburi 34:4
Kama hukusoma sehemu ya tatu ya makala hii unaweza kubofya hapa kuisoma
Twende sasa!
Katika Biblia kinyume cha woga ni ujasiri na tunahimizwa kuwa na Imani na kuwa mahodari 1Kor 16:13
Ili kuweza kupambana na woga hatuna budi kuwa na ujasiri na watu wenye imani ya kutosha
Huwezi kupata haki yako kwa Mungu kama wewe siyo jasiri na haupo tayari kupigana kwa ajili ya kile ambacho unakihitaji maishani mwako
Ufalme wa giza upo bize sana kuhakikisha haupati baraka zako unazohitaji kutoka kwa Mungu, ndio maana Shetani atatumia kila mbinu kukuletea woga ili kukutoa nje ya baraka zako
Tunapojifunza habari za kina Daudi, Paulo, Yusufu, Musa kina Danieli, Joshua na wengineo tunajifunza ujasiri na mapambano
Ukisoma Mathayo 11:12 inasema kwamba ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu ndio wameuteka
Maana nyingine ni kwamba kama wewe ni dhaifu, mwoga, mwenye wasiwasi na kusita katika mambo yako huwezi kuuteka ufalme wa mbinguni
Tupo hapa duniani kwa kusudi maalumu na tukiendekeza woga katika maisha yetu, tutashindwa kuishi kusudi letu
Woga humfanya mtu kushindwa kufikiri vizuri, kupangilia vitu vizuri, kufurahia na wengine na pengine kushindwa kufanya mambo yako vizuri
Ukichunguza vizuri woga haupo kwenye kitu ambacho tayari kimetokea bali kile ambacho kitakachotokea
Hakuna mtu mwenye woga kwenye kitu ambacho kimeshamtokea, ni hofu ya mambo yajayo inachochea woga kwenye maisha yetu ya sasa
Woga unamnyima mtu kuishi maisha ya sasa na ya baadae, kwa sababu wakati ulionao sasa unautumia kuwaza mambo yajayo, woga ni kuogopa kitu ambacho hakipo
Woga upo kwenye akili na akili zetu ni kama sumaku hunasa na kuunganisha mambo yanayoendana na kile tunachokifikiri
Suleimani alisema "Awazavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo" mimi ninaongezea "na ndivyo itakavyokuwa"
Hivyo ukiogopa suala fulani akili yako itavuta na kukuletea mazingira, hali na matukio ya vitu vinavyoendana na woga wako
Woga hautokani na maisha bali ni hali ambayo ipo kwenye akili, ni kukosa ufahamu juu ya jambo fulani, unaogopa kwa sababu akili yako umeielekeza kwenye mambo ambayo hayapo
Unapaswa kufahamu kwamba unaweza kuipangilia kesho yako sasa na siyo kuiishi, wengi tunataka kuishi kesho sasa ndio maana tunaishia kuogopa
Kuna ukweli ambao lazima tuusadiki ambao ipo siku utaondoka katika dunia hii, lakini ipo wapi faida ya kuishi kama utakuwa una hofu na mashaka maisha yako yote?
Ifike sehemu ulazimishe akili yako kuona neema hata kwenye ubaya, kuona mpenyo kwenye changamoto, kuona furaha palipo na huzuni
Hivi ndivyo tunapoishinda hofu inayotusababishia woga katika maisha yetu, tupo hapa kwa muda mchache uwepo wetu lazima uwe wa utukufu na wa kustareheshwa pande zote
Mwanamke Thamani!
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana