Kusamehe ni kuuambia moyo wako nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba suala la namna hii halitatokea tena, kumbuka ya kwamba tunasamehe kwa sababu Mungu alitusamehe tangu mwanzo
Kama hukusoma mtiririko wa makala hii sehemu ya tatu Gusa hapa
Pindi inapotokea mmepishana kauli na rafiki yako au ndugu yako anza kuona kwamba huenda wewe ni chanzo cha kusababisha hitilafu hiyo kabla hujaanza kumlaumu na kumsema mwenzio juu ya mapungufu yake
Wote tuna mapungufu na madhaifu hakuna ambaye anaweza kusimama leo na kusema yeye ni mkamilifu asilimia 100% ila kupitia udhaifu tulio nao unatuwezesha sisi kusaidiana na kuwa wamoja
Jaribu kutafakari kama kila mtu angekuwa anaweza kufanya kila kitu mwenyewe bila msaada wa mtu yeyote jee hii dunia ingekuwaje?
Na ni mara nyingi sana baada ya kupishana kauli au kugombana watu hubeba vitu mioyoni mwao hata kama watasema kwamba wamesamehe, kwa maana nyingine ni kwamba watu hubeba vinyongo mioyoni mwao hata baada ya kuombwa msamaha
Kubeba kinyongo/kuhifadhi kitu moyoni kunamfanya mtu kujisikia vibaya na kukumbuka tukio lililopita ambalo huenda lilimuumiza na kumpa jeraha fulani moyoni kwa wakati ule na ndiyomaana Warumi14:19 inasema "Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana"
Waweza kufanya baadhi ya vitu vifuatavyo ili kuweza kujijengea moyo wa kuachilia mambo na kisamehe kila kitu
- Usikae ujaribu kujitetea kwa maneno,waache watu wengine wakutetee na kama hauna wa kukutetea huenda matendo yako hayahitaji kutetewa, kwa sababu kadiri utakavyokuwa unajitetea peke yako au kwenye uma wa watu ndivyo utakavyojawa na uchungu ndani yako
- Usiende kumuadithia mtu au watu namna ambavyo mtu fulani kakuudhi kwa sababu kila utakaporudia kusema kuhusiana na kitu hicho ndivyo utakavyokuwa unakiingiza katika kumbukumbu zako
- Usimjibu mtu vibaya kwa tuhuma zozote zile atakazotoa juu yako, hii ni ngumu lakini unapaswa kutulia kabisa na kusikiliza kile wanachokisema pasipo kuwajibu vibaya mpaka muda utakapodhihirisha ukweli wake, ili kusamehe mtu aliyekukosea unapaswa kumsamehe katika moyo wako na namna ambavyo utakavyokuwa unamtendea mtu huyo ( the way you treat him/her) haswa katika masuala ya kila siku kwenye maisha.
- Mfuate mtu huyo na mwambie kabisa nimekusamehe na baada ya hapo muombe akubali kupokea msamaha huo, kama usipofanya hivi huyo mtu hatofahamu kwamba akili yako na mtizamo wako juu yake umebadilika hivyo kila atakavyokuwa anakuona atafikiri kuna kizuizi baina yako na yeye. Mara nyingi atakuwa anajiuliza na kujishuku ni nini unawaza juu yake, lakini kama ukimtendea wema atafikiri kwamba unampaka kilemba cha ukoka, ni muhimu sana kumwambia umemsamehe na hakuna kizuizi chochote baina yenu wawili.
- Shirikiana naye kwenye mambo ya kijamii ( socialize) toka naye chakula cha usiku, nenda naye kwenye sinema, katizame naye mpira au fanya jambo lolote lile la kufanya mshirikiane hii itakufanya umsamehe naye atakuwa huru zaidi.
- Fikiria mambo yote mazuri yanayomuhusu yeye na mambo hayo yaseme au waambie watu wengine, haswa marafiki zako na pia rafiki zake.
Kuweza kusamehe aliyekukosea ni mwanzo wa kukomaa kiimani, kiakili, kimwenendo, kihisia na pia inaonesha kwamba umekua na unafahamu kuna kuteleza kwenye maisha na pindi mtu anapoteleza anapaswa kusamehewa na kuanza upya.
Mwanamke Thamani!
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana