Luka 5:1-11 Soma habari hii juuya uvuvi wa samaki.
Katika habari hii tunajifunza umuhimu wa mtazamo chanya katika maisha yetu, Simoni na nduguze walihangaika usiku kucha bila kupata samaki
Hali hii iliwafanya wabadili mtazamo wao na kuamini kwamba hawawezi kupata tena samaki
Kwa maana nyingine ni kwamba walikata tamaa moja kwa moja, unapokata tamaa juu ya jambo fulani hata mtazamo wako juu ya jambo hilo hubadilika
Mtazamo ni hali ya akili (state of mind) ambayo mtu anakuwa nayo na inaweza kuwa chanya au hasi
Katika maisha hauwezi kuwa na mitazamo miwili kwa wakati ni lazima uwe hasi au uwe chanya
Kwa sababu mtazamo ni hali ya akili huweza kubadilika baada ya muda, leo hii unaweza kumuona mtu anapenda kitu fulani lakini baada ya muda akawa ndio wa kwanza kukipinga na kukikataa
Mtizama wa Simoni na nduguze ulibadilika baada ya wao kuhangaika usiku kucha pasipo kupata mafanikio mstari wa 5b unasema Bwana tumehangaika usiku kucha bila mafanikio
Hebu tafakari maneno haya...
Wewe ni Roho ambayo inaishi (enye uhai) una akili na unaishi katika mwili. Mtizamo wako ni mjumuiko wa mambo matatu muhimu ambayo ni...
- Wazo/ mawazo fulani uliyokuwa nayo kwa wakati
- Hisia ambazo unakuwa nazo
- Matendo unayoyafanya
Hivyo mtizamo ni kama duara unaanza kwa kuchagua wazo fulanina hapo ndipo mtizamo wako unaanzia
Simoni na nduguze walichagua kutokufanikiwa kupata samaki baada ya kutupa wavu baaharini mara kadhaa na kushindwa kupata samaki
Inaendelea..
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana