Katika maisha yetu kuna sehemu inafika inabidi uchague kitu kimoja na saa zingine ubadili kabisa uelekeo na urudi nyuma kwenye kitu ambacho ulikiacha
Inawezekana ulifanya uamuzi fulani ambao baada ya muda umegundua kwamba haukuwa sahihi au haujaleta matokeo ambayo ulikuwa unayategemea
Pindi wakati huu unapofika ni lazima kufanya uchaguzi ama ubakie na hali uliyonayo ambayo unajua haitakufikisha unakotaka kwenda, huku ukijipa matumaini kwamba ukifurukuta na ukijituma kwa nguvu mambo yatabadilika na itakuwa njia sahihi
Kubadili uelekeo katika maisha kinaweza kuwa kitu kigumu, kinachoumiza na kitu ambacho kitakunyima furaha kwa wakati fulani
Hii ni kwa sababu kipindi unabadili uelekeo utakumbwa na mawazo kadhaa kama nimeshakwenda sana mbali kurudi nyuma ni ngumu, watu wakiniona tena huku nakoelekea watanifikiriaje na ntaanzaje upya tena
Na mara nyingi sana kutokana na mawazo haya huwa tunabakia katika hali fulani ambayo tunajua kabisa ni mbaya na kila kitu ndani yetu kinatuambia tunaelekea katika uelekeo usio sahihi
Kunadili uelekeo ama kupiga U-turn inaweza kuwa ni kuacha kazi unatoifanya baada ya kugundua ulichokuwa unafanya awali kilikuwa cha muhimu na chenye tija kuliko kazi unayoifanya.
Inaweza kuwa ni kubadili uelekeo fulani yawezekana ulipata girlfriend/ boyfriend na ulifikiri angekuwa sahihi kwako lakini ikawa ni kinyume chake
Inaweza kuwa ni kurejea kwenye mahusiano na rafiki zako wa zamani ambao unafikiri yalikuwa mazuri lakini mkakoseana hivyo inakubidi urudi nyuma ukatengeneze upya n.k
Kitu kimoja cha uhakika ni kwamba njia ambayo siyo sahihi siku zote itakupeleka sehemu ambayo siyo nzuri
Kadiri unavyoendelea kwenda uelekeo usio sahihi ndivyo unavyozidi kupotea zaidi
Wapi ambapo utapiga U-turn kwenye maisha yako?
Mwanamke Thamani!
No comments:
Post a Comment
Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana