Ilipoishia jana....
Simoni na nduguze walichagua kutokufanikiwa kupata samaki baada ya kutupa wavu baaharini mara kadhaa na kushindwa kupata samaki
Kama hukusoma makala hii sehemu ya kwanza Gusa hapa
Twende sasa!
Katika maisha ya Ukristo unapoamua kufanya kitu na ukaona hakijaenda sawa kama ulivyotarajia haupaswi kabisa kukata tamaa wala kukuri kwamba umeshindwa
Wazo ni nguvu ambayo inasafiri na kupenyeza sehemu yeyote na muda wowote na wazo ndio linalopelekea kutokea kwa kitu chochote
Nyumba, magari, biashara, majengo makubwa na vyote tunavyoviona vimetokana na wazo fulani ambalo mtu alikuwa nalo kisha akalipangilia vizuri na kuanza kulifanyia kazi
Katika dunia hii hakuna kitu kinachotokea chenyewe, hata binadamu alikuwa ni wazo la Mungu, vitu husababishwa kutokea
Wazo unapoliwekea hisia unalipelekea katika hatua ya pili ya mtazamo na unapofanya hivi unasababisha akili yako kwenda kwenye mtikisiko mwingine katika akili ambayo haijalala huitwa hisia
Simoni na nduguze baada ya kujaribu kuvua samaki usiku kucha na kushindwa waliamua kuchagua kushindwa, kumbuka wazo ni hatua ya kwanza katika kutengeneza mtazamo
Baada ya hapo weliwekea wazo la kushindwa hisia za kutokupata samaki siku ile
Hisia zinapoanza kuwekwa kwenye vitendo au mazoea zinapelekea hatua ya tatu ya mtazamo
Hapa tunajifunza kwamba hata utendaji kazi wa Simoni na nduguze ulibadilika na hali hiyo ndio iliyosababisha wasipate samaki siku ile
Hivyo basi mtazamo alionao mtu na matokeo havitengani, vinafuatana utafanya kama vile mtazamo wako utakavyokuwa
Ngoja niende mbali zaidi Yesu wakati anakuja katika vyombo vya kuvulia samaki vya kina Simoni na nduguze Biblia haisemi kwamba aliamuru samaki washuke kutoka mbinguni waingie kwenye nyavu zao
Wala hakuamuru samaki wa baharini waingie kwenye nyavu zao bali alisema tweka mpaka kilindini
Hivyo ni sawa nikisema tatizo la kukosa samaki lilisababishwa na mtazamo, Simoni na nduguze mtizamo wao uligeuka na kuamini wasingeliweza kupata samaki na ikawa hivyo
Itaendelea........
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana