MTAZAMO CHANYA NI USHINDI-III - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Thursday, January 4, 2018

MTAZAMO CHANYA NI USHINDI-III



Ilipoishia jana.....

Hivyo ni sawa nikisema tatizo la kukosa samaki lilisababishwa na mtazamo, Simoni na nduguze mtizamo wao uligeuka na kuamini wasingeliweza kupata samaki na ikawa hivyo 


Kama hukusoma sehemu ya pili ya makala hii gusa hapa

Twende SASA!

Yesu alikuwa na mtazamo chanya na anao hata sasa ni umilele wake, Mungu anataka watu wake wote wawe na mtizamo chanya

Tunaweza kupata mtazamo chanya kwa kumtegemea Mungu na kulipenda neno lake wakati wote

Hii ndio sababu anasema katika kitabu cha wafilipi 4:13 kwamba ninayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu

Unapomtegemea Mungu katika kila kitu naye hukupa kila kitu, hupenda tukimtukuza na kumuabudu katika roho na kweli

Ukiwa na mtizamo chanya hakuna nguvu yeyote ambayo inaweza kushindana na wewe ( positive mind belongs to God) na Mungu hashindwi hata siku moja

Kushindwa katika jambo lolote kunatokana mtu kubadili mtazamo juu ya jambo hilo yaani kuwa na mtizamo hasi katika suala husika
 feel down) hawa ni wale wenye mitazamo hasi

Katika habari hii mstati wa 11b unasema kwamba wakaacha vyote wakamfuata hii ni kwa sababu walivutiwa na Yesu 
Umeshawahi kujiuliza kwa mfano Yesu angefika kwenye ile mashua ya kina Simoni na kuanza kusema haiwezekani? 


Mtazamo chanya una tabia ya kuvutia watu siku zote utakuwa shahidi kwamba wapo baadhi ya watu mkikutana na kuongea unajisikia kuinuliwa na kujiona wa tofauti hawa wana mtazamo chanya

Lakini pia wapo ambao ukiongea nao unaishia kukasirika au kujisikia vibaya au pengine kukosa amani


Au pengine siku hizi samaki wamepotea sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa jee Simoni na nduguze wangemfuata?

Mtazamo wako juu ya dunia utapelekea mtazamo wa dunia kwako, swali kwangu na kwako Jee unaionaje dunia?

Unaiona kama sehemu ya kushinda, takatifu, yenye utajiri, sehemu unapopata milki zako, sehemu ya mafanikio, raha na upendo au sehemu ya chuki, umaskini, kukata tamaa, kuonewa, kuchosha, majonzi, shida na matatizo?


Mwanamke Thamani

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana