KILA MTU NA NEEMA YAKE - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Sunday, January 14, 2018

KILA MTU NA NEEMA YAKE


Mungu ameachilia neema yake kwa kila mtu na neema hiyo umeipata bure si kwa kuifanyia kazi
Neema huwa juu ya mtu katika hali yoyote na ukitaka kujua hili ni kweli, kuna mambo ambayo wengine ni vigumu sana kuyafanya lakini kwako ni marahisi sana

Yesu akiwa mlimani akifundisha zile Heri... moja ya heri ni ile heri masikini wa roho maana wataurithi ufalme wa mbinguni
Masikini ni mtu ambaye ana uhitaji wa jambo fulani, masikini wa roho ni mtu mwenye kiu na njaa ya neno la Mungu
Watu wengine huwa hawaelewi maana ya masikini kama ilivyotumika katika mafundisho hayo hufikiria ni yule masikini wa mwili
Umasikini umegawanyika sehemu mbili yaani umasikini wa roho na umasikini wa mwili, ukiwa masikini ni kwamba unahitajika kuongeza bidii zaidi katika kitu unachohitaji
Watu wengi hufikiri bidii ipo kwenye kutafuta hela pekee la hasha, ipo kila mahali ni mpka kwenye kulitafuta neno la Mungu 
Elia alikuwa mtu wa kawaida sana kilichofanya maombi yake yajibiwe ni bidii yake katika kuomba na kutafuta uso wa Mungu
Ukitaka kuuona upako wa Mungu ni lazima uwe na bidii sana katika kusikia, kumuomba na kulifanyia kazi neno la Mungu
Wote tumepewa muda sawa angalia wanafunzi wanafundishwa na mwalimu mmoja na mtaala ni mmoja, lakini mwalimu huwapima kwa mtihani baada ya muda
Kinachoshangaza ni kwamba wanafunzi hao hutofautiana katika matokea kutakuwa na wanaofanya vizuri zaidi, wastani na wa chini kabisa
Bidii inaachia neema na upako wa Mungu kwetu, habari ya Yusufu gerezani ni bidii yake katika kufanya kazi ndiyo iliyompa kibali
Kinachofanya mfanyakazi huyu apandishwe cheo na yule abakie pale pale ni bidii yake
Tuukubali ukweli kwamba majaribu yapo ila ni lazima tuongeze bidii zaidi kwenye kila jambo tunalolifanya
Pangilia muda wako vizuri acha kupoteza muda wako kwenye mambo ambayo siyo ya msingi

Mwanamke Thamani!

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana