Ilipoishia juzi
Mpaka Ayubu alipoingiwa na hofu ndipo mabaya yalipoanza kumpata, ukiishi maisha ya kuogopa ugonjwa fulani utaishia kuupata kama hukusoma sehemu ya pili unaweza kubofya hapa kuisoma
Twende sasa....
Joseph Campbell aliwahi kusema kwamba “The cave you fear to enter holds the treasure that you seek” yaani ( Pango unaloogopa kuingia ndilo lenye kito cha thamani unachokitafuta) Joseph Campbell wakati anatamka maneno haya alijua kabisa ni nini anamaanisha
Ni mara nyingi sana alitaka kufanya maamuzi katika maisha yake lakini aliogopa mara kadhaa kutokana na woga
Vitu vingi sana tunavyoogopa kuvifanya, sehemu tunazoogopa kwenda, watu tuoogopa kuongea nao huwa kwa namna moja au nyingine kuna uhusiano na mahali tunakotaka kuelekea.....
Ni mpaka Shetani anapokuletea woga ndipo anapoweza kukutawala na kukugeuza mtumwa wake
Woga unamaanisha kwamba haufahamu kitu fulani namna kilivyo au kitakavyokuwa mbeleni na ndio maana tunaweza kuushinda woga kwa kujifunza neno la Mungu
Mfano mtu anapokosa hela na maarifa ya neno la Mungu, Shetani humletea hofu na kumuonesha kwamba hatoweza kufanikiwa katika maisha
Lakini kama akijifunza zaidi juu ya kitu ambacho anakihofia woga aliokuwa nao hutoweka naye hubadilika na kuwa mtu mwenye matumaini na mwanga mpya
Jaribu kufikiri mtu aliye na hofu na maisha au afya yake akakutana na mtu akamfafanulia vizuri mstari huu Mathayo 6:33 "Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake, mengine yote mtazidishiwa"
Maana ya mstari mengine yote inamaanisha fedha, afya, utajiri, furaha, upendo, matumaini, amani, utulivu
Hivyo woga huja kwa kutokulifahamu neno na namna ambavyo linavyofanya kazi katika maisha yetu ya kila siku
Woga tunaouongelea upo kwenye akili na siyo kwenye moyo ndio maana ukishamfungua macho (akili) mtu aliyekuwa na hofu fulani na kumuonesha anachokihofia hakipo mtazamo wake hubadilika
Woga unapokujia kumbuka haya:
Zaburi 118:7 "Bwana yupo upande wangu, msaidizi wangu, kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa" Adui atakapoinuka na kuleta vitu ambavyo vipo kinyume na hatma yako kumbuka Mungu yupo pamoja nawe
Kila kitu unachokifanya Mungu ndiye anakusaidia huna sababu ya kumtegemea binadamu (Waebrania 13:6) "Hata twathubutu kusema Bwana ndiye anisaidiaye sitaogopa mwanadamu atanitenda nini?
Amani tumeipewa na Yesu Kristo na ndiyo kusudi lake na amani yake siyo kama ya ulimwengu huu bali kama ya mbinguni hakuna haja ya kufadhaika wala kuwa na woga Yohana 14:27
Nguvu zako zinatokea kwa Mungu na siyo kwako mwenyewe au kwa watu wanaokuzunguka na Mungu pekee ndiye wokovu wako hakuna sababu ya kuogopa tena Isaya 12:2
Kubwa kabisa usisahau kumtafuta Bwana Mungu akuponye na hofu zako zote Zaburi 34:4
Mwanamke Thamani!
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana