NGUVU YA MSAMAHA -VI - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Wednesday, January 24, 2018

NGUVU YA MSAMAHA -VI



Ukisoma Biblia utakutana na maandiko mengi yanayohusiana na mifupa na namna ambavyo mifupa inaweza kutabiriwa uhai

Kiroho mifupa imeambatanishwa na uhai wa mtu na ndio maana inawezekana kuiamuru Mifupa kujitengenezea mwili na mtu akapata uzima

Kama haukusoma sehemu ya tano ya mfulizo wa huu wa makala ya Nguvu ya msamaha Gusa hapa

Mtu anapokufa vitu vyote vya mwili wake huaribika lakini mifupa husalia kwa sababu mifupa ndio inaufanya mwili kuwa na maana

Ezekiel 37:1-14 inaongelea namna ambavyo Mungu alimwambia nabii Ezekiel atabirie mifupa uhai nayo ikatii akapata jeshi kubwa la watu ambalo Israel walilitumia katika vita na kushinda

Kitabu cha 2Wafalme 13:21 "Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu"

Maiti iligusana na mifupa ya Elisha na ikafufuka hivyo kiuhalisia upo uwezekano wa kufufua mtu aliyekwisha kufa/ au kutumia mifupa ya mtakatifu kufufua mtu

Mtu ambaye anashindwa kusamehe ajitesa mwenyewe na kuiharibu mifupa yake na Biblia imeliweka hili wazi katika kitabu cha Mithali 17:22 "Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa"

Kwa sababu tumeshaona kwamba mifupa ni uhai wa mtu kama mtu atakuwa anashindwa kusamehe kwa maana nyingine ni kwamba anajiuwa mwenyewe

Katika mada hii ya nguvu ya msamaha tuliona kwamba inakuwa vigumu kusamehe vitu ambavyo vimeingia kwenye mioyo lakini ni lazima tusamehe ili tuweze kusamehewa

Na siku zote kinachoujeruhi moyo ni maneno ambayo yameingia katika moyo ni bora mtu anaeutesa mwili kuliko anaetesa roho na moyo

Unaposhindwa kusamehe unatesa moyo wako na kumbuka huko ndiko chemchem za uzima hutokea 

Unajua hata kipindi Yesu anateswa hawakumvunja hata mfupa mmoja na hii ilikuwa ni muhimu sana katika ufufuko wake Yohana 19:36 "Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa"

Mwimba zaburi 34:20 yeye alisema wazi kabisa "Huihifadhi mifupa yake yote, Haukuvunjika hata mmoja" hivyo aina yoyote ile ya kuvunjika au ketenguka huwa ni shambulio la adui juu ya uhai wako

Hii inazidi kuthibitisha ni kwa nini watu wanaoanguka bafuni au chooni huvunjika kabla ya kufa kwao 

Kimsingi watu wengi wenye matatizo ya mifupa kama hayajatokana na ajali, Kiroho ni kwamba wamebeba  vitu mioyoni mwao na wameshindwa kusamehe hii ndio inapelekea wao kupatwa na magonjwa ya mifupa

Mwanamke Thamani!

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana