Wahenga wakasema "Sifa zinauwa" neno kuuwa siyo lazima roho ya mtu itoke inaweza kuwa ni vitu kuanza kwenda vibaya kama huduma kuharibika, biashara kufa, magonjwa kukuandama n.k
Kila binadamu anapenda kutambulika na kuthaminika kwa kile anachokifanya, lakini kutambulika hakupaswi kuwa kinyume na mpango na neno la Mungu
Binadamu akianza kujisifia/ kusifiwa na akalewa sifa na kumsahau Mungu sifa hizo humuuwa
Daudi rafiki wa Mungu angelikuwa anapenda sifa na kumsahau Mungu ndiye aliyemuwezesha yote haswa alipomuuwa Goliathi angalikufa mapema
Sifa anastahili kupewa nani?
Zaburi 145:3 Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana na wala ukuu wake hautambulikani, unachojisifia siyo chako ni Mungu kakupa mrudishie sifa
Ukijisifia sana mbele za watu na kuona umefanikisha huduma, biashara, mafanikio peke yako huna muda mrefu katika hilo unalojisifia litakufa
Wakati fulani niliandika Mungu hashei utukufu, kuna watu wanaowauwa watu kwa sababu wanawageuza watu hao kuwa mungu wao
Mungu hapendi wala hataki kusikia kitu chochote kinachukua nafasi yake katika maisha yetu, anapenda tumuweke namba moja katika kila kitu
2Samweli 22:4 Nilimuita Bwana astahiliye kusifiwa, hivyo nitaokoka na adui jibu linaonekana hapa anayestahili kusifiwa ni Mungu
Wapo watu wanaanzisha huduma zinafika mbali lakini wanafika sehemu wanajisahau, wanaona mafanikio yale ni juhudi zao na wanaanza kulewa sifa, jambo hili halimpendezi Mungu
Anguko la kitu chochote kile iwe ni biashara, huduma husababishwa na sifa, kukosekana kwa uongozi thabiti, kukosekana kwa hofu ya Mungu na kutojifunza mambo mapya
Binadamu anapewa pongezi, sifa anapewa Mungu Isaya 43:21 inasema watu wote niliowaumbia nafsi yangu wazitangaze sifa zangu
Habari ya tajiri mpumbavu aliyevuna mazao na akaweka ghalani, akasahau Mungu ndiye aliyemwezesha aliishia kufa usiku, kilochofanya afe ni kujisifu na kukosa shukrani kwa Mungu
Tukipenda tuishi vyema hatuna budi kufahamu mambo yanayomstahili mwanadamu na ya Mungu
Mwalimu, muimbaji, huduma, mwanamichezo ambaye anapenda sifa anguko lake hutokea mapema sana kabla ya wakati wake, ukiona mtu anafanikisha suala fulani kisha akaanza kujisifu anguko lake haliko mbali
Sifa ni kwa Bwana Yesu tuu!
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana