Kama hukusoma sehemu ya kwanza ya makala hii ya Woga unaondoa uwepo boyfa hapa kuisoma
Katika dunia ya sasa yapo mambo mengi sana yanayoendelea mfano vita, magonjwa, njaa mara free masons niliwahi kufuatilia habari zao sana kipindi fulani
Kiukweli ni kwamba mambo haya yanatisha leo utasikia raisi wa Korea kaskazini katupa bomu la nyuklia lenye nguvu kuliko yote duniani, mara kuna ugonjwa wa ebola upo nchi za jirani, mara kuna jiwe kubwa sana angani linaelea kubwa kuliko dunia n.k
Mambo haya ukijumlisha na mihangaiko ya maisha yanasababisha watu kuwa na woga na wengine kukata tamaa ya maisha moja kwa moja
Neno usiogope kwenye Biblia limeandikwa mara 365 maana yake ni kwamba kila unapoamka Mungu anakuambia usiogope
Hata pale hofu inapokuja Zaburi 56:3 inasema "Siku ya hofu yangu nitakutumaini wewe" vile vile zaburi 34:4 inasema " Nalimtafuta Bwana akanijibu akaniponya na hofu zangu zote"
Majaribu, mateso na habari za kutisha hazina budi kutokea mwimba zaburi 23:3 anakuambia "Nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti sitaogopa mabaya, maana wewe upo pamoja nami"
Biblia inaposema Mungu yu pamoja nasi ni kwamba wakati wowote sehemu yeyote unaweza kumuita Mungu naye akafanya
Unaporuhusu tuu woga kuingia katika akili yako hapo ndipo unapompa nafasi Shetani ya kuanza kukutawala na kukuletea jambo fulani
Watu ambao wanaishi kwa kuhofia mambo fulani yatatokea kwenye maisha yao ndio wanaoishia kuyapata
Makala ya jana nilisema kwamba woga hautoki kwa Mungu ukisoma 2timotheo 1:7 Biblia inasema "Maana Mungu hakutupa roho ya woga bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi" kama hukuisoma makala hiyo unaweza gusa hapa ......
Hata kama wanasema vyuma vimekaza wewe usikubali kukiri maneno ya namna hiyo pambana na mtumaini Mungu kwa sababu yeye ndiye anayekupa mkate kila siku
Unajua unapaswa kufahamu kwamba kila mtu anayo akaunti yake ya baraka mbinguni, malipo ya watu wanaomtumainia Mungu hayatokei duniani bali mbinguni
Ndiyo maana Mungu anasema atafungua madirisha ya mbinguni na kutumwagia baraka pale ambapo tutakapompelekea zaka
Ayubu mtumishi wa Mungu alipoingiwa na hofu alisema Ayubu 3:25 "Maana jambo hilo nichalo hunipata, nalo linitialo hofu hunijia"
Mpaka Ayubu alipoingiwa na hofu ndipo mabaya yalipoanza kumpata, ukiishi maisha ya kuogopa ugonjwa fulani utaishia kuupata
Inaendelea .......
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana