KWA NINI NI KUBWA KULIKO NINI! - MWANAMKE THAMANI

TV Online Channel

Tuesday, February 6, 2018

KWA NINI NI KUBWA KULIKO NINI!

Kwa  nini unafanya unachokifanya ni muhimu kuliko unachokifanya, tunapata hamu, tunajituma zaidi na tunakwenda mbali kwa sababu ya umuhimu wa kile tunachokifanya

Mtu anayetafuta fedha ili akanywe pombe na anayetafuta ili apate ada na chakula cha kulisha familia nguvu na ari ya utafutaji wao ni tofauti kabisa hii ni kutokana na sababu za kwa nini mtu huyo anahitaji fedha

Kama hukusoma na kuangalia video ya kipindi cha Mwanamke Thamani EP-2 Nguvu ya ulimi tafadhali ⇒⇒ GUSA HAPA

Sababu ya Yesu kufa msalabani kwa ajili yetu zilikuwa kubwa kuliko uhai wake na ndio maana alikuwa tayari kuutoa uhai wake  

Hatutoi vitu visivyo na thamani ili kupata vyenye thamani, bali kwenye maisha huwa tunatoa vitu vyenye thamani ili kupata vitu vyenye thamani kubwa zaidi, ndio maana sisi ni wa thamani sana mbele ya Mungu hata akawa tayari kuutoa uhai wake

Yeremia 31:3 " BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu", yaani kiufupi mapenzi ya Mungu kwetu hayakomi ni ya milele tofauti na ya kibinadamu yenye ukomo

Jaribu kufikiri sababu hizi Yesu alikufa ili kuondoa uadui baina ya mataifa Waefeso 2:14-16, 

Waefeso 5:25 " Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; hivyo alikufa ili kuirudishia ndoa uthamani wake

Warumi 5:10 " Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake, hivyo alikufa ili kutupatanisha na Mungu Baba

Warumi 5:8 "Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. hivyo alikufa ili kuuonesha upendo wa Mungu kwa wenye dhambi

Mathayo 20:28 "kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi, hivyo alikufa ili kuuonesha upendo wake kwetu sisi kwa kututumikia sisi na kutufanya wana wa mfalme

Hizo ni baadhi ya sababu na zipo nyingine nyingi lakini kikubwa cha kujifunza hapa ni kwamba tunaona sababu za Yesu kufa zilikuwa ni kubwa na zenye mantiki kuliko tunavyoona kifo chake

Nasi hapa tunajifunza neno kubwa sana kwamba kabla ya kufanya kitu tunapaswa kutafuta sababu za msingi na zenye mashiko za kukifanya, hizi ndizo zitatupa nguvu ya kuendelea hata ugumu unapokuja

Hatuna sababu ya kurukia mambo au kufanya kwa sababu fulani anafanya na anafanikiwa au anapata hiki na kile

Tupo hivi tulivyo kwa sababu ya Yeye, na sio sisi tuliomchagua bali Yeye ndiye alietuchagua na kutufanya kuwa wake, Yeye ameweka makusudi ndani yetu kwa kila mtu Yohana 15:16 "Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi;..."

Sababu za kufanya unachokifanya zinapaswa kuwa kubwa na zenye mantiki kuliko kile unachokifanya

(Why we do what we do is as more important as what we do)

Je unafanya mambo mema na kuishi kwa namna fulani ili watu wakuone na uonekane wa tofauti au unafanya ili usifiwe na watu ?

Kutumikia maono yetu kunahitaji jitihada na muda wa kutosha na kama tutakuwa tunafanya vitu kwa kusudi la kusifiwa au kufahamika tuu basi hakuna kitu kitakachotufanya tusiache tunachokifanya pindi ugumu utakapokuja

Tukifanya kitu kwa shauku ya kweli kutokea moyoni ya kubadilisha mambo, kutaka kuona mabadiliko, kusaidia wengine, kuwainua walioko chini, hata upepo wa kushindwa na kukatisha tamaa utakapovuma ni dhahiri tutaweza kusimama

Wakati unafanya kitu fanya kutokea moyoni ( do it with pure heart and not for more or other reasons)

Mwanamke Thamani "Wewe umewazidi wote"

No comments:

Post a Comment

Unaweza kutoa ushauri au kuwasiliana nasi kwa mafunzo zaidi, karibu sana