WOGA UNAONDOA UWEPO - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Thursday, January 4, 2018

WOGA UNAONDOA UWEPO



Kuna njia moja tuu ya uhakika ambayo Shetani anatumia kuangamiza watu nayo ni kumpa mtu hofu juu ya jambo fulani

Una miaka 40 hujaoa/ hujaolewa/huna mtoto wala nyumba anakuambia haiwezekani tena kupata vitu hivyo papo hapo anakuonesha watu wa rika lako walivyo na kila kitu


Umeanzisha biashara zako zimekufa unasukumwa kuanzisha nyingine anakupa hofu kwa kukukumbusha yaliyopita na kukuhakikishia hata hiyo itakufa

Na alivyo mjanja anapenda sana kukuletea ile hali ya kujilinganisha na wengine, hapo ndipo anapokukata maini na nguvu maana picha anazozileta ni za waliofanikiwa saana

Unajikuta umekata tamaa, nguvu zinakuisha na unapoteza matumaini na ukishafikia hali hii ndipo anapokutawala moja kwa moja

Popote woga ulipo Mungu hayupo, Mungu anapenda majasiri kwa sababu yeye ndiye amekupatia umiliki wa kila kitu unapokuwa muoga unajiondoa katika mpango wake

Ukitaka kuamini angalia wakati Joshua, Kaleb na wale wapelezi walipotumwa kuichunguza nchi ya Ahadi kilichotokea ni kwamba ripoti ya Joshua na Kalebu ya kwamba wanaweza kuimiliki nchi ndiyo iliyopitishwa

Wale walioleta ripoti ya kuogopa na kunung'unika walikufa pale pale kwa ugonjwa wa Tauni ambao ghadhabu ya Bwana ndiyo iliyouleta

Joshua alipewa uongozi sababu ni Jasiri, ufalme wa Mungu umetekwa na wenye nguvu na majasiri

Ukisoma Yoshua 1:6a, 7a na 18b maneno haya yamejirudia "Uwe hodari na moyo wa ushujaa"

Na kuthibitisha zaidi Joshua alipewa uongozi sababu ni Jasiri, ufalme wa Mungu umetekwa na wenye nguvu na majasiri

Haikuwa raisi Daudi kuchukua kombeo kupigana na Goliathi, ule ulikuwa ni ujasiri usiokuwa na kipimo unapokuwa jasiri Mungu anabariki kazi za mikono yako

Woga unasababishwa na kutolifahamu na kulisoma Neno la Mungu, ndani ya neno kuna kila ahadi, baraka, agano na majibu ya kila kitu usichokifahamu

Akili ambayo haina neno la Mungu ni lazima Shetani atajaza neno lake, ukikosa maarifa ya neno la Mungu utajazwa maarifa ya woga ya neno la Shetani

Usikubali kukaa bila kusoma Biblia, kusoma vitabu vya kukufundisha mambo mapya ya kimaendeleo n.k

Leo hii wapo watu waliopigwa na maisha, wamekata tamaa hata Mungu akiwatembelea kwa neno lake hawaamini na wanakataa sababu ya hofu na kukatishwa tamaa 

Woga pia unasababishwa na kufikiria sana kuhusu kesho Mathayo 6:34 " Basi msisumbukie ya kesho, kesho itajisumbukia yenyewe"

Kesho inatengenezwa na mipango mizuri ya leo, badala ya kuumia akili kuhusu kesho chukua muda wa kuipangilia vyema leo

Wapo watu wanaoifikiria kesho mpaka wanakosa furaha na amani ya leo hivyo wanapoteza matumaini kabisa

Kama ilivyo kwamba imani ni sasa, hata maisha tunayoyaishi ni ya sasa hivyo kesho isikukoseshe furaha na kumtumikia Mungu sasa

Unapaswa tuu kuipangilia na kisha itajisumbukia yenyewe, kila kitu kina wakati wake maalumu

Japokuwa Yesu alizaliwa kama binadamu wa kawaida na kuishi kama sisi alisubiria mpaka alipofika miaka 30 ndio akaanza injili 

Kila jambo na majira yake na kumbuka mama yake alimuita kwenye harusi kubadili divai alichosema ni kwamba wakati wake ulikuwa haujafika (Yohana 2:4)

Inaendelea
....... 

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana